Watoto nchini Chad wanakufa  wengi kutokana na utapiamlo Watoto nchini Chad wanakufa wengi kutokana na utapiamlo 

Viwango vya kutisha vya utapiamlo katika N'Djamena, Chadi!

Madaktari wasio na mipaka wameacha jibu la dharura tarehe 26 Julai, kwa kushirikiana na wizara ya afya, katika ufunguzi wa kituo cha lishe na tiba kitongoji cha Ndjari mchini Chad il kutibu watoto wa umri kati ya miezi sita hadi miaka 5 walioathirika na utapiamlo wa kukithiri.

Frt. Tito Kimario – Vatican

Utapiamlo mkubwa, umeibuka na hauathiri tu majimbo ya vijijini ya ukanda wa Sahel lakini sasa ni sugu na umefikia kiwango cha kutisha kati ya watoto chini ya miaka mitano katika N'Djamena, mji mkuu wa Chad, mji wa karibu milioni 1.5 wa wenyeji.

 

Wakifafanua hali ilivyo, madaktari wasio na mipaka wanasema, “kwakweli ni mwaka mgumu! Kwa sababu hali inazidi kuwa mbaya kiuchumi baada ya kuanguka kwa bei ya petroli” anasema Chibuzo Okonta, makamu wa mratibu wa dharura wa madaktari wasio na mipaka. Madaktari wasio na mipaka wameacha jibu la dharura tarehe 26 Julai, kwa kushirikiana na wizara ya afya, katika ufunguzi wa kituo cha lishe na tiba kitongoji cha Ndjari il kutibu watoto wa umri kati ya miezi sita hadi miaka 5 walioathirika na utapiamlo.

Watoto 100 walilazwa ndani ya wiki mbili ikiwa ni baada ya ufunguzi wa kituo. “tumefungua hiki kituo kwa sababu baadhi ya vituo vinavyohudumiwa na wizara pamoja na wadau wa afya vilikua vimezidiwa na kufanya kazi nje ya uwezo stahiki kutokana na wingi wa wagonjwa tena waliozidiwa” amekiri Patient Kighoma, mhudumu wa kituo kipya cha madaktari wasio na mipaka na kusisitiza kuwa watoto wanapofikishwa katika hali mbaya namna hiyo, afya zao huwa mashakani na hudhoofu kwa kasi kubwa.

Kituo kimegawanywa katika sehemu mbalimbali ili kutoa wasaa kwa watoto kuhudumiwa kulingana na hali zao kiafya. Jengo lina kitengo cha uangalizi mkubwa ambapo jopo la madaktari wasio na mipaka wanashughulika na wagonjwa mahtuti wanaohitaji msaada wa karibu zaidi wa matibabu.

Mara tu afya zao zinapoimarika na kuanza kupata hamu ya kula, tunawapa chakula laini chenye asili ya maziwa, ngano au karanga kilichoandaliwa na mtaalamu wa tibalishe. Hatimaye tunaendelea kuwapatia tiba hususani kutibu magonjwa mengine yanayoambatana na utapiamlo.

Kiwango kikubwa cha utapiamlo kinachojitokeza kila mwaka nchini Chadi ni matokeo ya sababu nyingi changamani.  Mwaka huu N’Djamena, suala la utapiamlo limesababishwa na mgogoro wa uongozi, uhaba wa chakula pamoja na migomo katika huduma za kijamii ambayo imeikumba kwa namna ya pekee sekta ya afya. Familia nyingi katika mji mkuu wamekumbwa na mgogoro huu na sio wote wana nyenzo za kuukabili!

24 August 2018, 08:36