Vatican katika mkutano kuhusu“Ufufuo wa Ukraine”huko Lugano
VATICAN NEWS
Mnamo Mei 30, iliyopita Rais wa Shirikisho la Uswisi, Ignazio Cassis na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, walitoa mwaliko kwa Vatican ili kushiriki katika Mkutano kuhusu Uokoaji wa Ukraine (mnamo 4-5 Julai huko Lugano). Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa aliongoza Ujumbe wa Vatican kwenye tukio hilo. Mwakilishi wa Kipapa huko Bern, Monsinyo Martin Krebs, alikuwa sehemu ya Ujumbe huo.
Monsinyo Wachowski alipeleka matumaini na sala za Baba Mtakatifu huko Lugano kwa ajili ya mustakabali wa amani katika ardhi ya Ukraine inayotamaniwa, ili kwa mshikamano wa wote, inawezekana kujenga kwa upya upendo kile kilichobomolewa huko na wazimu wa vita. Katika Mkutano huo ulihudhuriwa, angalau kwa ngazi ya mawaziri na zaidi ya nchi 40, ikiwa ni pamoja na Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula Von der Leyen, ambaye baadaye alitia saini kwa tamko na Kanuni za Lugano za ujenzi mpya wa Ukraine, kwa kukubaliana juu ya haja ya mageuzi ya kina na kwa ajili ya usasa wa nchi.
Katika hotuba yake fupi mjini Lugano, Monsinyo Wachowski ameeleza matumaini la Vatican kwamba mwisho wa vita utafikiwa haraka iwezekanavyo na kwamba juhudi za pamoja za Jumuiya ya Kimataifa zinaweza kupelekea kushinda maafa makubwa ya kibinadamu na maafa makubwa ya ujenzi mpya wa kiungo cha nyenzo na hali ya kiroho ya kijamii, kuwa ishara ya nguvu ya matumaini kwa watu wa Ukraine.