Olimpiki 2020-2021-TOKYO Olimpiki 2020-2021-TOKYO 

Olimpiki:Miduara mitano ya olimpiki kuwakilishamabara.Ni ishara ya udugu

Michezo ya Tokyo imeitimishwa Jumapili tarehe 8 Agosti lakini kuanzia Agosti 24 Paralimpiki inaendelea.Katika Gazeti la Osservatore Romano limetoa tafakari fupi kwa kuangazi ishara kadhaa zinazo zungumzia juu ya ushiriki zaidi kwa ushindani na matokeo yake.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kusema ukweli, Michezo ya Olimpiki ya Tokyo haikuishia kufungwa Jumapili tarehe 8 Agosti tu kwani kuna mapumziko ya kiufundi ya wiki mbili (kidogo kama kati ya nusu ya kwanza na ya pili ya mechi ya mpira wa miguu) na Jumanne tarehe 24 Agosti inaanza tena ile ya Paralympics. Kwa maana hiyo Michezo huko Tokyo itaisha Jumapili tarehe 5 Septemba 2021, hasa kwa kumalizia na hiyo Paralympics. Kwa maana nyingine watapitisha kijiti kwenda Beijing, ambayo kuanzia tarehe 4 Februari 2022 itakuwa ndiyo mwenyeji wa Olimpiki na Paralympics za msimu wa baridi.

Sehemu ya kwanza ya Michezo ilimalizika kweli tarehe 8 Agosti na mbio za mwendo kasi ambazo tunaweza kusema ni alama ya mbio, ikishinikiza maisha ya kila mtu. Lakini pia ni  ishara ya kuchochea katika kuvuka mstari wa kumaliza na kugeuza viwango vya uchumi na viwango vya Pato la Taifa ambavyo daima ni kwa wanariadha kwa kile kinachoitwa ulimwengu wa tatu. Katika mashindano ya mbio za Olimpiki alishinda Mkenya Eliud Kipchoge, kwa sala za mama yake Janet kila ushindi wa mtoto wake. Mama huyo amekuwa anakwenda misa katika Kanisa la kijiji chake cha Kapsisiwa ili kutoa shukrani kwa Mungu. Hata hivyo katika mbio za uchovu, Waafrika wamekuwa ndiyo wanashinda, hata wakati wakiwa wamevaa fulana ya nchi iliyowakaribisha.

Eliud Kipchoge wa Kenya akisheherekea medali yake huko Tokyo Japan
Eliud Kipchoge wa Kenya akisheherekea medali yake huko Tokyo Japan

Katika wimbo wa Olimpiki wa Tokyo Jumamosi tarehe 7 Agosti kulikuwa na mwingine  ambayo tunaweza kusema ni sherehe ya kukaribisha, kwa hakika cheti cha michezo. Bingwa wa ulimwengu Timothy Cheruiyot wa Kenya katika mbio za mita 1500 na raia wa Norway Jakob Ingebrigsten ambaye alipata ushindi wa medali ya dhahabu na, mara tu baada ya kumaliza, alimbatiza kuwa ni Mwafrika kwa hiari, na aliyemvalisha bangili na rangi za Kenya kwenye mkono wake. Kwa kifupi, alimkaribisha, mwenye nguvu ya mbio kutoka kusini mwa ulimwengu  na akamfungulia mikono yake na kuijumuisha ile ya Kaskazini.

Mshindi wa Pili Timothy Cheruiyot akisheherekea na bendera ya taifa baada ya mbio za mita 1500
Mshindi wa Pili Timothy Cheruiyot akisheherekea na bendera ya taifa baada ya mbio za mita 1500
Timothy akimvalisha bangili mkononi mshindi wa medali ya dhahabu Jakob Ingebrigtsen wa Norway
Timothy akimvalisha bangili mkononi mshindi wa medali ya dhahabu Jakob Ingebrigtsen wa Norway

Olimpiki ni historia za wanawake na wanaume ambao leo hii hawawezi kumaliza vita vya tatu vya ulimwengu vilivyo gawanyika vipande vipande lakini wanapendekeza uwezekano wa ubinadamu wa kindugu zaidi. Baba Mtakatifu Francisko akizungumza kwa timu yake, tarehe 29 Mei iliyopita alisema kwamba kila kitu kinachomhusu mwanadamu kiko katika moyo wa Kanisa. Na kwa sababu hiyo ni muhimu sana pia kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Utamaduni, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imeongeza neno la Kilatino Communiter yaani Pamoja katika kauli mbiu ya Olimpiki.

Na mara moja wanariadha wawili  Mutaz Ezza Barshim wa Qatar na Gianmarco Tamberi mwitaliano walichagua kushiriki medali ya dhahabu katika kuruka juu na kuwaondoa wale ambao wanataka ushindi kwa nguvu. Kumbe ni kweli kwamba inawezekana kubadilisha utamaduni wa ushindi kwa gharama yoyote na unaweza kushinda pamoja kwa neno moja  kiukweli ni Communiter.

Ushindi wa medali ya dhahabu ya pamoja kwa Mutaz Ezza Barshim wa Qatar na Gianmarco Tamberi wa Italia
Ushindi wa medali ya dhahabu ya pamoja kwa Mutaz Ezza Barshim wa Qatar na Gianmarco Tamberi wa Italia

Gazeti la Osservatore Romano limechapisha hata hivyo picha katika ukurasa wa kwanza baadhi ya historia za Olimpiki. Kwanza kabisa wasifu wa Timu ya Wakimbizi. Na huko Tokyo pia kuna Saamiya Yusuf Omar. Kwenye Michezo ya Beijing mnamo 2008, alikuwa na umri wa miaka kumi na saba na alichezea Somalia kwa kumaliza na mita 200. Saamiya alikuwa na tumaini la kurudia uzoefu wa Olimpiki huko London mnamo 2012,  lakini alifariki katika pwani ya Lampedusa, kwa kuzama kwa mtumbwi ambapo alikuwa amewekeza ndoto yake kama msichana. Huko London, pia, labda angemaliza au labda ulikuwa ndiyo mwisho. Lakini kwanza yumo katika orodha ya wale ambao wanajua jinsi ya kutumaini dhidi ya tumaini lote.

Miduara mitano ya mabara matano ni ishara ya udugu
Miduara mitano ya mabara matano ni ishara ya udugu

 

 

 

09 August 2021, 16:18