Askofu mkuu  Luigi Pezzuto tarehe 31 Agosti 2021 ameng'atuka kutoka madarakani. Askofu mkuu Luigi Pezzuto tarehe 31 Agosti 2021 ameng'atuka kutoka madarakani. 

Askofu mkuu Luigi Pezzuto Ang'atuka Kutoka Madarakani 2021

Askofu mkuu Luigi Pezzuto alizaliwa kunako tarehe 30 Aprili 1946 huko Squinzano, Kusini mwa Italia. Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Septemba 1971. Tarehe 6 Januari 1997 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu. Amewahili kuwa Balozi: DRC, Gabon, Tanzania, El Salvador, Beliza, Antilles na mwishoni alikuwa huko nchini Bosnia-Herzegovina na Montenegro.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu mkuu Luigi Pezzuto la kutaka kung’atuka kutoka madarakani kama Balozi wa Vatican. Askofu mkuu Pezzuto amewahi kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Monaco, Bosnia, Erzegovina na Montenegro. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Pezzuto alizaliwa kunako tarehe 30 Aprili 1946 huko Squinzano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Septemba 1971.

Tarehe 6 Januari 1997 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu. Tangu wakati huo amekwisha tekeleza dhamana na utume wake wa kidiplomasia nchini DRC, Gabon, Tanzania, El Salvador, Beliza, Antilles na mwishoni aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bosnia-Herzegovina na Montenegro.

Askofu Mkuu Pezzuto
31 August 2021, 14:19