Papa akutana na Michel:katika mazungumzo niwakimbizi wa Afghanis
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Siasa za kimataifa na za kikanda, hasa kwa hali ya nchi ya Afghanistan, na baadaye changamoto za Ulaya ndizo zimekuwa mada muhimu katikati ya mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Rais wa Baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel, ambaye amepolkewa katika Jumba la kitume Vatican. Bwana Michel, baada ya mkutano na Papa vile vile amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Ushirikiana na Nchi.
Wakati wa mazungumzo yao yamekuwa mazuri kwa mujibu wa taairfa kutoka Ofisi ya Wanahabari Vatican na kwa maana hiyo masuala kadhaa ya siasa za kimataifa na za kikanda zilijadiliwa, kwa kuzingatia hali ya wakimbizi wa Afghanistan. Vile vile wakiendelea na mazungumzo hayo wamekuwa na mtazamo wa Mkutano juu ya mustakabali wa Ulaya unaotarajiwa.