Watanzania wametakiwa kutambua na kuzingatia umuhimu wa kura yao hapo tarehe 28 Oktoba 2020 na kwamba, uongozi wa nchi si mahali pa kufanyia majaribio hata kidogo! Watanzania wametakiwa kutambua na kuzingatia umuhimu wa kura yao hapo tarehe 28 Oktoba 2020 na kwamba, uongozi wa nchi si mahali pa kufanyia majaribio hata kidogo! 

Uchaguzi Mkuu Tanzania 2020: 28 Oktoba! Umuhimu wa Kura Yako!

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watambue umuhimu wa kura zao watakapoenda kuchagua viongozi tarehe 28 Oktoba, 2020. “Tambua umuhimu wa kura yako. Uongozi wa nchi hautaki majaribio, unaweza kufanya majaribio kwa viongozi wa vikao vya harusi au “send-off” lakini siyo uongozi wa nchi,” amesema.: Haki, amani na utulivu ni muhimu sana!

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Wizara ya Kilimo kukutana na menejenti ya kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea ya YARA ili kuhakiki na kupata ithibati ya mbolea ya bure itakayogawiwa kwa wakulima wadogo nchini kupitia mpango wa “Action Africa”. Ametoa wito huo leo (Jumatano, Oktoba 7, 2020) alipotembelea kiwanda cha YARA kilichoko jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kampuni ya YARA kwa uwekezaji mkubwa na utekelezaji wa mpango huo wenye thamani ya shilingi bilioni 16.5. “Serikali inawashukuru sana YARA kwa kutoa mbolea kwa ajili ya wakulima nchini lakini ni muhimu ithibati ifanyike ili iruhusu mbolea iende kwa wakulima. Mpango huu ni mzuri kwa sababu unaendana na malengo ya Serikali katika kukuza sekta ya kilimo hasa uzalishaji wa chakula” Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuunga mkono wadau wanaosaidia sekta ya kilimo na amewahakikishia wawekezaji hao usalama na mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini. Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kuiga mpango huo wa YARA.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amemwomba Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bibi Elizabeth Jacobsen aanzishe Jukwaa la Biashara kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na Norway ili wapata uzoefu wa kibiashara kutoka kila upande. Kwa upande wake, Mkugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA, Bw. Winston Odhiambo amesema mpango huo utawanufaisha wakulima wadogo 83,000 nchi nzima ambapo tani 12,500 za mbolea ya zitagawiwa bure kwa wakulima wa mahindi na mpunga. Bw. Odhiambo alisema kuwa mpango huo una lengo la kusaidia uzalishaji wa chakula ambapo wanufaika pia watapewa ushauri wa bure kutoka kwa mabwana shamba wa kampuni ya YARA ili kuleta ufanisi katika uzalishaji. Naye, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bibi Jacobsen amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya dunia kuhusu uhakika wa upatikanqji wa chakula katika bara la Afrika. Wanufaika wa mpango huu ni wakulima wadogo kwa ajili ya msimu huu wa kilimo ulioanza Septemba hadi Desemba, 2020 ambao tayari wamekwisha sajiliwa kupitia mpango huo.

Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watambue umuhimu wa kura zao watakapoenda kuchagua viongozi tarehe 28 Oktoba, 2020. “Tambua umuhimu wa kura yako. Uongozi wa nchi hautaki majaribio, unaweza kufanya majaribio kwa viongozi wa vikao vya harusi au “send-off” lakini siyo uongozi wa nchi,” amesema. Ametoa wito huo Jumanne, Oktoba 6, 2020 wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kilindoni wilayani Mafia, mkoani Pwani kwenye mkutano wa kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Mafia, Bw. Omari Kipanga na mgombea wa udiwani wa kata ya Kilindoni, Bw. Salum Ally. “Nawaletea viongozi kutoka chama ambacho ni taasisi madhubuti yenye kuweka mipango yake kwenye Ilani yake ya uchaguzi. Watakuja wagombea mbalimbali hapa, wasikilizeni, wapimeni lakini tambueni umuhimu wa kura zenu,” amesisitiza.

“Viongozi wa CCM ninaowaleta kwenu wana mambo ya kueleza. Wanaeleza ni nini wamefanya katika miaka mitano iliyopita na nini watafanya katika miaka mitano ijayo. Tunatafuta kiongozi wa nchi, ambaye ametulia, anayekwenda kuongoza watu zaidi ya milioni 60 wenye dini tofauti, makabila na itikadi tofauti, tunatafuta kiongozi ambaye anaweza kuzitunza tunu za Taifa ikiwemo amani,” amesema. Amesema Watanzania wanapaswa kumchagua Rais ambaye anaweza kuzifanya rasilimali za nchi ni mali za Watanzania na siyo za hao anaowajua yeye na akawaacha Watanzania wakihangaika. “Lazima tumpe urais mtu ambaye tunamjua kwa historia, ambaye amewahi kuongoza kikundi cha watu na akapata mafanikio. Tunataka tumchague Rais ambaye anayeweza kutuletea maendeleo na siyo maneno tu. Tumebakiza siku 21 tu, tunataka kiongozi ambaye kwa dhamira yake mwenyewe anamtanguliza Mungu mbele.” Akielezea kuhusu uboreshaji wa barabara, Mheshimiwa Majaliwa amesema sh. bilioni mbili zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, ya muda maalum na madaraja kadhaa katika Halmashauri ya Mafia.

“Matengenezo ya kawaida yamefanyika katika barabara za: Kilimahewa – Mdundani (km. 2), Jimbo – Jojo (km. 10), Baleni – Kipingwi (km 6.4) na matengenezo ya maeneo korofi yamefanyika katika barabara za Ndogoni - Kimtondo; Baleni - Kipingwi, na Mwambae – Tumbuja. Pia matengenezo ya muda maalum yamefanywa katika barabara za Marimbani – Utende (km 4.2) na Baleni – Kilombero (km 8.3),” amesema. Akielezea kuhusu uboreshaji wa sekta ya maji, Mheshimiwa Majaliwa amesema Mafia kuna miradi mikubwa ya maji ambayo imepatiwa sh. bilioni 5 ili kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama. “Shilingi bilioni 5 zimetumika kwa ajili ya miradi ya mikubwa ya maji ikiwemo ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Bweni; ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Kanga; uchimbaji visima vitatu vya Kigamboni, Vunjanazi na Dawe. Na pia ujenzi wa mradi wa maji ya bomba vijiji vya Jibondo, Juani na Chole umetumia fedha hizo.” Amesema kiasi kingine cha sh. milioni 66 kimetumika kwenye miradi ya ukarabati wa miundombinu na kuboresha mtandao wa maji ya bomba katika kijiji cha Kilindoni. Amesema zilitolewa pia sh. bilioni 2 ili kutandika mabomba chini ya maji kwenda Jibondo. Kuhusu sekta ya elimu, Mheshimiwa Majaliwa amesema kiasi cha sh. bilioni 1.5 kimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha VETA ambacho ujenzi wake hadi sasa umefikia asilimia 40. “Ujenzi wa chuo hiki unaendelea; ukikamilika, tunataka vijana wa Mafia waende pale wakajifunze ufundi uashi, ujenzi au utaalamu wa kompyuta,” amesema.

07 October 2020, 16:07