Kardinali Parolin Katibu wa Vatican Kardinali Parolin Katibu wa Vatican 

Kard.Parolin:mateso nchini Afghanistan,yangezuilika!

Hali halisi kwa nchi za Asia na masuala ya chanjo ndiyo baadhi ya mada ambazo Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican amezungumzia wakati wa ziara yake huko Montevergine,wilaya ya Avellino nchini Italia katika kufunga shereh za Siku kuu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hali halisi nchini Afghanistan ambayo siyo rahisi, ingewezekana kabisa kufikia maamuzi sahihi ya kutoa wanajeshi wa nchi za magharibi kwa kutumia uamuzi mzuri bila kusababisha mateso yaliyopo. Ndilo limekuwa wazo la Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican wakati alikuwa kwenye madhabahu ya Montevergine, kwa kuadhimisha misa ya kufunga sherehe za Mama Maria katika madhabahu hiyo.

Kardinali Paparolin ameeleza vile vile ambavyo ameweza kufuatilia hali halisi nchini Afghanistan hasa kwa mtazamo wa huduma kibinadamu na kuwa na mawasilianao kwa wale wanatoa huduma ya kibinadamu na upendo.  Kwa maana hiyo amethibitia jinsi ambavyo iliwezekana kurudisha nyumbani mapadre na watawa wa Mama Teresa wa Kalckutaa a ambao walikuwa katika mmaeneo yao ya kitume japokuwa hawakuwa wanataka kuacha watoto na vijana wao walio kuwa wakiwahudumia katika hali halisi ya vugivugu la vurugu hizo. Kardinali amesema kunda katikati ya msuko suko huo ni vema kuona ishra za upendo ambazo zinaweza kutolewa kwa furaha na matumaini na kuweza kufanya vema zaidi.

Akifafanua juu ya hali halisi ya maambukizi ya covid na sheria ambazo zimewekwa na Italia, amerudia kusema kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko alisema kwamba "kupata chanjo ni tendo la upendo kwa mtu binafsi na kwa wengine, kuchanjwa chanjo iliyoidhinishwa na Serikali na Mamlaka husika ni kitendo cha upendo. Na ikiwa kama watu wengi zaidi watapata chanjo dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ni kitendo cha upendo wa hali ya juu sana. Na huu ni upendo wa mtu binafsi; upendo wafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na hatimaye ni upendo kwa watu wote”. Kwa maana hiyo ni kitendo cha wajibikaji na Kardinali amerudia kutoa wito wa kukabiliana na changamoto kwa ujasiri kutokana na dharura ya kiafya. Kuhusu kuumwa kwa Papa mnamo Julai iliyopita, anaelezea kuwa Papa Francisko amepona vizuri sana na kwa maana hiyo Kama Katibu alikuwa kama msemaji wake na mtoa shukrani kwa Mama Maria wa Montevergine.

06 September 2021, 15:33