Papa Francisko amemteua Padre Anthony Pascal Rebello kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Francistown. Papa Francisko amemteua Padre Anthony Pascal Rebello kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Francistown. 

Askofu Anthony Pascal Rebello Jimbo Katoliki la Francistown!

Askofu mteule Anthony Pascal Rebello, S.V.D. alizaliwa tarehe 18 Machi 1950 Jijini Nairobi, nchini Kenya. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, tarehe 10 Mei 1977 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre nchini India. Tangu wakati huo kama Padre kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1979 alijiendeleza kielimu na kufanikiwa kujipatia Shahada ya kwanza katika Elimu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Pascal Rebello, S.V.D., kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Francistown, nchini Botswana. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Anthony Pascal Rebello, S.V.D. alikuwa ni Paroko wa Parokia ya “Holy Cross” huko Mogoditshane. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Anthony Pascal Rebello, S.V.D. alizaliwa tarehe 18 Machi 1950 Jijini Nairobi, nchini Kenya. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, tarehe 10 Mei 1977 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre nchini India. Tangu wakati huo kama Padre kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1979 alijiendeleza kielimu na kufanikiwa kujipatia Shahada ya kwanza katika Elimu.

Na kati ya Mwaka 1979 hadi mwaka 1981 alitumwa nchini Botswana na kuteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Palapye. Kati ya Mwaka 1981 hadi mwaka 1984 alipelekwa nchini Kenya kama mmisionari. Kati ya Mwaka 1984 hadi mwaka 1987 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Kanda Kishirika. Mwaka 1987 hadi mwaka 1990 alitumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu nchini Angola na huko akapangiwa kuwa Paroko, Mlezi wa Wanovisi na huduma za kichungaji Parokiani. Kati ya Mwaka 2000 hadi mwaka 2002 alitumwa India na huko alitekeleza utume wake kama Paroko. Tangu mwaka 2003 akatumwa kwenda Jimbo Katoliki la Gaborone nchini Botswana ambako amekuwa akihudumia kama Paroko na hatimaye amekuwa Paroko wa Parokia ya “Holy Cross” huko Mogoditshane, nchini Botswana!

Uteuzi Botswana

 


 

06 July 2021, 08:26