Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Raphael Macebo Mabuza Ncube kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Hwange, Zimbabwe. Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Raphael Macebo Mabuza Ncube kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Hwange, Zimbabwe. 

Askofu Raphael Macebo Mabuza Ncube Jimbo Katoliki la Hwange!

Askofu mteule Raphael M. M. Ncube, alizaliwa tarehe 4 Oktoba 1973 huko Bulawayo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Februari 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo kama Padre, amebahatika kuwa Paroko-usu, Paroko na baadaye kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari Ndogo ya Mtakatifu Bernard.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Raphael Macebo Mabuza Ncube kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Hwange, nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Raphael Macebo Mabuza Ncube alikuwa ni Padre mshauri wa maisha ya kiroho kwenye Seminari ya “Saints John Fisher and Thomas More” huko Chishawasha, iliyoko kilometa 25 kutoka Harare, Zimbabwe. Askofu mteule Raphael Macebo Mabuza Ncube, alizaliwa tarehe 4 Oktoba 1973 huko Bulawayo, Zimbabwe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Februari 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tangu wakati huo kama Padre, amebahatika kuwa Paroko-usu, Paroko na baadaye kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari Ndogo ya Mtakatifu Bernard. Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2015 alitumwa kwenda Roma ili kujiendeleza zaidi kimasomo na hatimaye, akafaulu kutunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Somo la Sayansi ya Maisha ya Kiroho kutoka Taasisi ya Kipapa ya Tasaufi ya Teresianum iliyoko mjini Roma. Tangu mwaka 2016 hadi kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francisko amekuwa ni Padre wa maisha ya kiroho kwenye Seminari ya “Saints John Fisher and Thomas More” huko Chishawasha.

Zimbabwe
06 July 2021, 15:56