WASI WASI WA WHO KUFUATIA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI  AMBAYO BADO YANAENDELEA KUENEKA KILA KONA YA DUNIA WASI WASI WA WHO KUFUATIA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI AMBAYO BADO YANAENDELEA KUENEKA KILA KONA YA DUNIA 

COVID-19:Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani Afrika kuongezeka!

Nchi zinazoongoza kwa maambukizi ya virusi kwa sasa ni Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribean.Katik bara la Afrika idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani imeanza kupindukia.WHO imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzuka upya kwa mlipuko wa virusi vya corona barani Ulaya.

Na Sr.Angela -RwezaulaVatican

Amerika ya kusini na visiwa vya Carribean imekuwa na pigo kubwa zaidi ya janga la virusi vya corona kifikia mwisho wa wiki iliyopita. Nchini Venezuela bado wanaendelea kuwa karanti kwa siku nyingine 15 zaidi. Nchini Mexico kwa mara ya kwanza wamefungua makanisa yao baada ya miezi minne huku wakiendelea  kufuata sheria za kuvaa barakoa na wa kukaa na umbali. Ulaya na Uingereza bado wanaendelea na sheria za karantini kwa watu ambao wanatoka nchini Usihipania. Hata hivyo maambukizi mapya bado yanaongezeka. Nchini Canada maambukizi zaidi yameanza kuwapo kati ya watu wenye umri wa miaka 20 hadi 40. Marekani imeanza  kupungua kidogo kutoka maambukizi ya watu 60,000 hadi kufikia 55,000 katika ripoti ya masaa 24 ya tarehe 26 Julai 2020. Hata hivyo mchakato wa kutafuta chanjo nchini Marekani bado unaendelea kwa kasi ambapo taarifa inasema kuwa siku  za hivi karibuni watatoa matokeo ya majaribio katika maabara.

Wakati huo huo zaidi ya watu 800,000 wameambukizwa virusi vya corona barani Afrika: Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani Afrika imepindukia watu 800,000. Wakati huohuo WHO imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzuka upya kwa mripuko wa virusi vya corona barani Ulaya. Kwa mujibu wa taarifa ya wakala wa afya wa Jumuiya ya Afrika inayosimamia vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa barani humo, CDC, Afrika Kusini ndio inaongoza kwa kuwa na nusu ya idadi iliyotajwa ya watu walioambukizwa katika jumla ya mataifa 54 yaliyopo barani Afrika.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba viwango vya maambukizi vinaongezeka kwa kasi katika mataifa mengine barani humo na imeitaja Kenya iliyo na zaidi ya watu elfu 16 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona mpaka sasa. Bara la Afrika limekuwa likiwekewa hofu kabla ya hata kuripotiwa maambukizi ya kwanza barani humo yaliyothibitishwa mnamo Februari 14. Katika tamko lake kuhusu hali ya dharura ya afya duniani kote mnamo mwezi Januari, Shirika la afya duniani WHO lilisema bara la Afrika lingeathirika zaidi na janga la corona kutokana na kuwepo mifumo duni ya huduma za afya.Wataalamu wa afya wametahadharisha kwamba huenda janga la COVID -19 likaendelea kuwepo kwenye baadhi ya nchi za Afrika kwa muda mrefu.

Wakati huo huo shirika la afya duniani WHO limeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzuka upya kwa mripuko wa virusi vya corona barani Ulaya baada ya Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Austria kutangaza sheria kali za kuvaa barakoa na kusisitiza juhudi za kuwapima watu kwa wingi. Bara Ulaya linajumuisha humusi moja ya maambukizi ya zaidi ya milioni 15 ya virusi vya corona kote duniani na linaendelea kuwa eneo lililoathirika zaidi kutokana na watu waliokufa kutokana na COVID -19. 

Bara Ulaya lina watu 207, 118 waliothibitishwa kuwa wameambukizwa virusi vya corona kati ya jumla ya watu 630 000 walioambukizwa kote duniani tangu kuzuka mara ya kwanza kwa virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka jana. Shirika la afya duniani WHO limetaja kuongezeka kwa maambukizi kote barani Ulaya katika muda wa kipindi cha wiki mbili zilizopita na limesema hatua kali zaidi huenda zitahitajika kukabiliana na kuenea kwa virusi nya corona.

27 July 2020, 15:06