Umetangazwa mkakati wa kampeni ya kuokoa maisha ya watoto zaidi ya milioni 50 Umetangazwa mkakati wa kampeni ya kuokoa maisha ya watoto zaidi ya milioni 50 

Unicef,Who-Gavi/Chanjo:Kampeni 60 kwa nchi 50 kuokoa milioni 228 ya watu

Mkakati wa kimataifa wa chanjo unaoongozwa na Umoja wa Mataifa umezinduliwa Jumatatu tarehe 26 Aprili 2021 kwa lengo la kuwafikia watoto zaidi ya milioni 50 ambao wamekosa chanjo za kuokoa maisha dhidi ya magonjwa kama vile surua,homa ya manjano na ugonjwa wa homa ya mapafu,kwa sehemu kubwa ikiwa ni kwa sababu ya athari za janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa Bi Henrietta Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Watoto (UNICEF) amesema: “Hata kabla ya janga hilo, kulikuwa na dalili za kutia wasiwasi kwamba tulikuwa tunaanza kupoteza msingi katika vita dhidi ya magonjwa ya watoto yanayoweza kuzuilika, na watoto milioni 20 tayari wamekosa chanjo muhimu”. Kwa mujibu wa UNICEF, usumbufu uliosababishwa na janga la COVID-19 mwanzoni mwa 2020 ulimaanisha kuwa utoaji wa chanjo ulishuka kutoka chanjo bilioni 2.29 mnamo 2019, hadi dozi za chanjo zaidi kidogo ya bilioni mbili mwaka jana.  Bi. Fore ameongeza kuwa “Janga hilo limefanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi na kusababisha mamilioni ya watoto kukosa kinga. Sasa kwa kuwa chanjo ziko katika mstari wa mbele kwenye akili za kila mtu, lazima tudumishe nguvu hii kusaidia kila mtoto kupata chanjo yake ya polio na chanjo zingine. Hatuna wakati wa kupoteza. Mwelekeo uliopotea na muda inamaanisha ni kupoteza maisha.

Kwa kuunga mkono ujumbe huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus pamoja na mshirika wa GAVI, Muungano wa Chanjo duniani, wamesisitiza upatikanaji wa chanjo na uwekezaji mkubwa zaidi katika huduma ya msingi ya afya ili kusaidia misaada ya chanjo. Amesema kuwa chanji zitawasaidia kumaliza janga la COVID-19 lakini ikiwa tu watahakikisha upatikanaji wa haki kwa nchi zote, na kujenga mifumo madhubuti ya kuzitoa. Kwa mujibu wa WHO huduma za chanjo zimeanza kupata ahuweni kutoka kwenye usumbufu uliosababishwa na vizuizi vya COVID-19 mnamo mwaka  2020. Lakini utafiti wa WHO umeoneesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya nchi zilisema zimeathirika bado zinaripoti shida katika utoaji wa chanjo za kawaida.

WHO imeonya kuwa “leo hii kampeni 60 za chanjo ya kuokoa maisha katika nchi 50 zimehairishwa, na kuwaweka karibu watu milioni 228 hasa watoto katika hatari ya magonjwa kama vile ukambi, homa ya manjano na polio.”  Zaidi ya nusu ya nchi hizo 50 zilizoathiriwa ziko Afrika, wakati kampeni za ukambi au surua zimshuhudia usumbufu mkubwa, ambapo kampeni 23 za zimeahirishwa, na kuathiri watu wanaokadiriwa kuwa milioni 140. “Kampeni nyingi hizi za ukambi  zimecheleweshwa kwa zaidi ya mwaka mmoja”, limesema shirika la WHO likionya kuwa kutokukinga dhidi ya ugonjwa huu wa kuambukiza kuna hatari ya milipuko mikubwa popote ambapo watu hawajachanjwa.

