2021.08.31 Kardinali Parolin akiwa anaadhimisha Misa katika madhabahu ya Mama Maria huko Brezje nchini Slovenia katika fursa ya maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru nchini humo. 2021.08.31 Kardinali Parolin akiwa anaadhimisha Misa katika madhabahu ya Mama Maria huko Brezje nchini Slovenia katika fursa ya maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru nchini humo. 

Kad.Parolin:Ulaya ijengwe kwa misingi ya ukweli,haki,uhuru na upendo

Katika mji wa Brezjen nchini Slovenia Kardinali Parolin Katibu wa Vatican aliadhimisha misa kwa ajili ya miaka 30 ya uhuru na kumbikizi la mia 25 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembea nchi hiyo.Kiini cha mahubiri ni umuhimu Ulaya na ulimwenda kutoa msingi thabiti unaojengwa juu ya Neno la Mungu kwa kutoa upendo utokanao na matunda yake

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican yuko katika safari, kwanza nchini Slovenia kwa ajili ya kushiriki jukwaa la kimataifa la mkakati wakati ujao wa ulaya 'Bled Strategic Forum' lilionza tarehe 31 Agosti na litafungwa tarehe 2 Septemba 2021. Bled Strategic Forum (BSF) ni jukwaa la kipekee la kujumuishana linalowaleta pamoja washiriki kutoka pande zote za jamii. Jukwaa hili linajengwa juu ya mafunzo waliyojifunza kutoka zamani na linajaribu kutoa sehemu yake ya mchango wa mawazo katika kuunda maisha yao ya baadaye yaliyo bora. Ni jukwa ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2006, na kwa maana hiyo baada ya hilo Kardinali atakuwa huko Madrid, Hispania kwa ajili ya Mkutano wa II wa viongozi Katoliki wa Amerika ya Kusini; vile vile ataendelea kusindikiza hija Papa Francisko nchini Hungaria katika mji wa Budapest na Slovakia inayotarajiwa kuanzia tarehe 11 hadi 17 Septemba 2021.

Katika ajenda hiyo Kardinali ameweza kujibu mwaliko wa Rais ili kushirishi maadhimisho ya miaka 30 ya Uhuru wa nchi ya Slovenia. Katika fursa hiyo Kardinali Parolin, Jumanne tarehe 31Agosti ameongoza misa Takatifu katika madhabahu ya Mama Maria wa BREJZE, Slovenia. Akianza mahaburu ametanguliza kuwaslimu na kutoa salamu kwa niaba ya Baba Mtakatifu. Akidadavua somo lakwanza (taz 1 Tm 2, 1-2), amesema Mtume Paulo anasema: "kabla ya mambo yote, kuomba, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, kuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu". Hili ndilo lilikuwa lengo la Misa kwa kuwakumbuka wote na kila mzalendo katika nchi hiyo, mamlaka hadi kufikia aliyezaliwa siku hiyo kwa namna ya pekee wale ambao wanateseka kimwili na kiroho, amesema Kardinali.

Kwa wakristo na uzalendo wa nchi ni thamani kubwa. Upendo wa nchi, alisema Papa Francisko akiwa nchini Chile mnamo 2018 kuwa ni upendo wa thamani. Huo ni kweli kwani katika sehemu nyingine Mtakatifu Paulo anathibitisha kwamba: “wenyeji wetu uko mbinguni”; (Fil, 3,20; 2 Cor 5,1). Kardinali Parolin ameongeza kuwa, pamoja na hayo hali halisi ya nchi inaundwa na thamani za watu za kweli hata kama sio za kipekee na zilizo za juu.  Kila nchi yenye uzalendo wa uhuru na demokrasia na mahali ambapo kanuni msingi za haki, heshima ya haki za binadamu, haki ya wema wa pamoja, zinahamasisha na mahali ambapo umeenea utamaduni wa kidugu, kwa kutoa bure na mshikamano wa upendo ndiyo thamani kubwa kwa sababu zinaunganisha moja kwa moja na hadhi ya binadamu. Kwa upande mwingiene, amesema mazingira ya kijamii ya amani na usalama ndani ya kila nchi inahakikishwa hata kwa vipimo ambavyo vinapingana na matukio ya kimataifa.

Kardinali Parolin akitazama miaka 30 tangu kupata uhuru nchini Slovenia, akifikitia ukuu wake pia kutoa shukrani ya kumbukizi ya miaka 25 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea nchi yao amesema kwamba alikwenda hata katika madhabahu ya Brezje ili kuikabidhi taifa hilo kijana kwa ulinzi wa Bikira Maria Mama wa Mungu. Ni mama ambaye kwa karne nyingi watu wamefanya ibada kama mama wa Msaada na Msimamizi ambaye anaendelea kuwapo hata leo hii katika nyakati zao. Wakati wa ziara yake Papa Yohane Paulo II alisisitizia furaha yake kwa ajili ya nchi ya Slovernia kuwa na uhuru kwamba ziara ya kwanza ya papa kichungaji nchini Slovenia imetokea baada ya kufikia uhuru. "Haki hii, ni moja ya historia ya watu wetu, inakuwa ndiyo sababu ya furaha kwa uwepo wangu kati yenu". Kardinali amesema kuwa waanzilishi wa Umoja wa Ulaya walikuwa wakristo waaminifu katika ulazima wa kutafuta kama Yesu anavyosema kuwa Ufalme wa Mungu na haki kwa sababu wanaweza kupewa haya wengine mali ambayo sisi tunahitaji kwa ajili ya maisha yenye adhi. (taz, Mt 6,13). Yesu anawakilisha misingi ya ukweli na picha ya nyumba iliyojenga juu ya mwamba na katika nyumba iliyojengwa juu ya mchanga kwenye Injili iliyosomwa (Mt 7, 24 – 28).

