Dominika 23 Julai 2023 ni siku ya Wazee duniani. Dominika 23 Julai 2023 ni siku ya Wazee duniani.  (bernardbodo.com)

Katika Siku ya Wazee,watakabidhi ishara ya msalaba kwa vijana wa WYD

Huruma zake ni za kizazi hata kizazi(Lk 1:50),ndiyo kauli mbiu inayoongoza siku ya Wazee duniani na Papa Francisko anatarajia kuongoza Misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.Zaidi ya watu 6,000 watashiriki katika misa hiyo.Wazee 5 kutoka mabara watakabidhi mfano wa msalaba wa vijana 5 watakaokwenda Lisbon kwenye WYD.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha,w ametoa maelekezo ya siku ya Wazee dunia wakati wa Ibada ya Misa Takatifu kuwa wa wazee 5 watakabidhi mfano wa msalaba wa Hija wa Siku ya Vijana duniani (WYD), Dominika tarehe 23 Julai 2023, siku ambayo mwaka huu inaoogozwa na kaulimbiu:“Huruma  zake ni za kizazi hata kizazi”(Lk 1:50). Papa Francisko anatarajia kuongoza Misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Zaidi ya watu 6,000 watashiriki katika misa hiyo, wakiwemo wazee wengi kutoka pande zote za Italia na kwengineko. Hawa watakuwa ni babu na bibi wakiandamana na wajukuu zao na familia zao, wageni wa wazee katika nyumba za mapumziko na nyumba za wazee, pamoja na wazee wengi wanaohusika katika maisha ya parokia,  Majimbo na vyama vya kitume. Mwishoni mwa maadhimisho hayo, wazee 5 wanaowakilisha mabara matano duniani  watakabidhi kwa njia ya mfano msalaba wa mahujaji wa  Siku ya vijana duniani (WYD) kwa vijana 5 watakaoondoka kwenda Lisbon, nchini  Ureno ikiwa ni ishara ya kueneza imani kutoka kizazi hadi kizazi. Ishara ya kutuma pia inataka kuwakilisha ahadi ambayo wazee, babu na bibi wamekubali, kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu, kuwaombea vijana watakaoondoka na kuwasindikiza kwa baraka zao.

Sala kwa ajili ya siku ya III ya wazee duniani

Kwa washiriki wote wa maadhimisho hayo katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Jimbo kuu la Roma litatoa sala kwa ajili ya Siku ya III ya Wazee  Duniani na ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya maadhimisho hayo. Katika dokezo hilo, Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha linapyaisha  mwaliko wake wa kuadhimisha Siku ya Mababu na Wazee Duniani katika kila jimbo katoliki  duniani na kwa Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili yao na kuwatembelea wazee waliyo peke yao. Atakayetimiza ishara hiyo anatakuwa amepokea hata msamaha wa dhambi, au rehema kamili (Indulgenza plenaria) hasa kwa kutimiza vigezo ambavyo vinahitajika na ambavyo vimewekwa na Kanisa. Kwa  hiyo, mifano miwili yamaadhimisho, kati ya mengi yatakayofanyika duniani kote, pia  ni ile ya Baraza la Maaskofu wa Brazil, litakaloadhimisha misa pamoja na wazee kwenye Madhabahu ya parecida na lile la Baraza la Maaskofu wa Canada, ambalo limetoa video ya kuwaalika vijana kuwatembelea wazee katika nyumba za mapumziko. Kamati ya ndani ya maandalizi ya WYD huko Lisbon nchini Ureno  ilijiunga na mwaliko wa Papa Francisko, kuzindua mipango miwili: ya kuhamasisha  mlolongo wa maombi kwa ajili ya babu na bibi na wazee ili kusindikiza vijana wanaoondoka kwenda Lisbon na changamoto ya mitandao ya kijamii kuwaalika vijana wote kutembelea babu na bibi zao kabla ya siku na kuchukua picha au video wakiwa pamoja nao.

Lisbon: Stempu kwa ajili ya tukio la siku ya vijana

Hata hivyo Siku chache kabla ya kufunguliwa kwa Siku ya vijana  (WYD) huko Lisbon, Ofisi ya Posta ya Ureno iliwasilisha stempu ya pili ya kipekee inayotolewa kwa ajili ya Siku hiyo. Kamati ya ndani ya maandalizi ya WYD inaeleza kuwa Ofisi ya Posta,  imetoa mfululizo wa stempu mbili zenye thamani ya uso ya euro 0.61 na 1.15, na mzunguko wa nakala 75,000 kila moja, Picha ndogo ndogo za stempu ambazo zinaweza kununuliwa kwa euro 3. Kwa hivyo hata stempu zinakuwa sehemu ya mpango wa kitaifa wa siku ya WYD. Stempu hizo  mpya zinawakilisha Papa Francisko na alama za WYD  ambayo ni  Msalaba wa Hija na Picha ya Bikira Maria , Salus Populi Romani yaani Afya ya Warumi, ambazo zimekuwa kwenye hija nchini kote na sasa ziko tayari  Lisbon, kituo chao cha mwisho. Toleo hili la pili linafuatia lile la tarehe 1 Agosti 2022. Si mara ya kwanza kwa Ofisi ya Posta ya Ureno kushirikiana na Kanisa Katoliki. Mnamo 1895, wakati wa kumbukumbu ya miaka 700 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Anthony, mfululizo wa Stempu  uliwasilishwa.

Mwenyeheri Frassati katika Kanisa la Mama Yetu wa Rozari, Fatima

Katika Siku ya Vijana duniani huko Lisbon   aidha katika Kanisa la Mama Yetu wa Rozari ya Fatima shoka la barafu na rozari ya Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati itawekwa. Ikumbukwe kuwa Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati, ni mmoja wa watakatifu wasimamizi wa Siku ya vijana duniani waliochaguliwa katoloa toleo hili na  ambapo masalia yake yatakuwakpo  huko Lisbon katika Kanisa la Mama Yetu wa Rozari huko  Fatima (Av. Marquês de Tomar, 1050-154), ambapo baadhi ya masalio yake (la piccozza ed il rosario domenicano) yanaweza kutazamwa. Hii ilitangazwa na Chama cha Pier Giorgio Frassati, kikumbusha kwamba pamoja na Pier Giorgio, katika kanisa hilo hilo pia inawezekana kumheshimu Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alimwita “Mtu wa Heri nane.”

13 Julai ni siku ya III ya Wazee duniani
21 July 2023, 16:11