Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi nchini Tanzania kuhakikisha kwamba, wanawapunguzia watoto wao majukumu ya nyumbani ili kuwawezesha kupata muda wa kujisomea. Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi nchini Tanzania kuhakikisha kwamba, wanawapunguzia watoto wao majukumu ya nyumbani ili kuwawezesha kupata muda wa kujisomea. 

Wanafunzi Wapewe Fursa Zaidi za Kujisomea na Kujipumzisha!

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema iwapo watoto watapata muda mzuri wa kujisomea na kupumzika itawasaidia katika kuwaongezea ufaulu kwenye masomo yao na kutimiza ndoto zao kielimu. Pia, Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanafunzi wananunuliwa vifaa vyote vinavyohitajika shuleni kama sare, madaftari pamoja na kufuatilia mienendo yao kielimu.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Ruanga

Elimu ya msingi kwa wote ni lengo namba mbili la Malengo ya Maendeleo Endelevu (MDGS) linalosisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na elimu kwa wote ili kuwezesha mchakato wa maendeleo fungamani katika sekta zote. Nchini Tanzania licha ya changamoto kadhaa lakini inaendelea kujikita katika maboresho ya elimu katika ngazi mbalimbali ili kuhakikisha lengo hilo linatimizwa siyo tu kwa ujenzi wa madarasa lakini pia kuongeza kiwango cha uandikishaji shuleni na ufaulu wa wanafunzi! Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanawapunguzia watoto majukumu ya nyumbani na kuwawezesha kupata muda wa kujisomea na kupumzika. Ameyasema hayo Jumanne, Februari 23, 2021 wakati akizungumza na walimu, wanafunzi na wazazi baada ya kukagua miundombinu ya shule ya Msingi Mitope, Ruangwa. Waziri Mkuu amesema iwapo watoto watapata muda mzuri wa kujisomea na kupumzika itawasaidia katika kuwaongezea ufaulu kwenye masomo yao na kutimiza ndoto zao kielimu.

Pia, Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanafunzi wananunuliwa vifaa vyote vinavyohitajika shuleni kama sare, madaftari pamoja na kufuatilia mienendo yao kielimu. ”Wazazi tufuatilie na kujiridhisha kama watoto wetu wanafika shule na kuingia madarasani. Pia tuwe tunakagua madaftari yao na pale tunapoona hawafanyi vizuri tuwasiliane na walimu.” Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake kuendelea kusimamia vizuri shughuli za maendeleo. Kadhalika, Mkuu huyo wa wilaya ameahidi kuendelea kusimamia vizuri fedha zote za maendeleo zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya wilaya ya Ruangwa ili zitumike ipasavyo. Awali, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mitope, Margareth Mselewa alisema walimu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafunzi wote wa darasa la saba wanafaulu kwa asilimia 99. Mwalimu huyo alisema katika matokeo ya   mitihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka jana shule yao ilikuwa na jumla ya wanafunzi 21 ambao wote walifaulu na kwenda sekondari.

25 February 2021, 14:53