Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaendelea kulipa gharama zaidi katika  migogoro inayoendelea na kusababisha vifo vingi vya watu Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaendelea kulipa gharama zaidi katika migogoro inayoendelea na kusababisha vifo vingi vya watu 

CAR:Madaktari wasio na mipaka wanaomba msaada!

Wakati wa mapigano kaskazini mwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanamgambo wa silaha wamechoma makambi ambayo yalikuwa yanakaliwa na maelfu na maelfu ya watu. Nyumba nyingi zimechomwa moto. Kutokana na hilo watu wamekimbilia katika Kituo cha afya cha Madaktari wasio na mipaka huko Batangafo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mapigano makali huko Kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati, yamelazimisha zaidi ya watu 10,000 kutafuta kimbilio katika Hospitali ya Madaktari wasio kuwa na Mipaka huko Batangafo. Wiki mbili zilizopita, zaidi ya watu 5,000 wanaishi katika hali mbaya sana inayozidi kuleta wasiwasi mkubwa wa raia wake.

Ipo hatari ya kuenea kwa malaria, kuhara na magonjwa ya mlipuko

Wakati wa mapigano kaskazini mwa nchi na ya kutisha, wamechoma makambi ambayo yalikuwa yanakaliwa na maelfu na maelfu ya watu. “Ni picha ya kutisha.  Tumeona mamia ya nyumba zikiwaka moto, na hata leo hii unaweza kusikia harufu ya kuungua”. Hayo ni maneno ya Bi Helena Cardellach, Mkuu wa Mpango wa Madaktari wasio na Mipaka, huko Batangafo Afrika ya Kati akisimulia hal hasi ya sasa ya kutisha kutokana na mapambano hayo. Hata hivyo ameongeza kusema kuwa: “kutokana na vizingiti vya kutoweza kutoa huduma ya matibabu kwa watu hadi sasa ipo hatari ya kwamba watu hawa watashambuliwa na malaria, kuhara na maambukizo, pia magonjwa ya mlipuko kuweza kusambaa”.

Kampeni ya “kusaidia matibabu ya moyo wa migogoro"

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaendelea kulipa gharama zaidi katika  migogoro, ambayo imesababisha  wakimbizi 570,000 kukimbilia katika mipaka ya nchi za karibu na 690,000 ambao wamekusanyika ndani ya nchi. Kutokana na taarifa hiyo, Madaktari wasio na Mipaka wanakumbusha kuwa,  bado Kampeni yao ya “kusaidia matibabu ya moyo wa migogoro, inaendelea hadi tarehe 30 Novemba 2018 na ili kuweza kuwasaidia Madaktari hao katika matendo yao ya dhati,  katika mantiki hiyo ya vita.

Vurugu hizi zote zinaendeshwa na makundi ya wanamgambo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo yanaendelea kufanya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika kipindi kati ya kipindi cha  mwaka 2013  hadi sasa. Mauaji ya watu wengi yamesajiliwa kufuatia na jinai zinazofanywa na magenge ya wanamgambo wanaobeba silaha nchini humo. Vilevile  ukosefu wa usalama na mapigano ndiyo yaliyopelekea kutokea hali hiyo ya kuogofya. Kwa maana hiyo Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhakikisha kuwa watu milioni 1.9 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaweza kufikishiwa hata  msaada wa chakula haraka iwezekanavyo ili kuisaidia na kuindoa nchi hiyo katika hatari ya mgogoro mkubwa wa kibinadamu unaoendelea kuikumba hadi leo hii.

Ripoti ya Misaada ya kibinadamu ya umoja wa Mataifa OCHA

Vilevile ikumbukwe mapema 4 Septemba mwaka huu, Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) iliripoti kuwa, hali ya wakazi wa mji wa Alindao wa kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mbaya sana kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya makundi ya waasi.  Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani, ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé kufuatia hujuma ya waasi wa Seleka. Tangu wakati huo hadi hivi sasa nchi hiyo imekuwa uwanja wa mapigano ya kila kuchao kati ya makundi hasimu, hususan lile la Kikristo la Anti-Balaka na kundi la Seleka. Miito mingi inaendelea kutolewa  ili kusitisha vita hivyo kwa pande zote, lakini matokeo kuona amani inaonekana bado kuwa mbali.

 

16 November 2018, 15:30