Vatican News
Daktari akiwa anavua baada ya kutoka chumba cha wagonjwa mahututi wa virusi vya covid-19 Daktari akiwa anavua baada ya kutoka chumba cha wagonjwa mahututi wa virusi vya covid-19  (ANSA)

Covid-19#mtazamo wa hali katika ulimwenguni!

Mji wa Wuhan haukurekodi kifo hata kimoja kwa mara ya kwanza tarehe 7 Aprili wakati nchini Marekani vifo kwa masaa 24 vilikuwa ni 2000.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nchini china Jumanne 7 Aprili 2020 katika mji wa Wuhan kwa mara ya kwanza hapakuwapo na vifo vilivyo rekodiwa vya virusi vya corona. Wakati huo huo nchini Marekani, vifo vilivyorekodiwa vilikuwa 2000. Rais Trump ameshutumu na Shirika la Afya duniani kwamba wamependelea nchini China na ametishia kusitisha michango yake.

Nchini Ufaransa: Baada ya Italia na Uhispania, nchini Ufaransa umezidishwa vifo 10,000 na sasa wameweka sheria kali katika baadhi ya miji. Na huko Uingereza, waziri wake, Bwana Boris Johnson bado anaendelea kutibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na hali yake ni thabiti baada ya kupewa oksijen kutokana na ugonjwa wa mapafu covid-19.

UE:Umoja wa nchini za Ulaya washindwa kuwa na makubaliano kati ya mawaziri wa fedha katika mkutano wa  27 uliofanyika tarehe 7 Aprili 2020 ili kubaini mpango wa msaada kamili wa Ulaya ambao wamekuba na kuathirika sana na mlipuko wa virus vya corona. Waliangazia kuweka mtazamo wao katika nafasi ya kugawana madeni (eurobonds au coronabonds) lakini ilishindikana hivyo Mkutano mwingine utafanyika  siku ya Alhamisi.

Iraq:Nchi ya Marekani na Serikali ya Iraq wataanza mchakato wa makubaliano katikati ya mwezi Juni ili kuona juu ya uwezekano wa uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika nchi  hiyo kwa wakati ujao.

Msumbiji: siku ya Jumatatu na Jumanne tarehe 7-8 Aprili 2020 kumekuwapo na mashambulizi ya kijihad dhidi ya vijiji  vya kaskazini mwa nchi. Ni miaka miwili sasa vikundi vya kiitikadi kali ya kiislam inasambaza hofu kubwa katika nchi hiyo. Migogoro hiyo imekwisha sababisha vifo vya raia 900 na kusababisha watu 150,000 kurundikana pamoja kwa sababu ya mashambulizi hayo.

Tabianchi: Hali ya hewa inakabiliwa na hali ya hewa ya joto Kali katika Bahari kuu ya kizingiti cha Australia. Zaidi ya miezi ya majira ya joto imerekodiwa hali  ambayo haijawahi kuonekana hapo awali. Kwa hakika inatishia napia tishio la urithi wa ulimwengu,(UNESCO)

Ukrane: Moto mkali unaendelea kurarua na huharibu msitu katika ukanda mwekundu wa mkoa wa Chernobyl nchini  Ukranine.

Umoja wa Mataifa: tarehe 8 Aprili 2020 ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa unafanya siku ya Kimataifa ya Waromania na Wasinti. Lengo la siku hii ni kutaka kutambua kuwawatu hawa wanapaswa kuheshimiwa , kulindwa na kuthamaniwa utu wao. Mara nyingi watu hawa wanatengwa na kunyanyaswa kwa mateso makali na kunyimwa haki zao msingi.

08 April 2020, 15:29