Hija ya kitume ya Papa Francisko Budapest:maoni ya Andrea Tornielli

Katika Video inaonesha Dk. Andrea Tornielli,Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano akitoa maoni yake kuhusu hali ilivyokuwa ya Papa Francisko katika mji mkuu wa Hungeria kwenye mikutano ya kina asubuhi ya leo.

Katika hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Hungaria, Dominika tarehe 12 ametua katika mji wake, ambampo Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anatoa maoni yake kuhusu hali ilivyokuwa mara tu baada ya hitimisho la misa Takatifu. Katika maelezo hayo anasema: Akihitimisha Kongamano la Kimataifa la Ekaristi kutoka uwanja wa Mashujaa huko Budapest, Papa Francisko anakumbuka kwamba Mungu wa Kikristo alijifanya mtumishi kwa kutufia. Kwa maana hiyo safari ya Kikristo sio kufuata mafanikio, lakini huanza na kurudi nyuma, kwa kuondoa kujiweka katikati ya maisha ili kutoa nafasi kwa ajili ya Mungu aliyekufa msalabani, kumkaribisha kulingana na mantiki ya kimungu ya kutoa huduma, na sio kulingana na matakwa ya mwanadamu ya kutumia nguvu na ushindi.

Baada ya salamu fupi kwa watu wenye mamlaka, miongoni mwao alikuwa Waziri ni Mkuu Orban, katika mikutano iliyotangulia misa ya kuhitimisha Kongamano ambalo limekaribisha hapa Kanisa lote kutoka ulimwenguni, Baba Mtakatifu Francisko amewaalika maaskofu wasijifungie katika ugumu wa kujilinda, kwa kile kinachoitwa kitambulisho chetu “lbadala yake ni kujifungulia mkutano na mwingine na kukuza pamoja ndoto ya jamii ya kidugu”. Amewaalika kila wakati kufuata mtindo wa Mungu, ambao ni wa ukaribu, huruma na upole. Amewasihi wasitumie maneno ambayo yanaashiria umbali na kutoa hukumu, lakini yawe yale ambayo yanasaidia kutazama siku zijazo kwa ujasiri.

Kukaribisha, ufunguzi wa mmoja na mwingine na kujenga madaraja zilikuwa mada ambazo Papa amesisitiza kwa wawakilishi wa makanisa mengine ya Kikristo na wajumbe wengine wa jumuiya za Kiyahudi. Akiwageukia hasa hawa wa mwisho, Papa amezungumzia tishio la kupambana na hatari inayo ukumba Uyahudi, ambalo bado lipo Ulaya na mahali pengine, na kusema kwamba “ni hatari ambayo inapaswa kuzimwa.

12 September 2021, 15:11