Kard.Parolin:inawezekana kufunga kurasa za uchungu kwa ajili ya amani ya nchi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, ambaye anaanza sehemu ya pili ya safari yake barani Afrika kwa niaba ya Papa, tarehe 4 Julai 2022 amesema anaondoka akiwa ametulizwa na uzoefu aliokuwa nao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kituo kilikuwa ni Juba cha mji mkuu wa Sudan Kusini ambapo Kadinali huyo akizungumza kwa vyombo vya habari Vatican alivyoandamana navyo kwenye safari yake amethibitisha matumaini yake ya kusaidia kuleta amani ya kudumu, ili kuwe na uwezo wa kusuluhisha na kupata makubaliano ya kufunga ukurasa huu mchungu. Labda kabla ya uchaguzi mkuu wa 2023.
Kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kadinali amesisitiza saa chache kabla ya kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Addis Ababa, nchini Ethiopia, kwamba ilikuwa wakati mzuri sana, wa nguvu na chanya. Angalau maoni yake ya kwanza alithibitisha kwamba ziara hiyo ilitumika kwa usahihi kuleta uwepo na upendo wa Papa kwa idadi ya watu na kwa Kanisa lililokuwa likimngojea kwa matumaini makubwa. Natumaini kuwa haya yote yanaweza kurudiwa nchini Sudan Kusini”. Kardinali Parolin amesisitiza kuwa hakika hata hali ile ya kisiasa, ni dhaifu sana. Kwa hiyo, kama vile Vatican ilivyofanya siku zote, kuna haja ya kuendelea kusisitiza amani ili kuwe na uwezo wa kupatanisha na kupata makubaliano ya kufunga ukurasa mchungu. Inatarajiwa pia katika chaguzi zijazo za 2023 kuwa hii inaweza kufikiwa.
viongozi wa Sudan Kusini huko Santa Marta
Katibu wa Vatican baadaye alikumbuka mafungo ya Mtakatifu Marta mnamo Aprili 2019, ambayo yalihudhuriwa na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, na makamu wa rais walioteuliwa, Riek Machar na Rebecca Nyandeng De Mabio. Kwao Papa, mwishoni mwa siku za sala na majadiliano, kwa ishara isiyo na kifani, alipiga magoti kubusu miguu yao na kuiombea nchi amani. Kwa kufuata, mfano huo, Kardinali Parolin alisema wanafuata nyazo hizo, kwa usahihi kusisitiza mwaliko huo, mawaidha hayo ma maombi hayo ya amani. Katibu wa Vatican kwa maana hiyo aliondoka katika mji mkuu Kinshasa wa Congo mapema alasiri y tarehe 4 Julai, baada ya kuadhimisha Misa na jumuiya ya seminari kuu ya Jimbo Kuu asubuhi mapema. Huko alisalimiana na kuzungumza na wafundaji na waseminari ambao alikaa nao kwa mkutano wa udugu, kwa kusikiliza nyimbo mbali mbali na chereko.
Kardinali pia alitia saini Kitabu cha Heshima, baadaye akahamia kwenye Nyumba ya Ubalozi wa Kitume, ambayo lilimkaribisha kwa upendo mkubwa katika siku hizi tatu. Kwa familia nzima ya Ubalozi, iliyoongozwa na Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Parolin alihutubia maneno ya shukrani na kutia moyo: “Mnafanya kazi kwa ajili ya Papa, msimsahau”. Kwa mara nyingine tena, kadinali alithibtisha nia ya Papa ya kwenda maeneo hayo haraka iwezekanavyo.
Mpango huko Juba
Shughuli ya kwanza katika ratiba ya Juba ilikuwa ni mahojiano alasiri na Rais wa Jamhuri, Salva Kiir, na kufuatiwa na wa makamu wa kwanza wa rais, Riek Machar. Wakati jioni, ilikuwa ni mkutano na maaskofu wa nchi hiyo. Moja ya wakati muhimu zaidi wa safari ya Sudan Kusini itafanyika mnamo Jumatano tarehe tarehe 6 Julai 2022: katika ziara ya kambi ya Bentiu kati ya watu waliokimbia makazi yao wanaoishi katika mazingira magumu, na huduma duni za maji na vyoo. Kardinali Parolin ataadhimisha Misa kwa ajili yao, ili kukutana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mtawala.
Mnamo alhamisi tarehe 7 Julai badala yake itakuwa siku ya Misa katika Hifadhi ya Mausoleum ya John Garang, ukumbusho uliowekwa wakfu kwa kiongozi wa Sudan na makamu wa kwanza wa rais wa Sudan baada ya mapatano ya amani. Ni mahali pale pale ambapo Papa alipaswa kuadhimisha Misa, Katibu wa Vatican atabariki jiwe msingi la Ofisi mpya ya Kitume mjini Juba na atakutana na wakleri na Watawa. Hatimaye, mwishoni mwa safari, ziara yake atakwenda Chuo Kikuu Katoliki na kile Kituo cha Watoto huko Usratuna, hali halisi ambayo watawa mbalimbali hushirikiana kwa ajili ya ushirikiano wa watoto wenye ulemavu na malezi ya familia zao. Tarehe 8 Julai mchana kadinali ataondoka kuelekea Roma, ambako anatarajiwa kuwasili siku itayofuata.