Hija ya kitume ya Papa Francisko Slovakia:wakristo wawe wasukaji wa mazungumzo

Papa Francisko amehitimisha ziara yake ya kitume Jumanatano Septemba 15 katika madhabahu ya Šaštín,katika siku kuu ya Mama Maria wa Mateso Saba,msimamizi wa Slovakia.Waamini 60elfu wameshiriki tukio hilo.Baadaye Papa Francisko ameagwa rasmi katika uwanja wa ndege na kurudi jijini Roma tayari kuendelea na utume wake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mahubiri yake Papa amewapa onyo la kutupunguza imani katika sukari ambayo inaleta utamu wa maisha. Mbele ya Yesu huwezi kubaki umesimama ukiwa umevaa viatu miguu miwili. Kwa maana hiyo ametoa mwaliko wa kuwa katika hija ya safari daima na kwamba Kanisa linaposimam, basi lipenda. Na wakati wa kuaga Nchi hiyo Papa amewambia jinsi ambavyo anawapeleka wote ndani ya moyo wake. Habari katika picha zinaonesha matukio halisi ya  siku hii.

Papa Francisko akiagana na Rais na kupanda ndege ya kurudi Roma. Mara baada ya kusali pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Slovakia, kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Šaštin Papa Francisko amerejea jijini Vatican.

Papa akiagana na Rais na kupanda ndege kurudi Roma
Papa akisalimiana na Rais wa Nchi kabla ya kurudi Roma
Papa akisalimiana na Rais wa Nchi kabla ya kurudi Roma

Video inaonesha wakati muhimu wa Misa Takatifu katika madhabahu ya Mama Maria wa Mateso saba.

Papa akiadhimisha Misa Takatifu
Papa mbele ya Mama wa Mateso saba
Papa mbele ya Mama wa Mateso saba
Mama wa Mateso saba
Mama wa Mateso saba
Papa akitoa mahubiri
Papa akitoa mahubiri
Papa akitoa mahubiri
Papa akitoa mahubiri

Huu ulikuwa ni wakati mwingine wa kipekee wa Papa Francisko kukutana na Jumuiya ya Warom. Jumanne tarehe 14 Septemba 2021, Papa amepata nafasi ya kutembelea Jumuiya ya Warom wanaoishi huko Luník IX. Hili ni eneo la watu maskini ambalo kimsingi linakosa mahitaji muhimu ya binadamu. Watu wote wanapaswa kushirikishwa katika mchakato wa maendeleo fungamani ya binadamu, ili kulinda na kudumisha: utu, heshima na haki msingi za binadamu Papa Francisko amesema ndani ya Kanisa hakuna mgeni wala “mtu wa kuja” wote ni watoto wa Mungu walioumbwa kwa sura na mfano wake.

Papa alikutana na Jumuiya ya Warom
Papa alitembelea Jumuiya ya Warom
Papa alitembelea Jumuiya ya Warom
Papa alitembelea Jumuiya ya Warom
Papa alitembelea Jumuiya ya Warom

Sherehe za kuaga Papa Francisko akiwa uwanjani kurudi Roma.

Sherehe za kuagwa akiwa uwanja wa ndege kurudi Roma
Mavazi ya utamaduni wa Slovakia
Mavazi ya utamaduni wa Slovakia
Makaribisho ya waamini
Makaribisho ya waamini
Kwaheri ya kuonana
Kwaheri ya kuonana
15 September 2021, 16:40