Janga la UVIKO-19 limeonesha tofauti kubwa za kiuchumi na kijamii katika suala la kiafya. Janga la UVIKO-19 limeonesha tofauti kubwa za kiuchumi na kijamii katika suala la kiafya. 

Askofu Mkuu Paglia:upatikanaji wa chanjo ya Uviko ni msingi

Janga,changamoto zake na swali la afya ya umma katikati ya Mkutano wa Chuo cha Kipapa cha Maisha mwishoni mwa mwezi.Rais wake amesema lazima kushinda mapungufu na kila mtu ana haki ya kupata matibabu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ili kutunza afya lazima kwanza tuwe hai! Kwa nchi za Magharibi, kipaumbele kinawakilishwa na chanjo na kiukweli tunashuhudia juhudi kubwa zaidi ya chanjo iliyowahi kutekelezwa katika historia. Hivi ndivyo Askofu mkuu Vincenzo Paglia, rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha amewasilisha katika Mkutano wa 2021 wa Chuo yenyewe, ambao utafanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba, kwa njia ya uso kwa uso na mtandanoni, wakiongozwa na kaulimbiu: ‘Afya ya umma katika mtazamo wa ulimwengu. Janga, Bioethics, na wakati ujao’.

Chanjo ni msingi kwa ajili ya kudhibiti Uviko-19: Kwa idadi kubwa ya watu ulimwenguni pamoja na chanjo, ufikiaji wa kweli na bora wa matibabu ni kipaumbele, ameeleza Askofu Mkuu Paglia, lakini pia kwa mali zinazoruhusu kuishi. Kwa hivyo mapungufu yanayohusu sio chanjo tu, bali pia ufikiaji wa afya ya umma lazima yashindwe, kwani janga limeonesha tofauti kubwa za kiuchumi na kijamii katika suala la afya. Kwa mawazo ya Askofu amesema, chanjo ni msingi katika mtazamo wa ulinzi wa ulimwengu dhidi ya Covid-19, lakini swali kuu linahusu uwezekano wa kushinda tofauti kweli na haraka, kwa kutekeleza sera ya afya ya ulimwengu kulingana na haki ya wote kupata matibabu.

Mkutano utaudhuriwa na wataalam kutoka mabara matano:Katika mkutano huo utahudhuriwa na wasomi na wataalam kutoka mabara matano, ambao watajadili juu ya Covid-19 na uzoefu wa janga hili, ili wakati huo kuweza kuchangia mjadala juu ya afya ya umma na juu ya shida ambazo changamoto ya afya imeangazia. Washiriki watakao jumuika miongoni mwake yupo Jules Hoffman (Tuzo ya Nobel ya Tiba 2011), John Nkengasong (Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa, Cameroon), David Barbe (Rais wa Jumuiya ya Madaktari Duniani), Carissa Etienne (Mkurugenzi wa Pan American Health. Chama), na Walter Ricciardi (Chuo Kikuu cha Katoliki cha Moyo Mtakatifu).

Mkutano na Papa Francisko na Tuzo ya kulinda Maisha: Kwa Wanataaluma kutakuwa na nyakati mbili zilizohifadhiwa: mkutano na Baba Mtakatifu Francisko asubuhi  tarehe 27 Septemba na,na  jioni ya Septemba 28, kutakuwa na afla ya kutoa tuzo ya Ulinzi wa maisha, iliyoanzishwa na ambayo itapelekwa kwa Dale Recinella, mchungaji mlei  ambaye anahudumia katika mkono wa kifo wa gereza kubwa huko Florida Marekani na ambaye atahudhuria Mkutano huo.

12 September 2021, 11:44