Janga hilo linaendelea kushika kasi na katika wiki sita zilizopita idadi ya wagonjwa imeongezeka takriban mara mbili Janga hilo linaendelea kushika kasi na katika wiki sita zilizopita idadi ya wagonjwa imeongezeka takriban mara mbili 

WHO:Ikiwa tunataka kushinda covid-19 maamuzi magumu yafanyike!

Tarehe 30 Julai 2020 itakuwa ni miezi sita kamili tangu shirika la Afya ulimwenguni WHO lilipo tangaza janga la COVID-19 kuwa dharura ya kimataifa inayotia hofu kubwa.Ni lazima kuchagua maamuzi magumu ikiwa tunataka kupambana na janga hili.Janga hilo linaendelea kushika kasi na katika wiki sita zilizopita idadi ya wagonjwa imeongezeka takriban mara mbili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Serikali kila mahali zinapaswa kuchukua mtazamo madhubuti zaidi ili kukomesha maambukizi endapo zinataka kuepuka kufanya upya hatua za kusalia majumbani kutokana na janga la corona au COVID-19. Ni kwa mujibu wa  taarifa la shirika la afya duniani WHO. Ujumbe huo umetolewa  na WHO mjini Geneva Uswisi ambapo mkuu wa masuala ya dharura wa shirika hilo Dkt. Mike Ryan amependekeza vita dhidi ya COVID-19 vitumie nyenzo maalum kwa ajili ya upasuaji ili kuhakikisha matokeo mazuri kwa wagonjwa. Mapendekezo hayo yamekuja wakati ambapo WHO imetangaza karibu watu milioni 16 kuwa wameambukizwa corona kote duniani huku vifo vikiwa ni zaidi ya 640,000.

“Ni suala linaloeleweka kwamba hakuna nchi yoyote duniani ambayo imepitia hatua za kufunga kila kitu inayotaka kurudi tena kwenye hali hiyo. Nani anayetaka kurudi huko, kwani kuna athari kubwa sana za kiuchumi na athari zingine.” Amesema Dkt. Ryan na kuongeza kuwa “Endapo utaelewa mwelekeo wa maambukizi na kuwa makini katika uelewa wako kuhusu ugonjwa huu unaweza kuchukua hatua muafaka za kuukabili. Ni kama katika upasuaji ukifikiria watu waliofanyiwa upasuaji wa ubongo, wapasuaji mara nyingi hutumia darubini ili waweze kushughulikia pale panapohitajika tu. Na tumeona idadi kubwa na kuimarika kwa idadi ya wanaopona baada ya upasuaji wa ubogo, kwa sababu tuko makini zaidi na upasuaji huo.”

Akirudia kusisitiza haja ya watu kuendelea kuwa makini na waangalifu dhidi ya janga hili na umuhimu wa haja ya kuongeza kasi ya ufuatiiaji wa wagonjwa na waliokutana nao,  mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros amesema Alhamisi wiki hii  tarehe 30 Julai  itakuwa ni miezi sita kamili tangu shirika hilo la afya kutangaza janga la COVID-19 kuwa dharura ya kimataifa inayotia hofu kubwa.  “Hii ni mara ya sita kutangazwa dharura ya afya ya kimataifa chini ya taratibu za afya za kimataifa, lakini hili ni janga baya zaidi” ameongeza kuwa janga hilo linaendelea kushika kasi na katika wiki sita zilizopita idadi ya wagonjwa imeongezeka takriban mara mbili. Amezitaja nchi za Cambodia, New Zealand, Rwanda, Thailand, Viet Nam, visiwa vya Pasifiki na Caribbea ni maeneo ambako wamejitahidi kuzuia mlipuko mkubwa kwa kuheshimu na kuzingatia hatua za kuzuia maambukizi kwa uangalifu na umakini mkubwa. Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Dkt. Tedros pia amezipongeza Canada, China, Ujerumani na Jamhuri ya Korea kwa kuweza kudhibiti milipuko mikubwa iliyowakabili.

Mkuu huyo wa WHO amesisitiza kwamba kujizatiti kuudhibiti ugonjwa huo kwenye vyanzo vyake ni muhimu katika kukomesha maambukizi Pamoja na “utayari wa kufanya maamuzi magumu ili kuhakikisha sisi wenyewe tuko salama na wengine wako salama. Ingawa dunia yetu imebadilika nguzo za msingi za hatua za kupambana na janga hili ziko pale pale, uongozi wa kisiasa, kutoa taarifa, kushirikisha na kuzisikiliza jamii. Pia hatua za msingi zinazohitajika kukomesha maambukizi na kuokoa maisha hazijabadilika. Tafuteni wagonjwa, wapimeni na kuwahudumia na fuatilieni na kuwaweka katika karantini waliokutana nao." Amekumbusha kwamba hakuna njia moja pekee ambayo inatosheleza kudhibiti COVID-19 na ametoa wito kwa watu kuchukua tahadhari na kujitenga umbali unaotakiwa na watu wengine, kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko na hasa maeneo ya ndani. Mahali ambako hatua hizi zinazingatiwa idadi ya wagonjwa imekwenda chini na ambako hazizingatiwi idadi ya wagonjwa imekwenda juu.” Msaada uliotolewa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Norway umewezesha watoto katika maeneo ya kusini mwa Madagascar kuweza kupata elimu katika mazingira yenye staha.

Maeneo hayo ni wilaya za Anosy, Androy na Atsimo Andrefana ambako hali ya maisha ni duni ambapo msaada huo uliotolewa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 umezaa matunda. Serikali ya Norway ilitoa dola milioni 21 za kutekeleza mradi huo wa msaada uliokuwa katika maeneo matatu, ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilipatia mafunzo walimu 11,364 sambamba na vifaa vya kufundishia kwa shule 4,000. Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP lenyewe lilihusika na ujenzi wa majengo 350 ya kantini katika shule 70,520 huku shirika la kazi duniani, ILO likijenga vyumba 158 vya madarasa na ukumbi wa kulia chakula katika shule 97. Mkurugenzi wa elimu ya msingi katika kituo cha Amphany nchini Madagascar Emilie Tamara anasema kuwa, “katika nchi yetu, kiwango cha watoto kumakinika kinaongezeka. Wale ambao walikuwa watoro shuleni sasa wamerejea, hii ni kwa sababu ya mbinu bora za kufundishia. Walimu na wafanyakazi wengine wa shule wamepatiwa mafunzo ya kina. Shule yetu pia imepata majengo mapya, madawati mapya vifaa vipya vya kufundishia, na pia tuna kantini ya shule ambayo ni kivutio pia kwa watoto kufika shuleni.”

Mkurugenzi huyo wa elimu ya msingi anaenda mbali kusema kuwa kiwango cha ufaulu kwenye mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kimepanda kutoka asilimia 64 mwaka 2017 hadi asilimia 98 mwaka 2019. Halikadhalika kiwango cha kurudia elimu ya msingi kwenye maeneo hayo kimeshuka na kufikia asilimia 26 ikiwa ni chini ya wastani wa kiwango cha kitaifa cha asilimia 28.4. Akizungumzia msaada wao, Afisa kwenye ubalozi wa Norway kwenye mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo,  Andreas Danevad amesema kuwa, “elimu ni moja ya vipaumbele vikuu vya Norway kwenye ushirikiano wa kimataifa. Inafikia karibu theluthi mbili ya ushirikiano wetu wa kimaendeleo na Madagascar. Tunafurahia sana kuweza kuendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili hatimaye Madagascar iweze kufanikisha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambalo ni elimu bora.”

28 July 2020, 17:52