Kard.Parolin amefika Sudan Kusini:Mpo mioyoni mwa Papa na anasali kwa ajili yenu
Na Angella Rwezaulla- Vatican.
Katika uwanja wa ndege, mbele ya Balozi wa Vatican na mshauri mkuu wa serikali, kulikuwa na sherehe kati ya watawa na wanawake wa makabila tofauti ambao walipiga vigeregere wakicheza ngoma. Haya ni maelezo kutoka kwa waandishi wa habari Vatican wanaoongoza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican katika safari ya Sudan Kusini mara baada ya kutoka Congo DRC. Kwa mujibu wao wanasema kwamba Jumanne tarehe 5 Juni 2022, abiria waliokuwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia walianza kutazamana katika dakika za mwisho za kutua ili kuelewa ni nani angepokelewa nje ya uwanja wa ndege wa Juba nchini Sudan Kusini. Ndege ilikuwa bado haijagusa ardhi ambapo kwa chini ilikuwa tayari inasikika milio ya ngoma na milio ya vifundo vya miguu ya wanawake ambao kwa kuona ndege hiyo tu walijiachia kwa vigeregere visivyozuilika na kucheza.
Kardinali Pietro Parolin aliegemea dirishani na kuanza kusema ni makaribisho gani mazuri namna hiyo wakati inaanza kuonekana hata rangi nyekundu ya kapeti ndefu mlangoni, pembe za ndovu za sare za kijeshi, manjano, kijani kibichi, rangi ya machungwa ya mavazi ya kikabila ya wanawake na watoto waliocheza na zana za majani mikononi mwao, vikundi vya watawa wenye vitambaa vyeupe vichwani wakipeperusha mabango yaliyoandikwa “Karibu Kusini”.
Imeanza katika hali ambayo ni rahisi ya ziara ya Katibu wa Vatican katika mji mkuu wa Juba, kama hatua ya pili ya safari yake barani Afrika kwa niaba ya Papa na mara moja akatunukiwa maua na mkufu wa kawaida wa shanga za rangi. Waliokuwa wakimsubiri chini ya ngazi walikuwa Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Hubertus Mathews Maria van Megen, Kardinali Gabriel Zubeir, askofu mkuu mstaafu wa Khartoum, na maaskofu kadhaa waliovalia mavazi meupe, miongoni mwako akiwemo Padre Christian Carlassare, askofu mmsionari wa Rumbek.
Salamu za Kardinali
“Ni furaha kubwa kwangu kuwa hapa na kukaa hapa kwa siku chache kusherehekea, kusali, kukutana na watu, na kufanya hivyo niaba ya Baba Mtakatifu Papa Francisko ambaye daima anafikiria moyoni mwake, anajali, kwa ajili ya amani na maridhiano ya Sudan Kusini na anafuatilia maendeleo mazuri ya mahusiano. Asanteni sana”, alisema Kardinali Parolin.
Umaskini uliokithiri
Kardinali Parolin baadaye alipelekwa katika Ofisi uya Ubalozi wa Vatican lakini jengo ambalo linakodishwa kwa sasa. Kwa hakika, Kadinali atalibariki jiwe la msingi la 'Nyumba mpya ya Kiapa' nchini Sudan Kusini katika siku zijazo. Hatua hiyo ya kwenda huko ilikuwa katika gari aina ya jeep, gari pekee linaloweza kusafiri katika barabara hizo mbovu zilizotengenezwa kwa udongo mwekundu unaoshikamana. Lakini ni safari ambayo haikuwa mbali, safari hata hivyo inatosha kurudisha kikamilifu taswira ya umaskini uliokithiri ambao jiji hilo la Kiafrika linaishi. Kipande kikubwa cha barabara nyekundu ya ardhi ambazo hushikamana na majengo yaliyopangwa ambayo, kando ya barabara, kuna vibanda vya mbao, majani na vikaratasi.
Magari yenye bendera nyeupe ya manjano ya Vatican yalipopita, waliwezea kugeuka kutazama watoto waliokuwa wanasalimu. Wanatembea peke yao kati ya paka na mbuzi, au kusimama karibu na akina mama kwenye vibanda vya nguo na matunda wakiwa wamepumzika kwenye udongo. Kwa idadi hii ya watu wanaoteseka, na vile vile kwa hali ya maisha pia kwa ukosefu wa utulivu unaotokana na vita na ghasia zilizoenea kwa miaka katika maeneo haya, Kardinali Parolin sasa anapeleka bembelezo la Papa Francisko.