Askofu mkuu Augustine Kasujja kutoka Uganda aliteuliwa na Mt. Yohane Paulo II 26 Mei 1998 kuwa Balozi wa kwanza wa Vatican kutoka Barani Afrika. Askofu mkuu Augustine Kasujja kutoka Uganda aliteuliwa na Mt. Yohane Paulo II 26 Mei 1998 kuwa Balozi wa kwanza wa Vatican kutoka Barani Afrika. 

Askofu mkuu Augustine Kasujja Ang'atuka Kutoka Madarakani 2021

Askofu mkuu Augustine Kassuja alizaliwa kunako tarehe 26 Aprili 1946 huko Mitala- Maria nchini Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 6 Januari 1973. Tarehe 26 Mei 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Balozi wa kwanza kutoka Afrika na kumtumwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Algeria na Tunisia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Augustine Kasujja la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Augustine Kasujja kabla ya kung’atuka kutoka madarakani alikuwa Balozi wa Vatican nchini Luxembourg na na Ubelgiji! Askofu mkuu Kassuja alizaliwa kunako tarehe 26 Aprili 1946 huko Mitala- Maria nchini Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 6 Januari 1973. Tarehe 26 Mei 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Balozi wa kwanza kutoka Afrika na kumtumwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Algeria na Tunisia.

Tarehe 22 Agosti 1998 akawekwa wakfu kuwa Askofu. Kunako tarehe 22 Aprili 2004 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Madagascar, Visiwa vya Usheli sheli, Comoro na Mauritius. Tarehe 2 Februari 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Nigeria. Tarehe 12 Oktoba 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji na mwishoni tarehe 7 Desemba 2016 akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Luxembourg.

Askofu mkuu Kasuhha
31 August 2021, 14:39