Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19.Ni wito wa nguvu katika Siku ambayo UN inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa siku ya Wazee kimataifa. Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19.Ni wito wa nguvu katika Siku ambayo UN inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa siku ya Wazee kimataifa. 

Siku ya Kimataifa ya Wazee.Wao ni urithi usiotakiwa kupoteza

Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19.Kulingana na mada ya maadhimisho ya mwaka huu, lazima pia tuchunguze jinsi janga hilo linavyoweza kubadilisha jinsi tunavyo shughulikia umri na uzee katika jamii zetu.Kupanua fursa kwa wazee na kuongeza ufikiaji wao wa afya,malipo ya uzeeni na ulinzi wa jamii ni muhimu.Ni katika fursa ya kuadhimisha Siku ya Wazee duniani Mosi Oktoba.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana  Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa tarehe 1 Oktoba 2020 katika fursa ya kuadhimisha miaka 30 ya Siku ya Wazee duniani amesema “Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19”. Ni katika muktadha wa  kutathimishi athari mbaya na kali ambazo janga la COVID-19 limesababisha kwa wazee ulimwenguni na sio tu kwa afya zao, bali pia juu ya haki zao na ustawi wao. Katika siku hii inayoangazia kwa namna hiyo wazee Bwana Guterres amesema “Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19. Kulingana na mada ya maadhimisho ya mwaka huu, lazima pia tuchunguze jinsi janga hilo linavyoweza kubadilisha jinsi tunavyoshughulikia umri na uzee katika jamii zetu. Kupanua fursa kwa wazee na kuongeza ufikiaji wao wa afya, malipo ya uzeeni na ulinzi wa jamii vitakuwa muhimu.”    

Katika ufafanuzi wa siku hii aidha Bwana Guterres amesema wakati ulimwengu unapotafuta kupona vizuri kwa pamoja, lazima wanadamu wafanye juhudi za pamoja katika kipindi cha miaka kumi kilichopewa jina muongo mmoja wa kuzeeka kwa afya yaani mwaka 2020 hadi 2030 kuboresha Maisha ya wazee, familia zao na jamii, “uwezo wa wazee ni msingi mzuri wa maendeleo endelevu. Zaidi ya hapo awali, lazima tusikilize sauti zao, mapendekezo na mawazo ili kujenga jamii jumushi na rafiki.”  Naye Claudia Mahler ambaye ni Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu wazee kufurahia haki zote za binadamu, ametoa wito kuwapa kipaumbele wazee katika kipindi hiki cha dunia kurejea katika hali yake baada ya COVID-19 na hata baada ya hapo.  Kupitia ujumbe wake alioutoa tarhe Mosi Oktoba 202  kuhusu siku hii ya kimataifa ya wazee Bi Mahler amesema wazee wana majukumu kadhaa muhimu katika jamii ikiwemo kulea, kujitolea na viongozi wa jamii. Mchango muhimu wa wazee katika kushughulikia janga ikiwemo kama wahudumu wa afya na walezi, mara nyingi hupuuzwa na kunatakiwa kutambuliwa

Naye Rais Sergio Mattarella akikimbuka Siku ya Wazee kimataifa  ambayo imefikia mwaka wa thelathini tangu kuanza kwake amesema “Mara nyingi ni wazee ambao hutufundisha kuheshimu maadili, kutukumbusha mizizi yetu, kutuonyesha njia ya utu, kujitolea, ukarimu. Mfano wao katika wakati huu mgumu ni urithi wa ajabu ambao hatupaswi na hatutaki kupoteza”. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliazimia siku hii kwa kutaka kufahamisha Mataifa na maoni ya umma suala la kuzeeka kwa idadi ya watu na hitaji la msaada na utunzaji wa wazee hao lakini pia na uwezo wote ambao vizazi vilivyokomaa zaidi vinaweza kuelezea kwa niaba ya jaamii na jumuiya . Siku inaleta  maana maalum sana leo  hii amesisitiza Rais Matarella kwamba mbele ya janga ambalo linafanya ulimwengu wote kuwa na shughuli nyingi na ambayo hadi sasa limeathiri sana wazee, kuvunja maisha na upendo na kuonesha  wazi  udhaifu wa afya zao, kuwalazimisha kuwa katika visa vingi  hasa vya kutengwa na, kwa maana hiyo  hatari ya kutengwa sana na ubaguzi. Rais Matarella ameseongeza kusema “Jamuiya zote zinahitaji mchango wa vizazi tofauti. Kila kizazi kina mchango muhimu wa kuleta faida kwa wote. Jambo la kusikitisha, katika miezi ya hivi karibuni, tumeshuhudia mateso na kifo cha wazee wengi. Na mahalia mabapo virusi vimeenea sana au au mahali ambapo hali ya umaskini ilikuwa mbaya zaidi, uchungu ulikuwa mkubwa zaidi”.

 

 

 

 

01 October 2020, 13:44