Vatican News
Rais Kiir wa Sudan Kusini amemtangaza Mache kuwa makamu wake na shukrani kwa Papa Francisko na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kutokana na kuongoza mchakato wa majadiliano hadi kufikia hatua hiyo Rais Kiir wa Sudan Kusini amemtangaza Mache kuwa makamu wake na shukrani kwa Papa Francisko na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kutokana na kuongoza mchakato wa majadiliano hadi kufikia hatua hiyo  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Hatimaye Kiir ameunda serikali ya Muungano!

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameunda serikali ya muungano ambapo Riek Machar anakuwa makamu wake.Kiir anashukuru Papa Francisko kwa kuwasindikiza kwa sala na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambayo imenuia kusaidia kuunda muungano huo na zaidi kwa njia ya mchakato hadi kufikia mkataba wa kusitisha vizingiti katika kuelekea aman ya nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ninashukuru Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa kuanzisha majadiliano huko Roma. Ndivyo alivyoanza Rais wa Sudan Kusini Bwana Salva Kiir, ambaye tarehe 24 Februari 2020 ametangaza uundaji wa serikali ya muungano wa Taifa kwa kumtangaza kiongozi Riek Machar aliyekuwa mpizani wake kuwa makamu Rais. Katika hafla ya uundaji wa serikali mpya kati ya walioshiriki ni wawakilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambapo Kiir wamewapongeza kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa safari ya majadiliano uliofanyika Roma na kuruhusu kushirikisha upande wa nguvu za upinzani ambao hadi wakati ule hawakuwa katika mchakato kuelekea amani kwa namna ya pekee: SSOMA Thomas Cirillo, Paul Malong na  Pagan Amun. Aidha ameendelea kusema kuwa: "Ninapenda kuwapongeza kwa ajili ya kutia sahihi ya mkataka huko Roma wa kusitisha vikwazo na ninawatakia waendelee na mchakato wa majadiliano ya haraka na wawakilishi wa Serikali wanaoongozwa na Barnaba Marial Benjamin. Sisi sote tutatumia wakati huu ili kuwezesha maisha mapya katika Nchi Yetu kwa njia ya amani, mapatano na msamaha. Sisi tunatambua thamani ya Papa Francisko kwa sala zake na kwa njia ya kuomba amani kwa ajili ya Sudan Kusini. Katika hafla hii muhimu leo hii, sisi kwa hakika tunahisi na tunajivunia kuweza kutangaza kuwa tumepatana”, amehitimisha Bwana Kiir.

Hata hivyo hatua hiyo inafuatia na mkutano uliofanyika katika Ikulu katika mji mkuu wa Juba siku ya Alhamisi 20 Februari 2020 na ambapo Rais Kiir alikuwa ameahidi kuwalinda viongozi wa upinzani. Washiriki wa Bwana Machar walikuwa wanatafuta uhakikisho kuhusu usalama wake iwapo atarudi katika mji mkuu wa Juba. Bwana Kiir alisema kwamba masuala muhimu ambayo hayajasuluhishwa, kama vile jinsi yeye na Machar watakavyogawana mamlaka ni masuala ambayo yanatarajiwa kuangaziwa na kukamilishwa katika siku zijazo. Bwana Machar alikubali kuchukua wadhfa wake wa zamani kama makamu wa rais wa kwanza na Baraza la Mawaziri lililopo kuvunjwa ili kuruhusu viongozi zaidi wa upinzani. Kuna matarajio kwamba makubaliano hayo yatamaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka sita ambavyo vimegharimu maisha ya zaidi ya watu 400,000. Watu wawili hao waliunda serikali ya muungano ya muda mfupi mara moja 2016. Ilikuwepo kwa miezi mitatu pekee kabla ya Bwana Machar kuondoka Juba huku mapigano yakiendelea. Kila upande umekuwa ukimshutumu mwenzake. Kundi la Machar linalilaumu kundi la rais Salva Kiir kwa kushindwa kuiongoza nchi na limekuwa likimtaka kiongozi wa taifa hilo kujiuzulu.

Vile vile Umoja wa mataifa na Marekani umetishia kuidhinisha vikwazo dhidi ya watu wa Sudan kusini iwapo hawafikii makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi. Makabiliano hayo yamesababisha vifo vya watu wengi na kusababisha zaidi ya watu milioni moja kukosa makazi. Mapigano yalianza Juba na kuenea katika maeneo mengine yakiwemo Bor, Jonglei na Bentiu. Ikumbukwe kuwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, imenuia kutoa mafunzo kwa ajili ya muungano wa nchi mpya ambao umetarajiwa kwa mufa mrefu. Kwa njia ya mhusika wa mahusiano ya kimataifa wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Mauro Garofalo anasema “ ni kuunda hatimaye nafasi ya wakati endelevu wa nchi mbali na mapigano ya kislaha. Tuko tunafanya kazi na makundi yote ya kisliaa hadi sana ambayo yalikuwa yamebaki nje ya mchakato wa amani, kwa sababu waweze nao kufungamainishwa na naweza kuanza kwa upya majadiliano na serikali”.

24 February 2020, 12:02