Vatican News
Shule:Tarehe 14 Septemba 2020 Nchini Italia shule zimefunguliwa kwa wanafunzi milioni 5,6. Shule:Tarehe 14 Septemba 2020 Nchini Italia shule zimefunguliwa kwa wanafunzi milioni 5,6.  (ANSA)

Italia:Wanafunzi warudi shuleni licha ya maambuzi ya covid-19!

Wakati mwaka wa masomo unafunguliwa nchini Italia tarehe 14 Septemba 2020,wazazi wa watoto wenye ulemavu wanaomba uhakika wa mfumo maalum wa elimu binafsi kwa ajili ya watoto wao.Ni vyama vya Angsa na Coordown waliobaini ukosefu wa mpango huo sehemu nyingi za mikoa katika kipindi hiki cha covid-19.Wakati Shule za Congo DRC zimefunguliwa mwezi uliopita wakizingatia kanuzi za mamlaka ya afya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hatimaye mwaka wa shule nchini Italia umefunguliwa kwa kuanza na Kaskazini huko Bolzano lakini katika sehemu kubwa ya mikoa, pamoja na ufunguzi wa shule Jumatatu 14 Septemba kuna matatizo. Wanafunzi 254 elfu ni walemavu ambao wameanza (karibia asilimia 3 ya jumla watotot wote wa shule) na wazazi wengi wanaogopa sana kuhusiana na ongezeko la hatua za kisheria ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya corona na kuishia kutengwa au kutelekezwa kwa watoto wao. Hizi ni taarifa zilizobainisha na vyama vya Angsa na Coordown ambavyo kwa mujibu wao vinabainhsa  juu ya ukosefu wa mpango maalum wa watoto katika ufunguzi wa mwaka wa shule katika  hemu nyingi za mikoa mkwenye kipindi hiki kigumu cha covid-19.

Kwa mujibu wa kanuni zilizoweka hata hivyo zinaeleza  kuwa ikiwa mtoto, mwanafunzi au mhudumu atabainisha kuwa na virusi, ni Kitengo cha Afya cha mkoa watatathimini ikiwa waweke wanafunzi wote karantini  katika darasa moja na wahudumu wote wa shule. Kufungwa kwa shule au sehemu moja ya shule hiyo intathiminiwa kulingana na idadi ya kesi zilizothibitishwa ndani ya jumuiya ya shule. Na zaidi ikiwa mwanafunzi ataonyesha dalili akiwa shuleni, wanashauri aweze kutengwa katika eneo lilioandaliwa na taasisi hiyo na kusaidiwa na mtu mzima ambaye atakuwa amevaa barakoa za kitibabu.

Wakati huo huo hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imeitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kufungua shule ili wanafunzi wanaofanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari waweze kuendelea masomo yao licha ya kuwepo kwa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo taifa hilo la maziwa makuu.

Shule nchini DRC zimefunguliwa mwezi uliopita huku mamlaka ikizingatia kanuni zilizopendekezwa na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, (WHO), la kuhakikisha kuna huduma za kujisafisha ikiwemo maji ya kunawa mikono na sabuni ya mara kwa mara,  kuvaa barakoa  sambamba, na umbali wa mita mbili kati ya wanafunzi iwe ni darasani au wakati wa michezo. Katika shule zilizofunguliwa hivi karibu wanaendelea kuhakikisha na kuheshimu umbali wa kutochangamana ili kuepusha maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo hadi sasa havina tiba wala chanjo..

14 September 2020, 13:07