Vatican News
Mkutano wa kimataifa ukiangazia Wanawake na Covidi-19 uliofanyika tarehe 31 Agosti 2020 kwa kuudhuriwa na viongozi wakuu wa umoja wa Mataifa. Mkutano wa kimataifa ukiangazia Wanawake na Covidi-19 uliofanyika tarehe 31 Agosti 2020 kwa kuudhuriwa na viongozi wakuu wa umoja wa Mataifa. 

UN:Mkutano wa wanawake:Ni wakati wa kujumuisha sauti kukabili pengo la usawa!

Ni wakati wa kutambua sauti za wale wasiojumuishwa na wale ambao mahitaji yao ndiyo malengo ya hatua za wanaharakati katika nyanja zote.Haya ni maoni ya mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake(UN Women),Bi.Mlambo-Ngcuka.Janga la COVID-19 limeanika na kuongeza vikwazo vinavyowakabili wanawake katika kufikia haki zao na uwezo wao ìamesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Tarehe 31 Agosti  amefanya mkutano wa kimataifa na mamia ya wawakilishi kutoka asasi za kiraia kumulika suala la wanawake baada ya mkutano wa kila mwaka kuhusu hali ya wanawake duniani, mkutano ambao kila mwaka hufanyika mwezi Machi lakini uliahirishwa kutokana na janga la corona au COVID-19 mwaka huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameudhuria ambapo Mkutano huo umefanya kwa njia ya mtandao kwa kujikita kwa dhati  na mada ya ‘wanawake na COVID-19’. Mkutano huo umehudhuriwa pia na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina J. Mohammed na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka ambaye amezungumzia suala la kuwajumuisha wanawake na wasichana kutoka kila kona ya dunia na suala zima la uongozi.  Katika taarifa yake katika mkutano huo Bi.Ngcuka amesisitiza kwamba, “ni wakati wa kutambua sauti za wale wasiojumuishwa na wale ambao mahitaji yao ndio malengo ya hatua za wanaharakati katika nyanja zote.”   Ameongeza kuwa asasi za kiraia na harakati za wanawake ni washirika wakubwa katika juhudi za kubaini na kukabiliana na pengo la usawa ambalo limeongezeka sana wakati wa janga la COVID-19.

Naye Katibu Mkuu Antonio Guterres amesisitiza kwamba, “janga la COVID-19 limeanika na kuongeza vikwazo vinavyowakabili wanawake katika kufikia haki zao na uwezo wao.”  Ameeleza kwamba hatua kubwa zilizopigwa zimerudi nyuma na itachukua miaka na hata vizazi kurejea natika mafanikio hayo lakini kwa kuchukua hatua maalum inawezekana.  Kwa mantiki hiyo Bwana. Guterres amesema “Wakati wanawake wana uwezo wa kufanya maamuzi, ni ushindi kwa kila mtu” akisistiza ujumuishwa wa kundi hilo katika ngazi ya maamuzi.  Katika taarifa yake pia Katibu Mkuu amesema kwamba kulinda haki za wanawake na wasichana wakati huu wa janga la corona ni kipaumbele cha hali ya juu cha Umoja wa Mataifa. Amefafanua kwamba katika awamu ya kwanza, kipaumbele ni kuchukua hatua za afya, katika hatua ya pili ya kukabiliana na janga hilo, lengo ni kupunguza athari za kuchumi na kijamii zilizosababishwa na mgogoro huu wa kimataifa n ani kuanzia kwa uwekezaji kwa wanawake wanaofanyakazi katika sekta rasmi na zisizo rasmi.

Bwana Guterres amesisitiza kwamba katika awamu ya tatu ya hatua, kipaumbele ni kujikwamua vyema kutoka kwenye janga hili na kujenga mustakhabali uliobora. Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga hili linaonyesha kwamba karne ya mfumo dume imesambabisha wanaume kuitawala dunia kwa utamaduni ambao unawaumiza wanawake, wanaume, wasichana na wavulana. Katibu Mkuu ameomba kwamba katika dharura ya mgogoro huu wanawake wanapaswa kuwa na fursa sawa kwa uongozi na uwakilishi.  Kwani amesema hivi sasa ni salimia 8 tu ya viongozi wakuu wan chi na serikali ndio wanawake.  Wanawake wabunge ni chini ya asilimia 25 ya wabunge wote duniani na ingawa asilimia 70 hadi 90 ya wahudumu wote wa afya ni wanawake, chini ya theluthi moja ya wahudumu hao ndio wanaoshiriki katika ngazi ya maamuzi yanayoathiri katika sekta hiyo

01 September 2020, 16:54