Tarantola:Kuamsha kuta hakusaidi,njia pekee ni ushirikiano kidugu
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji ndiyo mada inayoongoza kingamono la kimataifa la siku mbili 21-22 Oktoba ambalo limefunguliwa katika ukumbi mpya wa Sinodi Vatican na litahitimishwa na kukutana na papa Francisko mnamo 23 Oktoba. Ni mambo msingi matatu ya matumaini ambayo Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice, wameandaa katika tukio hili kwa kupitia kauli mbiu ndogo ya dawa kwa ajili ya kupambana na ukosefu wa haki, usawa na ubaguzi. Kwa maana hiyo mada hiyo ndiyo itakuwa ncha kali ya kukabaliana na watoa mada kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu kama vile Mtuzwa nobel ya Fisikia 2018, Gérard Albert Mourou, na wakuu wa Vatican, miongoni mwao akiwamo Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na Nchi, Kardinali Peter Turkson, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Frangamani ya Binadamu.
Kuna majadiliano katika meza ya mduara na mtazamo juu ya nyaraka za Papa Francisko za Fratelli Tutti na Laudato si na ambazo kwa mujibu wa waandaji zinawakilisha mwendelezo wa kweli wa mafundisho Jamii ya Kanisa katika historia. Kwa mujibu wa waandaji wamsema tuki la kongamano hili litahitiishwa na mkutano na Papa Francisko kwa washiriki wote. Lengo la tukio hilo ni kutathimini kwa dhati ikiwa wanaweza kujikita kwenye mazoezi ya thamani za mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji, kutokana na maelezo ya Bi Anna Maria Tarantola, Rais wa Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice. Na thmani msingi za kukabiliana kwa dhati katika changamoto zote ambazo leo zipo mbele yak ila mmoja, kwa mfano kiafya kichumi kidigitali na kiikolojia ulimwenguni.
Mabadiliko ya tabiachi yanahitaji uongofu wa wote kwa maana kuna mtindo ndani mwake wa kibiashara, kiuongozi katika misingi miwili ya elimu na mawasiliano. Bi Tarantola aidha amesebainisha kuwa lakini ni mabadiliko ambayo hayawezi kutimizwa bila kuwa na nanga za ushirikiano, mshikamano na uwajibikaji. Hii yote imejionesha katika tukio la kidunnia la janga la UVIKO kwamba bila kujiweka katika matendo, thamani hizi zinakosa njia na hakuna matokeo mema, lakini kwa kuunganisha misingi hiyo mitatu matokeo ni makubwa mno. Bi Tarantola amesema kuwa mabadikio hata hivyo yanapaswa yawe ya mzunguko kauanzia juu kwenda chini, kulia na kushoto kwa maana wote ni wawajibikaji. Ametoa mfano kuhusu kijana mdogo Greta Thunberg: kwamba vijana walianzia chini na wako wanaendelea kwa kasi kubwa lakini inayohitaji utambuzi wa kweli wa hali ya juu kwa kwa viongozi na ambayo ni muhimu sana, kwani kuamsha kuta hakusaidii katu, kinachotakiwa ni ushirikiano na mshikamano kwa wa kidugu na ambao unaweza kuoka sayari yetu.