Diplomasia ya huruma ambayo huweka wazi mlango wa mazungumzo
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Miaka kumi baada ya upapa wa Papa Francisko, ujumbe wake unaohusishwa na ‘diplomasia ya huruma’ unaonekana wazi zaidi leo hii. Hayo yalisemwa na Katibu wa wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, katika hotuba yake huko Villa Malta, makao makuu ya gazeti la Civiltà Cattolica, wakati wa kuwasilisha kitabu cha Padre Antonio Spadaro chenye kichwa: "L'Atlante di Francesco. Vatican na siasa za kimataifa". Kwa mujibu wa Kardinali Parolin, nguvu ya ujumbe huo ni kubadilisha maana ya michakato ya kihistoria kwa kuelewa kwamba hakuna mtu anayepaswa kufikiria kama aliyepotea katika mahusiano kati ya mataifa. Mazungumzo, hata katika hali ngumu zaidi, yanahitajika kwa ajili ya amani, alisisitiza katibu wa Vatican, akibainisha kwamba Makao makuu yanaamini kwa dhati katika umoja wa pande nyingi na kwa hatua yake ya kidiplomasia itapatikana kila wakati kujitolea kwa ajili ya amani. Utatuzi wa migogoro, amesema hawezi kuja kwa kugawanya kwa hivyo inawezekana kila wakati kuacha mlango wazi wa mazungumzo. Kardinali Parolin aidha akarejea katika mtazamo ambao alisema lazima ujumuishe na usiwatenge adui kwani hii inaweza kuchukuliwa kuwa ushindi wa huruma.
Diplomasia ya huruma ambayo huweka wazi mlango wa mazungumzo
Katika wakati wa kihistoria unaojulikana na vita vya Ukraine, ambapo watu bilioni mbili wanaishi katika maeneo yaliyokumbwa na migogoro na ambayo imegawanyika katika vipande vipande vya Vita vya Kidunia vya Tatu ni muhimu diplomasia ambayo isiwe huduma ya maslahi ya taifa tu bali iweze kufungua mlango wa mikakati bunifu kwa ajili yasuluhishoi madhubuti na endelevu, alisisitiza Kardinali.
Kwa mujibu wa Kardinali Parolin anaona, kwa hivyo kwamba Vatican inaweza kuwa mhusika wa sehemu kubwa kwani kipaumbele chake ni kwa ajili ya maisha ya watu na hasa wale wanaoteseka. Yeyote anayefanya vita husahau ubinadamu, haanzii kutoka kwa watu na haangalii maisha halisi ya watu, alisisitiza Kardinali Parolin akinukuu maneno ya Papa Francisko. Kwa hiyo amani, kwa mujibu wa Kardinali, ni mwanzo tu wa mchakato mpana ambao unaweza pia kufanya uwezekano wa kuondokana na sababu za kijamii za umaskini. Changamoto kubwa za wakati wetu zote ni za kimataifa, alihitimisha Parolin, akimaanisha juu ya yote suala la uhamiaji na mabadiliko tabianchi.
Waziri Mkuu wa Italia Bi Meloni:Kiini cha Huruma katika hatua za kisiasa
Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni, pia alihudhuria katika uwasilishaji wa kitabu hicho katika makao makuu ya Civiltà Cattolica. Kwa maoni yake aliona kuwa huruma inaweza kuwa kiini cha hatua za kisiasa. Bi Meloni alitaja mpango wa Mattei kwa Afrika uliotangazwa na serikali yake kufafanua ushirikiano wa maendeleo kama silaha ya uhuru. Mgogoro huo alisema Waziri Mkuu akipokea msukumo kutoka kwa mafundisho ya Papa Franciko pia ilikuwa ni fursa, kwa sababu inawalazimisha kuchagua alisema. Serikali ya Italia, kulingana na Bi Meloni, inajaribu kugeuza mgogoro kuwa fursa”.
Kuhusu vita vya Ukraine Meloni alisema “ni lazima ieleweke wazi kwamba kuna mtu aliyeshambuliwa na kuna mchokozi. Kama hatungesaidia walioshambuliwa kujilinda, tusingekuwa na amani alisema. Kitu pekee kinachoweza kufanywa, chenye ufanisi zaidi, ni kuwaunga mkono wale wanaojitetea ili kanuni ya kwamba haki ya mwenye nguvu ina thamani zaidi kuliko nguvu ya sheria isipite”. Vatican ndio wanaofaa zaidi kupendelea suluhisho lililojadiliwa, alihitimisha waziri mkuu wa Italia huku akibainisha kuwa hilo linawezekana hasa kwa sababu halichochewi na maslahi ya taifa. Hatimaye Bi Meloni alikumbusha mada ya mateso ya Wakristo. “Mateso makubwa zaidi yanayoendelea duniani pia ni yale ambayo yanazungumzwa kwa uchache zaidi, alitangaza wazi waziri mkuu, akikumbuka mkutano uliofanyika tarehe 8 Machi na wasichana wawili ambao walikuwa wahanga wa Boko Haram nchini Nigeria.