Kwa mujibu wa UNESCO  nusu ya watoto katika ufunguzi wa mwaka mpya wa shule ndiyo wataweza kuanza shule kutokana na shida ya covid-19 na sintofahamu. Kwa mujibu wa UNESCO nusu ya watoto katika ufunguzi wa mwaka mpya wa shule ndiyo wataweza kuanza shule kutokana na shida ya covid-19 na sintofahamu. 

UNESCO:shule zitafunguliwa zikiwa na nusu ya watoto darasani!

Kwa mujibu wa shirila la elimu, syanasi na utamaduni Unesco limesema kuwa nusu watoto katika ufunguzi wa mwaka wa shule ndiyo watakaoweza kuingia madarasani kutokana na sintofahamu iliyogubika maeneo mengi ya dunia sasa hivi kutokana na vizuizi vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 na sababu nyinginezo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema muhula mpya wa masomo alianza Agosti hadi Oktoba mwaka huu, theluthi moja ya wanafunzi bilioni 1 nukta 5 wa shule za awali hadi sekondari ndio wamejiandaa kurejea shuleni. UNESCO hata hivyo katika taarifa yake iliyotolewa jijini Paris, Ufaransa, imesema ni nusu yao hao tu ndiyo watakaoweza kuingia madarasani kutokana na sintofahamu iliyogubika maeneo mengi ya dunia sasa  hivi kutokana na vizuizi vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 na sababu nyinginezo.

Kwa mujibu wa  UNESCO inasema nusu hiyo ambayo ni sawa na watoto milioni 488 wataweza kujifunza kwa mbinu mchanganyiko ikiwemo kujifunzia wakiwa nyumbani au kuingia madarasani, “ingawa idadi kubwa bado inasubiri muongozo wa kile wanachotarajia wakati siku za kufungua shule zimekaribia.” Shirika hilo linasema kuwa hali hii ni tatizo kubwa ikizingatiwa ukosefu wa usawa utokanao na wanafuzi kusomea majumbani, hali itakayoathiri jamii zilizo hatarini zaidi.

Akizungumzia sintofahamu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema “Janga la elimu linasalia kuwa tatizo kubwa, vizazi kadhaa vinakumbwa na tishio la shule kufungwa, hali inayotia hofu kwa mamilioni ya wanafunzi na imedumu kwa miezi kadhaa. Hii ni dharura kwa elimu duniani.”  Leo hii, wanafunzi duniani kote wamepoteza wastani wa siku 60 za masomo shuleni tangu vizuizi vya COVID-19 vianze mwezi  Februari na Machi mwaka huu. UNESCO inasema katika mazingira kama hayo suala la utoro shuleni, kupungua kwa ubora wa elimu na madhara yake kiuchumi na kijamii ni bayana.

Kwa mantiki hiyo, shirika hilo linatoa wito kwa mamlaka kubaini haraka hatua bora za kuchukua ili watoto waweze kurejea shule salama huku afya ya wanafunzi na wafanyakazi ikizingatiwa. Tayari UNESCO kwa ushirikiano na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na mpango wa chakula duniani, WFP na Benki ya Dunia wameandaa muongozo wa kusaidia nchi kufungua tena shule na vyuo vya elimu ya juu.

02 September 2020, 13:13