2022.06.23 Misa kwa ajili ya Familia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro iliyoongozwa na Kardinali Farrell Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. 2022.06.23 Misa kwa ajili ya Familia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro iliyoongozwa na Kardinali Farrell Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. 

Kard.Farrell:Familia zijenge madaraja kati ya vizazi!

Familia ziwe walinzi wa utakatifu wa maisha,ngome dhidi ya chuki,watangazaji wa huruma na mashuhuda wa Yesu. Kuna jukumu la kikanisa la watu wenye ulemavu,wito wa watu wapweke,familia zinazoishi matukio fulani kama vile kifo cha mtoto.Hayo ni katika Mahubiri ya Kardinali Farrell wakati wa Misa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petropia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaalimungu kichungaji katika Ukumbi wa Paulo VI.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali  Kevin J. Farrell, Mwenyiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, katika mahubiri yake kwenye  Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa asubuhi  tarehe 23 Juni 2022 katika  Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, wakati wa ufunguzi wa siku ya pili ya Mkutano wa Familia duniani  unaoendelea mjini Vatican amesema Leo jamii inajenga kuta kati ya vizazi, lakini familia lazima ziwe madaraja. Akizungumzia juu ya kifungu cha Injili kuhusu  kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji ambaye siku kuu yake imefanyika siku moja kabla, kwa sababu Ijumaa  tarehe 24 Juni  2022 ni maadhimisho ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kardinali amesisitiza kwamba katika"hali za shida, mateso, fedheha na  kuvunjika moyo kwa familia nyingi Mungu anaweza kuingilia kati kila wakati, kama ilivyokuwa kwa Elizabeti na Zekaria, na anaweza kuwafungulia kwa jambo lisilotarajiwa kabisa. Kwa maana hiyo amewashauri kutopoteza tumaini kamwe.

Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican
Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican

Kwa ajili ya Familia zote, Kardinali Farell amewakabidhi utume kwa kufuata mfano wa Mtakatifu Yohane Mbatizaji. Kwanza kabisa, anajenga madaraja kati ya vizazi, kwa kuzingatia oamoja yake ya zamani, ya sasa na siku zijazo pamoja. Kwa njia  hiyo amewaomba wahifadhi tumaini katika magumu yanayopatikana kila siku. Kabla ya kuzaliwa katika tumbo la mama yake Yohanaealitambua uwepo wa Bwana katika tumbo la Maria. Tangu wakati huo aliwekezwa na kazi yake kubwa. Hii inafanya kuelewa kwamba kazi nyingine kwa familia ni kuwa walinzi wa utakatifu wa maisha ya mwanadamu tangu kutungwa mimba hadi kifo chake cha  kawaida.

Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican
Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican

Mungu ana mipango kwa kila mmoja, amesisitiza Kardinali  Farrell huku  akikumbuka kwamba Injili ya siku  inatoa nyakati tatu msingi kwa Myahudi ambayo ni tohara, ubatizo na jina. Mtoto anapopokea jina, anapokea pia utume.  Kwa sababu hiyo kama waamini na kama wanafamilia wote wana  utume wa kutimiza.   Kutokana na hilo ndipo ametoa wito kwa Familia kwamba wao ni ngome dhidi ya chuki inayoongezeka ulimwenguni.  Amewaomba wawe watangazaji na vyombo vya huruma, manabii wa uaminifu kwa Mungu na mapaji yake na kuwa  mashuhuda  wa Yesu ”.

Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican
Misa kwa ajili ya washiriki wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Vatican

Na katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa X kwa Kongamano la Kitaaalimungu katika Ukumbi wa Paulo VI, Vatican ambao umeongozwa na Mada “ Upendo wa Familia: wito na njia ya Utakatifu amesema  Familia iliyoanzishwa juu ya  sakramenti ni ya kuzidisha ambayo sio tu kwa wanandoa. Kwa maana hiyo Kanisa linahitaji familia na mchango wao wa vitendo hai. Ni lazima kujiuliza katika nyanja gani wanaweza kutenda vyema zaidi ili kuzifanya familia kufahamu wajibu walio nao katika Kanisa. Kuhusiana na sehemu za pembezoni zinazowezekana, Kardinali amependekeza kutegemea utambuzi ambao ni jambo kuu. Ni kwa kufanya mang’amuzi stahiki tu ndipo wataweza kuwaleta pamoja watu kwa Kristo. Katika mkutano huu wa ulimwengu, alisisitiza jinsi ilivyo tofauti  na mikutano mingine kwa sababu ya janga la uviko , ikilinganishwa na zile za mwisho zilizofanyika.

Kongamano la kitaalimungu katika Ukumbi wa Paulo VI
Kongamano la kitaalimungu katika Ukumbi wa Paulo VI

Hata hivyo, shukrani kwa maendeleo ya vyombo vya habari vya kidigitali na njia za mawasiliano, amesisitiza Kardinali Farreli kuwa  kila wakati wot wanaweza kufuatilia dunaini kote. Zaidi ya yote, kuna kipengele cha mambo mapya ambayo lazima wayazingatie, hasa  katika kila bara Maaskofu nao wanafanya  mkutano sawa na familia kuhusu kauli mbiu  sawa ambayo watakuza jiji Roma kwa siku hizi hadi Dominika tarehe 26 Juni 2022. Kwa hakika anaamini kwamba ni muhimu wataweza kufanya uzoefu wa  siku hizi tatu zijazo pamoja kama wakati wa ushirika halisi wa kikanisa na familia zinazotarajia sio tu nyakati za usaidizi bali pai sishaea za  utambuzi wa hali nyingi zinazohitaji kushughulikiwa.  Watajikita katika uchunguzi wa masuala kulingana na kile ambacho kimeubuka kwa  mikutano yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Na wanapaswa kujumuisha mada nyingine ambazo zimeripotiwa kwao na ambazo wanafahamu.

Kongamano la kitaalimungu katika Ukumbi wa Paulo VI
Kongamano la kitaalimungu katika Ukumbi wa Paulo VI

Kardinali Farrell vile vile amefikiria kwa mfano juu ya jukumu la kikanisa la watu wenye ulemavu, wito wa watu wapweke, familia zinazoishi matukio fulani kama vile kifo cha mtoto. Sio suala la kuorodhesha hali zote maalumu lakini, ni suala la kuweka pamoja mtazamo wa usindikizaji wa kutosha wa kichungaji ambao, kama Papa Francisko anavyo waonesha katika waraka wake wa  Amoris Laetitia, na lazima waanzie kutoka kwa familia ni nini au mahali pa kuishi karibu na  ni upendo.

TAFAKARI NA HOTUBA YA KARDINALI FARRELL KATIKA MKUTANO WA X WA FAMILIA
23 June 2022, 18:12