2021.08.24 Hii ni Setempu mpya  inayoonesha miaka 100 ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu 2021.08.24 Hii ni Setempu mpya inayoonesha miaka 100 ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu  

Miaka 100 ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu

Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu kinafanya maadhimisho ya miaka 100 mwaka huu na kilianzishwa na Padre Agostino Gemelli mnamo 1921.Kampasi zake nchini Italia,Milano,Piacenza,Cremona,Brescia na Roma.Kufuatia na fusra hiyo imetengenezwa stempu mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tangu tarehe Mosi Novemba 2020, kulizinduliwa maandhimisho ya mwaka wa 100  tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Katoliki Cha Moyo Mtakatifu nchini Italia, na mwanzilishi wake ni Padre Agostino Gemelli mnamo 1921. Karne moja ya  historia ambayo ipo mbele yetu ndiyo kauli mbiu inayoongoza chuo kikuu hicho muhimu sana.

Kufuatia na fursa ya maadhimisho ya miaka 100, tangu kuanzishwa kwa taasisi kubwa hiyo ya elimu, Posta ya Vatican imetengeneza Stempu mpya ambayo inaonesha ishara za Chuo Kikuu katoliki cha Moyo Mtakatifu.

Ni chuo kikuu katoliki cha Kipapa kikubwa barani Ulaya lakini hata chuo kikuu kimoja wapo cha Italia ambacho kinajivunia ukuu wake wa kitaifa, shukrani kutokana na kampasi zake tano: Milano, Piacenza, Cremona, Brescia na Roma, mahali palipo na Chuo Kikuu cha A. Gemelli. Pamoja na pendekezo la elimu lililojikita katika malezi muhimu ya mtu huyo, Chuo Kikuu kinafaa katika mila na tamaduni za Ulaya  kama mahali pa maendeleo ya kiutamaduni panapowezekana kusoma na kutafsiri ugumu wa ukweli hali halisi ya sasa.

24 August 2021, 15:48