Mahujaji wa matumaini:Jubilei ya 2025 ili kujenga ulimwengu bora
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, Jumanne tarehe 28 Juni 2022 mchana akitoa hotuba yake katika Ukumbi wa Jumba la Kitume Vatican, katika uwakilishi wa Nembo rasmi ya Mwaka Mtakatifu, ametoa matashi yake mema kwamba kauli mbiu ya Jubilei ya 2025, “iweze kuwa kweli mahujaji wa matumaini na iweze kugeuka kuwa ulimwengu halisi kwa maudhui ya kufanya uzoefu”. Katika hotuba yake Kardinali Parolin alibainisha kuwa matukio ya miaka na miezi ya hivi karibuni yanaonekana kulilazimu Kanisa kuweka mtazamo wake katika fadhila ya matumaini, msingi wa maisha ya Kikristo pamoja na mambo mengine mawili ya fadhila ya kitaalimungu, ya imani na mapendo ambayo yanamtaka kila mtu kuwa mjenzi na mwajibikaji wa ulimwengu ulio bora. Kuhusiana na hilo, katibu mkuu wa Vatican alikumbusha kile ambacho Papa Francisko aliandika katika matazamio ya Mwaka Mtakatifu kwamba “Lazima tufanye kila kitu ili kila mtu apate tena nguvu na uhakika wa kutazama siku zijazo kwa nia iliyo wazi”.
Akizishukuru mamlaka za kiraia zilizokuwepo, na ambazo zinazohusika na majukumu maandalizi ya Jubilei, kwa ushirikiano unaotolewa kwa namna mbalimbali katika awamu hii ya maandalizi, Kardinali Parolin aliweka bayana jinsi hani utimilifu huo ulivyo muhimu na wenye manufaa kwa ajili ya manufaa ya wale watakaofanya mahujaji kwenye kaburi la Mtakaifu Petro na Paulo kwa kuvuka mlango Mtakatifu, kulingana na mapokeo ya Jubilei ya kale. Kwa upande huo Kardinali, alibainisha kuwa Jubilei ni fursa nzuri inayotolewa kwa namna ya pekee kwa jiji la Roma na Italia ikiwa ni wakati mwafaka wa kuwakaribisha mamilioni ya watalii watakaokuja kujionea tukio la imani na utamaduni. Na wakati wa kuiwakilisha nembo rasmi ya Jubilee ya 2025, ambapo alikuwa ni Askofu Mkuu Rino Fisichella, alisema hii ni nembo yenye maumbo manne yanaoonesha ubinadamu kutoka pembe nne za dunia, moja ikikumbatiwa na nyingine, ili kuonesha mshikamano na udugu ambao watu lazima wawe nao kwa pamoja, na huku safu iliyo wazi iking'ang'ania msalabani ambao kwa chini kuna nanga, ishara ya imani, ambayo pia inakumbatia na ya tumaini, ambayo haiwezi kuachwa. Mawimbi yaliyo chini yana yumba yumba kwa kuelezea kwamba hija ya maisha haisogei kila mara katika maji tulivu. Na kwa kukaribisha matumaini katika matukio ya kibinafsi na wakati matukio ya ulimwengu yanapoamuru kwa nguvu zaidi, sehemu ya chini ya Msalaba imerefushwa, ikijigeuza kuwa nanga, inayowakilisha tumaini ambalo linajiweka kwenye mwendo wa wimbi.
Sio kwa bahati mbaya juu ya uchaguzi wa rangi kwa wahusika: nyekundu ni upendo, matendo na kushirikishana; njano / machungwa ni rangi ya joto la binadamu; kijani huleta amani na usawa; samawati hafifu/bluu inaashiria usalama na ulinzi. Wakati Nyeusi / kijivu cha Msalaba / Nanga, kwa upande mwingine, inawakilisha mamlaka na nyanja ya undani. Uwakilishi mzima pia unaonesha ni kwa kiasi gani safari ya mahujaji si ukweli wa mtu binafsi, bali ni jumuiya na yenye nguvu inayoelekea Msalaba, pia yenye nguvu katika kujipinda kwake kuelekea ubinadamu kana kwamba inaelekea huko na sio kuiacha peke yake, bali kwa kutoa sadaka ya uhakika wa uwepo na usalama wa matumaini. Uwakilishi huo, unakamilishwa kwa rangi ya kijani, na kauli mbiu ya Jubilei 2025: Peregrinantes in Spem. Kwa kuongezea, Askofu Mkuu alisema, “Nembo hiyo, inawakilisha dira ya kufuata na kielelezao cha pamoja cha kujieleza chenye uwezo wa kupenyeza kwa njia iliyovuka vipengele vyote vinavyozunguka maadhimisho ya tukio la Jubilei na kueleza utambulisho na mada ya kipekee ya kiroho, ikijumuisha maana ya kitaalimungu ambamo Jubile inakua na kutendeka”. Nembo inayotambulisha Jubilei ya 2025 ni tunda la Mashindano ya Kimataifa, ambayo walishiriki walikuwa nu wanafunzi, wa mafunzo ya kisanii, picha, taasisi za kidini, wataalam na wasomi wa sanaa ambao walipaswa kukabiliana na kauli mbiu ya “hija na matumaini”. Mapendekezo 294 yalipokelewa kutoka miji 213 na nchi 48 tofauti. Umri wa washiriki ulikuwa kuanzia miaka 6 hadi 83.