Mlipuko mkubwa wa surua tayari umeripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Pakistan na Yemen kama matokeo ya mapungufu katika chanjo, limesema shirika la WHO, ikiwa ni mwanzo wa wiki ya chanjo duniani kwa 2021.  Mlipuko hii inatokea katika maeneo ambayo tayari yanakabiliwa na hali ya mizozo na usumbufu wa huduma za afya kwa sababu ya hatua zinazoendelea za kupambana na janga la COVID-19. Dunia ina chanjo za kuzuia magonjwa zaidi ya 20 yanayotishia maisha, kusaidia watu wa kila kizazi kuishi kwa muda mrefu, maisha yenye afya kama ilivyo haki yao  kulingana na mkakati wa ajenda ya chanjo  wa 2030 wa kusaidia kujikwamua kutoka kwenmye athari za COVID-19.

"Mifumo madhubuti ya chanjo itahitajika kuhakikisha kuwa watu kila mahali  wanalindwa dhidi ya COVID-19 na magonjwa mengine" Umesisitiza wavuti wa kampeni ya chanjo wa WHO na kuongeza kuwa kuna faifda kubwa kwa za kiuchumi na kuokoa maisha kwa kuwekeza katika mipango ya chanjo kwa watu binafsi, jamii na nchi .  "Kuhakikisha kila mtu anapokea chanjo anayohitaji itatoa faida ya kipekee kwenye uwekezaji na kusaidia kuiweka dunia salama kutokana na magonjwa ya mlipuko hapo baadaye."

Watoto kukosa chanjo: “Mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda wakakosa chanjo za msingi kwani janga la sasa linatishia kuathiri maendeleo ya miongo miwili ya chanjo ya kawaida” amesema Dk. Berkley, mkurugenzi mtendaji wa Gavi, Muungano wa chanjo duniani.  Ameongeza kuwa “juhudi zaidi zinahitajika ili kusaidia kujikwamua kutoka kwa janga la COVID-19 na kupambana na magonjwa ya mlipuko yajayo.  Vile vile ametaka chanjo ya kawaida ipewe kipaumbele na kulenga kufikia watoto ambao hawapati chanjo za kawaida, au watoto ambao hawajapata chanjo kabisa .

Ajenda ya chanjo ya 2030 (IA2030) inayounganisha WHO, UNICEF, GAVI na washirika wengine inazingatia chanjo katika maisha yote, tangu utoto hadi ujana na uzee.  Ikiwa itatekelezwa kikamilifu, itaepuka vifo vya watu milioni 50, kwa mujibu wa WHO  na asilimia 75 kati yao wako katika nchi za kipato cha chini na cha wastan. Umoja wa Mataifa umeelezea mshtuko wake na machungu makubwa kufuatia vifo vya watu 82 vilivyotokea baada ya moto mkubwa kulipuka katika hospitai ya Ibn Khatib inayotibu wagonjwa wa COVID-19 kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Hospitali hiyo  iliwaka moto usiku wa Jumamosi ambapo zaidi ya watu 100 wameripotiwa kujeruhiwa, vyombo vya Habari vikidai kuwa chanzo cha moto ni mlipuko wa mtungi wa hewa ya oksijeni.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq,  Jeanine Hennis-Plasschaert, ametumia taarifa iliyotolewa leo mjini Baghad kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza Maisha huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi. Mwakilishi huyo ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, ametoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua thabiti kuhakikisha janga kama hilo halitokei tena. Halikadhalika amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa msaada muhimu kwa sekta ya afya nchini Iraq wakati huu ambapo janga la Corona linazidi kushika kasi nchini humu, akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada zaidi na kusaidia mamlaka za afya kudhibiti ugonjwa huo.

Nchini Iraq, ugonjwa wa Corona umekuwa mzigo mkubwa kwa mfumo wa afya ambapo hospitali zimezidiwa uwezo na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, tangu mwezi Januari mwaka jana 2020 hadi sasa, Iraq imekuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 1 wa Corona ambapo kati yao hao 15,217 wamefariki dunia. Halikadhalika takwimu zinaonesha ongezeko la maambukizi tangu mwezi Februari mwaka huu. Mwezi uliopitam Iraq ilizindua kampeni ya chanjo dhidi ya Corona baada ya kupokea shehena ya kwanza ya chanjo za COVID-19 kupitia mfumo wa COVAX, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa chini ya uratibu wa pamoja wa WHO, ushirika dhidi ya magonjwa ya milipuko, CEPI na fuko la chanjo duniani, GAVI.

27 April 2021, 14:20