Je mwamba huo ni upi ambao unawezesha nyumba kuvumilia matukio yote ya hewa na ngumu sana ambayo leo hii tunafanya uzoefu daima kwa sababu ya maabadiliko ya tabiachi? Kardinali ameuliza na kujibu kwamba " ni Neno la Mungu ambalo Yesu anatangaza, kusikilizwa na kujikita katika matendo. "Yeyote anaye sikiliza maneno yangu na kujikita katika matendo atakuwa kama mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake katika mwamba. Kanisa kwenye mchakato wake wa kuwap hasa katika karne za mwisho kwa na ya pekee haukuacha kamwe kupe, katika mambo yake mengi na ulazima wake kama (familia, makundi na vyama, jumuiya za kisiasa kitaifa na kimataifa) na lazima kuwa na msingi wa Neno la Mtungu, kulisikiliza na kuliweka katika matendo ya dhati. Mafundisho jamii ya Kanisa kwa namna hiyo ndiyo yanajieleza na kuweka bayana ujumbe huo, amesisitiza kardinali Parolin. Ni mwaliko kwa namna hiyo wa Yesu anaouto katika Injili kwa wote waliuganika katika Kanisa na kila mmoja kadiri ya wito wake, na uwakijibikaji wake wa kujenga daima nchi hiyo ikiwa imefikia miaka 30 ya uhuru wake na Ulaya iliyounganisha na jumuiya ya kimataifa katika mwamba wa Neno la Mungu yaani katika msingi ya ukweli, haki, uhuru na upendo. Ukweli wakati mwingine unaonekana kuwa mwangaza wa sura ya Bwana aliyesulibiwa na kufufuka.

Anayemfuata Kristo anafanya vile vile na ndiyo hivyo leo hii Kardinali Parolin amesema wanataka kukumbusha. "Ni ukweli unaotufanya kuwa huru, kwa maana hiyo uhuru dhidi ya mitindo ya utumwa na vielelezo vya kusonga hadhi ya mtu, kuunda uhuru wa sura na mfano wa Muumba wake akijumuishwa haki zake msingi na uhuru wa kufanya mema".  Mtakatifu Paulo anashauri kuwa: “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo (taz Gal. 5,13). Papa Francisko katika Waraka wake wa 'Fratelli tutti', yaani 'Wote ni ndugu', anasema “Tunahitaji kujifunza jinsi ya kufunua wazi kutoka katika barakoa kwa njia ambazo ukweli hutumiwa, hupotoshwa na kufichwa katika mazungumzo ya umma na ya kibinafsi (Ft. 208) Ukweli unaundwa katika upendo. Unakuwa huru kwa ajili ya kupenda na kupenda ili kuwa huru. Kwa hakika ngazi ya kwanza ya upendo ni haki moja ya mihimili ambayo lazima ijengwe nyumba yetu.

Haki ina maana tofauti, lakini kimsingi tunaweza kuifafanua kama nia ya kila wakati na ya kudumu ya kumpa kila mmoja haki yake. Bila kusudi hili la kila wakati na la milele, hakuna hata upendo. Lakini upendo unapita zaidi ya yote, unajaza heshima na haki, kwa sababu unatoa zaidi, unashinda kile kisichostahili na mipaka kwa bure tu. Kristo, akiwa na mikono wazi msalabani, anaonesha Moyo wake bila kinga, katika tendo kuu la upendo kwa wanadamu wote. Huu ni mwamba wa mwisho kushikamana bila woga, ambao tunaweza kujenga utu wetu na jamii zetu, amesisitiza Kardinali Parolin. Sheria, kama ilivyo sawa, zinasimamia haki na wajibu kati yetu, lakini upendo unatuongoza kujitolea wenyewe, bila mahesabu na bila faida. Upendo unahitaji zaidi kuliko wajibu, lakini ni mwema; hauna hofu, bali imani. Ni upendo ambao Mtakatifu Paulo anasema ni wenye fadhili, sio wivu, haujisifu, haukujivuna, haukosi heshima, hautafuti masilahi yake mwenyewe, haukasiriki, hauzingatii uovu! haufurahii udhalimu lakini unafurahia ukweli”(1 Kor 13: 4-6). Upendo huo, tunda la ukweli, uhuru na haki, amesema Kardinali watajiuliza wenyewe, nchi ya Slovenia, Ulaya na kwa ulimwengu wote katika Misa hiyo Takatifu, kupitia maombezi ya Maria Mtakatifu mama Msaada wa Wakristo.

01 September 2021, 14:59