Kimetolewa Kitabu kipya chenye kichwa:“Pazia la ukimya. Nyanyaso, vurugu, frustrazioni katika maisha ya watawa wa kike".Kinapatikana katika duka la Vitabu Mtakatifu Paulo.(Paulinus) Kimetolewa Kitabu kipya chenye kichwa:“Pazia la ukimya. Nyanyaso, vurugu, frustrazioni katika maisha ya watawa wa kike".Kinapatikana katika duka la Vitabu Mtakatifu Paulo.(Paulinus) 

Kitabu kipya kinachosimulia kuhusu uzoefu wa watawa walioathirika na kukaa kimya

Kitabu kipya cha mtunzi Salvatore Cernuzio kichwa:“Pazia la ukimya.Nyanyaso, vurugu,kukatishwa tamaa katika maisha ya watawa wa kike”,kimechapishwa na duka la vitabu la Mtakatifu Paulo.Ifuatayo ni Dibaji ya kitabu iliyoandikwa na Sr.Nathalie Becquart,Katibu msaidizi wa Sekretarieti kuu ya Sinodi ya maaskofu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kimetolewa Kitabu kipya chenye kichwa: “Pazia la ukimya.Nyanyaso, vurugu,kukatishwa tamaa katika maisha ya watawa wa kike”, kimechapishwa na duka la vitabu la Mtakatifu Paulo ambacho kimeandikwa na Salvatore Cernuzio, ambacho katika dibaji imeandikwa na Sr. Nathalie Becquart, Katibu msaidizi wa Sekretarieti kuu ya Sinodi ya maaskofu. Sr. Nathalie anasema kuwa kitabu hicho cha ushuhuda kinatufanya kuhisi kilio na mateso mengi ambayo mara nyingi yamenyamazishwa na mtego wa hali za uchungu, ambazo sehemu kubwa ya mateso hayo kwa bahata mbaya yalipelekea watawa wengi kuacha maisha ya utawa. Mtunzi wake anasikiliza historia zao kwa uelewa ili kuweza kutoa ushuhda wa wanawake hao waliojeruhiwa na ambao wanatafuta kujijenga kwa upya na kutufanya kuhisi uzoefu wao, mapambano yao na matumaini yao. Kwa namna hiyo, yeye anachangia kukuza utambuzi wetu wa matatizo ya nyanyaso katika maisha ya kitawa na kutoa kipaumbe cha usikilizwaji wa waathiriwa ambao hawakuweza kusikiliziwa na kukaribisha, hawakuheshimiwa, hawakutambuliwa na wala kusindikizwavizuri katika jumuiya zao. 

Sr. Nathalie anawapongeza sana wanawake  ambao walipata ujasiri na kukubali kuzungumza na  kutoa ushuhuda wao wa kweli. Kwa maana hiyo anahimiza kwamba lazima kuwasikiliza na kufanya kutambua kuwa maisha ya kitawa katika tofauti zake, kama zilivyo hali nyingine za kikanisa, zinaweza kweli kuzaa mambo yaliyo bora na yaliyo mabaya zaidi. Sr anafafanua kwamba yaliyo bora ni pale ambapo nadhiri za watawa: ufukara, usafi wa moyo na utii zinakuwa mchakato wa safari ya kukua kibinadamu na kiroho, safari ya ukomavu ambayo inafanya kukua kwa  uhuru wa watu,  kwa sababu mamlaka ni wito wa kuhamasisha hadhi ya mtu. Na inawezekana kuwa mbaya zaidi ikiwa nadhiri za watawa zinatafsiriwa na kuishi kwa mtindo wa kitoto, kukandamiza au hata kuwatumia na kuharibu watu. Kwa njia hiyo Sr Nathalie katika dibaji hiyo anasema, kitabu kinatualika kwa namna hiyo kutazama kwa sura halisi na kusema ukweli katika kutafuta njia zinazowezekana ili kuwasindikiza watu ambao wanateseka katika maisha ya kitawa, au ambao waliteseka na waliondoka ndani mwa jumuiya hizo na wanahitaji sasa kujijenga kwa upya. Lakini zaidi ya hayo yote ni kutafuta njia iwezekanavyo ili kuzuia makosa na mzizi hasa unapotokea ili kusaidia jumuiya za watawa wachuke mtindo mmoja ambao ni wa kisinodi.

Akitazama juu ya safari ya mchakato wa Sinodi tunayoendelea, Sr Nathalie ameandika kwamba kwa hakika kama inavyokumbusha Hati ya maandalizi ya Sinodi ijayo kuhusu Sinodi katika sehemu yake ya kwanza, ambayo inajieleza muktadha wa mchakato wa sinodi inasema kuwa: “Hatuwezi lakini kijificha kuwa Kanisa lenyewe linapaswa kukabiliana na ukosefu wa imani na ufisadi hata ndani mwake. Kwa namna ya pekee hatuwezi kusahau mateso ambayo waliishi watoto na watu wazima waathirika kwa sababu ya nyanyaso za kijinsia, nyanyazo za madaraka na nyanyaso za kidhamiri zilizofanywa na idadi kubwa ya makleri na watu waliowekwa wakfu. Sisi sote tunaitwa kila mara kama watu watu wa Mungu kubeba mizigo ya uchungu wa kaka na dada zetu waliojeruhiwa katika mwili na katika roho. Kwa muda mrefu, kwa upande wa waathirika  walitoa kilio chao  ambacho Kanisa halikujua kusikiliza vya kutosha. Haya ni majeraha ya kina, ambayo ni vigumu kuponya, ambayo hatutawahi kuomba msamaha vya kutosha na ambayo huleta vikwazo, wakati mwingine katika mwelekeo wa kutembea pamoja”. Kanisa zima linaitwa kushughulikia uzito huo wa utamaduni ulioimarishwa na makleri, na ambao unarithi kutoka katika historia yake na aina za matumizi ya mamlaka ambayo ni aina tofauti za matumizi mabayaliyo pandikizwa kama vile (ya mamlaka, kiuchumi, kidhamiri, kingono)”. Kwa maana hiyo uongofu wa utendaji wa kikanisa hauwezi bila ushiriki hai wa vipengele vyote vya Watu wa Mungu na kwa maana hiyo, pamoja tumwombe Bwana neema ya uongofu na upako wa ndani ili kuweza kuonesha toba yetu na uamuzi wetu wa kupambana kwa ujasiri”.

