SR ALESSANDRA SMERILLI SR ALESSANDRA SMERILLI 

Sr. Smerilli ni Katibu wa Mpito wa Baraza Kipapa la Maendeleo fungamani ya binadamu

Mtawa ambaye amekuwa Katibu msaidizi tangu Machi 2021,anachukua nafasi ya muda iliyokuwa ya Monsinyo Bruno Duffé aliyemaliza muda wake na ambaye sasa na Padre Augusto Zampini, wa Argentina anarudi kuendelea na huduma yake katika jimbo lake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa amemteua Sr. Alessandra Smerilli kuwa katibu wa kipindi cha mpito cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binafamu na mwakilisho wa Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19, akichuchua nafasi ya Monsinyo Bruno Marie Duffé aliyemaliza muda wake mwezi Jualia pamoja na Katibu msaidizi mweingine wa Baraza hilo Augusto Zampino ambao wote wawili wamerudi katika majimbo yao kuendelea na huduma ya kichungaji. Kwa mujibu wa maandiko ya taarifa iliyotolewa tarehe 26 Agosti kwa waandishi wa Habari Vatican, inasema Baba Mtakatifu kwa hivyo ameelekeza kuwa Tume ya Vatican ya Covid-19 iundwe na Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza hilo, Sr. Alessandra Smerilli, na Padre Fabio Baggio, Katibu msaidizi wa kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi.

Sr. Alessandre Smerilli ni Mzaliwa wa Vasto (Chieti) Italia mnamo 1974, na tangu Machi 2021 alikuwa katibu msiaidizi wa baraza hilo pia mratibu wa Kikosi cha Uchumi cha Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19. Mtawa huyo kama katibu wa kipinid cha mpito anachukua nafasi ya Monsinyo Bruno-Marie Duffé, ambaye amemaliza muda wake wa usimamizi tangu Julai mwaka na pia anachukua nafasi ya Padri Augusto Zampini kama mjumbe wa Kikosi Kazi ya Covid-19, ambapo  Padre huyo anaondoka katika Baraza hilo na kurudi kutoa huduma katika jimbo lake nchini Argentina.

“Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa jukumu ambalo nimeitwa kufanya na ninamuomba Bwana anisaidie kuheshimu wito huu kwa roho ya kutii Kanisa; kwa unyenyekevu, shauku, ubunifu na ustadi wa kusikiliza ambao unahitaji. Shauku yangu na kujitoa ni kuweza kutumikia vyema utume wa Kanisa, kwa wakati ambao Papa anaona unafaa”, amesema hivyo Sr.  Smerilli mara baada ya kupata taarifa hiyo. Baada ya kuwashukuru wakuu, amesema ana uhakika kwamba anaweza kutegemea roho ya ushirika na ushirikiano wa Baraza nzima, na pia washirika wengi wa kimataifa wanaoshirikiana na Tume ya Covid, kwa kuhamasisha mbinadamu fungani na utunzaji ulioundwa kwa kuamasisha na kukuza kanuni hizo za mafundisho jamii ya Kanisa ambalo Baba Mtakatifu Francisko antukumbusha kila wakati kwa ajili ya ujenzi wa ulimwengu bora.

Taarifa ya Padri Augusto Zampini pia ilichapishwa katika Tovuti ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamni ya Bindanadamu ambapo anaandika: “Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa kunikabidhi jukumu lenye kudai la kuratibu Tume ya Vatican ya Covid-19 na kutumikia kama Naibu Katibu wa Baraza la Kipapa. Sasa kwa kuwa Tume iko tayari kuingia katika hatua mpya, na kwa muungano na askofu wangu, nimemwomba Baba Mtakatifu Francisko niweze kurudi Jimboni. Nina hakika kwamba chini ya mwongozo wa Sr. Alessandra Smerilli, Tume itaweza kuendelea na mchakato wa uponyaji ili kusaidia watu wote na sayari kutoka katika hali hii ngumu ”.

26 August 2021, 15:20