Tume ilitathmini kazi zilizowasilishwa kulingana na vigezo vitatu: uchungaji, ili ujumbe wa Jubilei uweze kueleweka kwa urahisi; kiufundi wa mchoro, ambao ulihakikisha uundaji mzuri wa picha uliozalishwa; uzuri, ili muundo ufanyike vizuri na kuvutia. Baadaya ya kuchuja , mipango mitatu ya mwisho iliwasilishwa kwa Papa ili achague ile iliyomvutia zaidi. Na kwa maana hiyo chaguo halikuwa rahisi kwake pia baada ya kutazama mipango mara kadhaa na kuelezea kuridhika kwake, chaguo liliangukia kwa pendekezo la Giacomo Travisani, amefafanua Askofu Mkuu Fisichella. Kwa mujibu wa maelezo ya mchoraji wa kazi hiyo Giacomo Trevisani kwa msisimko alisema: “Nilifikiria watu wa rangi zote, mataifa na tamaduni, wakizunguka kutoka pembe nne za dunia na kuelekea siku zijazo, wengine, ulimwengu kama matanga ya meli kubwa ya kawaida, shukrani kwa upepo wa Tumaini ambalo ni msalaba wa Kristo na Kristo mwenyewe”. Na katika kulifanya Tumaini mara moja alifikiria juu ya Msalaba kwamba Tumaini, nilijiambia, kuwa ni katika Msalaba”.
Kwa maana hiyo Travisani alimfikiria Papa, Petro wa leo hii, akiwaongoza watu wa Mungu kuelekea kwenye lengo la pamoja, akiukumbatia Msalaba, ambao unakuwa nanga, kama rejea thabiti ya ubinadamu”, huku watu wakimng’ang’ania yeye na pia nanga ambayo mahujaji wa nyakati zote hung’ang’ania. “Sisi ni 'Mahujaji wa Tumaini kwa sababu tunabeba hofu za majirani zetu pamoja na za kwetu kwa nia ya kuwashirikisha na kuzifanya kuwa zetu ndio maana ya picha ambazo zinakumbatiana kati yao kwa kutazama Msalaba kama njia ya maisha, alihitimisha mtunzi wa Nembo ya Kauli mbiu ya Jubilei ya 2025. Papa Francisko aliomba miaka miwili inayotangulia Jubilei izingatiwe katika mada mbili maalum. Na hivyo mwaka 2023 utawekwa kwa ajili ya kurejea mada kuu za Katiba nne za Mtaguso mkuu wa II wa Vatican, ambampo mnamo tarehe 11 Juni Oktoba utaadhimishwa miaka 60 ya ufunguzi wake “ili Kanisa liweze kupumua tena” “fundisho hilo la kina na la sasa liliozaliwa”, kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Mkuu Fisichella. Kuhusiana na hilo, kuna safu za mafundisho ya hali ya juu ambayo yameandikwa kwa lugha ya kuvutia ili kuruhusu wale ambao hawana kumbukumbu wawe wadadisi na kugundua shauku ya uvumbuzi ambayo imeliwezesha Kanisa kuingia katika milenia ya tatu ya historia yake. Na mwaka 2024, kwa upande mwingine, utakuwa mwaka wa kujitoa kwa ajili ya sala Wazo hilo ni kuunda muktadha unaofaa kwa ajili ya Jubilee na kuruhusu mahujaji kujiandaa.
Maandalizi ya Mwaka Mtakatifu 2025
Kwa ajili ya Mwaka Mtakatifu wa 2025, mafanikio ya sayansi na teknolojia pia yatatumika. Kwa maana hiyo Mamilioni ya watumiaji watalazimika kuruhusiwa kuwa mahujaji pia kupitia teknolojia ya dijitali na kuzunguka njia, kupokea uzuri wa utakatifu wa wakati huu, amefafanua Askofu Mkuu Fisichella. Kwa sababu hiyo wanataka kutoa uhai kwa mtiririko wa habari ambazo, ingawa zitaruhusu kukumbuka karne nyingi za historia, pia iyawalazimisha kubaki wamekita mizizi katika sasa. Baada ya kiangazi, tovuti rasmi ya Jubilei itapatikana na programu zake, zana mbili za kusaidia kufurahia vyema matukio yaliyopendekezwa, kuwezesha uzoefu wa kiroho na kiutamaduni wa jiji la Roma. Kwa maana hiyo, Tovuti itakuwa na, pamoja na Hati muhimu ya Hija, habari, maelezo ya kihistoria, habari ya vitendo, huduma na zana za vyombo vya habari katika lugha kumi na kiwango cha juu cha ufikiaji kwa watu wenye ulemavu. Hatimaye, Askofu Mkuu Fichella alionesha, kulingana na mpango wa kwanza, orodha ya matukio makuu yaliyopangwa kwa ajili ya: familia, watoto, vijana, Harakati na vyama, wazee, babu na bibi, walemavu, michezo, wagonjwa na afya, vyuo vikuu, ulimwengu wa kazi, kwaya, vyama vya Ndugu, mapadre, watawa, Wakatoliki wa Mashariki, makatekista, maskini, wafungwa. Lakini pia ratiba kamili itakuwa tayari mwishoni mwa mwaka.