Sr. Natahalie amesema sisi sote tumeitwa kufahamu matendo haya potovu ya utii na utumiaji wa mamlaka katika Kanisa, ambayo kwa bahati mbaya yametokea katika parokia na jumuiya za zamani na mpya za maisha ya watawa au vyama katoliki vya walei. Ni lazima tusikilize wito wenye nguvu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya uongofu wa kichungaji, unaotutaka tuache kielelezo cha ukleri wa Kanisa na kuingia katika maono mapya ya Kanisa la Sinodi ambayo ina maana ya kusikiliza na kushiriki kwa wote na kuchukua hatua za uwajibikaji wa pamoja. Kwa sababu wote, waliobatizwa, wanafunzi wamisionari, wana hadhi sawa na lazima wachukuliwe kama wadau na watendaji wa kiutume. Wote, wanaokaliwa na Roho Mtakatifu, na  wameitwa kufanya kuwa sauti zao zisikike. Ili kuendelea kutangaza Habari Njema ya Injili katika ulimwengu wa leo, Kanisa lazima ligundue tena na kutekeleza kwa vitendo sinodi ambayo ni sehemu ya asili yake.

Hiyo ni kutambua njia za kuishi nguvu hii ya muungano, ya sisi ambayo ni ya kikanisa inayoheshimu na kuunganisha utofauti wa umimi kuwa umoja, kukubalika na kuthamini utofauti wa karama kwa sababu Roho Mtakatifu hunena ndani ya kila moja na utii katika Kanisa lazima liwe na  usikivu daima wa kawaida wa Roho. Kwa njia  fulani, kupitia kitabu hiki mtunzi Salvatore Cernuzio , anabainisha Sr, anatupatia mtazamo kamili wa kile ambacho Mashirikia ya kitawa imeangazwa waziwazi kufanya katika hati yake muhimu ya mwelekeo yenye kichwa: “Kwa viriba vipya vya divai (2017), changamoto hiyo ya upyaishwaji wa lazima na malezi sahihi katika kutekeleza utii na mamlaka. Hati hiyo inasisitiza kuwa: “Katika baadhi ya matukio, ushirikiano hauendelezwi na utii na uwajibikaji (29), lakini kwa uwasilishaji wa kitoto na utegemezi wa umakini. Kwa njia hiyo, hadhi ya mtu inaweza kuharibika hadi kufikia kumdhalilisha. Katika uzoefu huu mpya au katika mazingira mengine, tofauti kati ya jukwaa la nje na la ndani haizingatiwi kila wakati kwa usahihi na kuheshimiwa ipasavyo”(30).

Kwa njia hiyo katika mabadiliko haya ya zama tunamoishi ni lazima tutambue kwamba: “Utii na huduma ya mamlaka hubakia kuwa masuala nyeti sana pia kwa sababu tamaduni na mitindo zimepitia mambo ya kina, yasiyo na kifani na katika baadhi ya mambo, pengine kwa baadhi ya mabadiliko ya kutatanisha. Katika muktadha tunamoishi, neno lenyewe la “Superiori” na “sudditi”,  yaani “wakuu” na “wanaongozwa” ni neno ambalo halistahili tena. Kile kinachofanya kazi katika muktadha wa uhusiano wa nchi ya juu na kimamlaka hautamaniki tena au kuishi katika unyeti wa muungano kwa njia yetu ya kuelewa na kutaka kuwa Kanisa.  Inapaswa ikumbukwe kwamba utii wa kweli hauwezi kujizuia kutanguliza utii kwa Mungu, wa mamlaka na wa wale wanaotii, sawasawa na utii wa Yesu; utii unaojumuisha kilio chake cha upendo wa Mungu: “Wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha? (Mt 27:36) na ukimya wa Baba wa upendo”. Kwa kuhitimisha, Sr. Natahalie ni matashi yake kuwa Kitabu hiki, ambacho kinatualika kutazama upande wa giza wa baadhi ya uhalisia wa maisha ya watawa, kitusaidie kusikia na kutekeleza mwaliko wa dharura wa Baba Mtakatifu Francisko  kwa jumuiya zote za ulimwengu ili kuomba  hasa ushuhuda wa ushirika wa kidugu na  ili uwe wa kuvutia na unaongaza. Na kwamba kila mtu aweze kufurahia jinsi wanavyojali mtu mwingine, jinsi wanavyotiana moyo na jinsi wanavyosindikizwa (26).

24 November 2021, 14:16