Tarehe 27 na 29 katika siku kuu ya Mtakatifu Petro na Paulo, makanisa yote ulimwenguni yanatoa mchango kwa ajili ya mfuko wa Mt. Petro Tarehe 27 na 29 katika siku kuu ya Mtakatifu Petro na Paulo, makanisa yote ulimwenguni yanatoa mchango kwa ajili ya mfuko wa Mt. Petro 

Guerrero:sadaka ya Mtakatifu Petro ya kusaidia utume wa Kanisa

Katika mkesha wa kiutamaduni wa kukusanya sadaka ya upendo na huduma ya Papa kwa ajili ya mahitaji ya Kanisa la ulimwengu,Rais wa Sekretarieti kwa ajili ya Uchumi ameonesha takwimu za makusanyo na jitihada za mifuko hiyo."Watu wanayo haki ya kujua jinsi tunavyotumia fedha”.

NA ANDREA TORNIELLI

“Ni muhimu kushirikiana kwa sababu hatuwezi kufikiria kuwa utume wa Kanisa unaweza kujisaidia bila mchango wa waamini. Tangazo la Injili ulimwenguni kote pamoja na yote ambayo yanajumuisha, linahitaji muundo wa msaada”.  Katika mkesha wa makusanyo ya Sadaka ya Mtakatifu Petro, Padre Juan Antonio Guerrero Alves, S.I, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi Vatican ameeleza katika mahojiana jinsi ambavyo fedha hizo za makusanyo zinavyotumika. Ni katika kuingilia kati katika matendo ya upendo na mchango kwa ajili ya huduma ya Papa kwa ajili ya Kanisa na kwa ulimwengu mzima.

Padre Guerrero, watu wengi wanauliza maswali na wanataka kujua juu ya sadaka baada ya habari nyingi zinazopingana.

Awali ya yote, ninataka kusema kwamba watu wanayo haki ya kujua ni jinsi gani tunatumia fedha ambazo tunapewa. Wakati mwingine mapingano yanazaliwa kutokana na ukosefu wa uelewa, ambao wakati mwingine unaweza kupelekea hata ukosefu wa uwazi. Nilipoanza huduma yangu kama Mwenyikiti wa Sekretarieti ya Uchumi, Baba Mtakatifu alioniomba kuwa makini sana katika uwazi. Katika kipindi hicho kwenye (SpE) nilitafuta kushirikishana na waamini takwimu za kiuchumi za Vatican ambazo ninafahamu na ambazo nilifikiri zinaweza kuwa muhimu.

Je Sadaka hii inasaidia nini?

Wanazungumza juu ya upendo wa Papa na ndivyo hivyo. Upendo kwa kawaida ni kutoa sadaka kwa Kanisa mahalia. Taasisi, familia au watu wenye kuhitaji. Lakini hii haihusiani na fedha tu, ambazo zinafika Roma na ambazo Vatican inagawanya katika sehemu mbali mbali ulimwenguni kwa ajili ya matendo ya upendo. Hii ni sehemu tu ya lengo la sadaka hiyo. Kuna zawadi kwa ajili ya sadaka ambazo zinafika na kwa haraka hugawanywa katika mahali ambapo kuna shida. Kwa kutoa mfano kwa kile ninachokifahamu, moja kwa moja: mnamo 2021 tangu niwe chini ya uangalizi na uthibiti wa Sekretarieti ya Uchumi hadi leo hii, Mfuko wa Sadaka umekwisha pokea sadaka ya Euro milioni 21(na bado kunaweza kuwa na kitu kutoka mwaka jana ambacho kilichelewa kufika). Katika hizo euro milioni 8 zimegawanywa kwa ajili ya uinjilishaji au mipango ya kijamii kwa ajili ya Makanisa yenye kuhitaji msaaada na hasa katika Nchi za Afrika, Asia na Amerika Kusini. Maendeleo ya nusu mwaka yanayo tolewa zawadi za moja kwa moja yanaonesha kufanana na miaka iliyotangulia.

Lakini mfuko huo wa sadaka hautumiki tu kwa kazi za hisani …

Kiukweli ni muhimu pia kuelezea na kuelewa sehemu hiyo ya upendo wa Papa inayotazama utume wake katika umoja katika upendo, ambao yeye anauendesha katika mabaraza na katika Taasisi za Jimbo la Roma kwa ajili ya huduma ya Kanisa la Ulimwengu. Sehemu ya bajeti nyingine za baadhi ya mabaraza ya Kipapa ni kuelekeza kwa Makanisa yenye kuhitaji na katika hali ngumu za kibinadamu, lakini kwa kawaiia siyo sehemu msingi ya utume wao na ambayo badala yake ni kutoa huduma yao maalum kwa Kanisa la ulimwengu.  Taasisi hizi za Kipapa hazina mapato yao wenyewe na kwa ujumla hazipati fidia ya kifedha kwa huduma zao wanazotoa. Tufikirie huduma ya umoja wa imani, liturujia, mahakama za Kanisa, mawasiliano ya Papa, utunzaji wa urithi uliopokelewa kwa karne nyingi kwenye Maktaba au kwenye Majalida, ambamo nyaraka muhimu za historia ya ubinadamu huhifadhiwa, wawakilishi wa kipapa ulimwenguni, nk. Huduma hizi zilizowekwa katika Kanisa la ulimwengi hazina vipato vyao na zinasaidiwa na mfuko wa makusanyo ya sadaka.

Mara nyingi wanazungumza juu ya mfuko wa sadaka wa mamilionea. Je! Unaweza kuelezea kwanini sehemu ya makusanyiko ya sadaka yameokolewa kuwa na akiba na kwanini mfuko umeanzishwa?

Kuhusu akiba na ukweli kwamba kumekuwa na mfuko wa mamilioni ya sadaka ambao umekuwepo kwa miongo kadhaa, maelezo kimsingi ni kwamba wakati michango mikubwa isiyo ya kawaida inapofika, kwa mfano urithi mkubwa wa utume wa Papa, siyo busara kuutumia mara moja katika mchakato wa mwaka. Huo unaweza kutumika kwa mujibu wa wakati, ikiwa kunakuwapo na mahitaji zaidi au inawezekana kuunda mfuko kwa ajili ya kusadia wakati wa mipango ya muda mrefu. Kuweka akiba katika miaka ambayo mahitaji yake ni kidogo na ili panapotokea mahitai basi ni jambo muhimu na la busara. Kiukweli, akiba hizi lazima zisimamiwe kwa uangalifu, kulingana na kanuni za mafundisho jamii ya Kanisa, kwa busara ya mtu mzuri wa familia na kwa ufahamu kwamba kile tunachopokelewa kila mwaka hakifuniki gharama zote za utume.

Mgogoro wa uchumi uliosababishwa na janga umeathiri sana makusanyo ya sadaka ya mwisho?

Tayari tumeona kupungua kwa makusanyo katika miaka ya mwisho. Kati ya 2015 na 2019 ukusanyaji umepungua kwa asilimia 23% na zaidi katika upunguaji huu, mnamo 2020, kwa mwaka wa kwanza wa COVID, mapato ya sadaka yalikuwa chini ya 18%. Mgogoro unaohusiana na janga hili huenda ukajifanya usikike tena mwaka huu. Misaada mingine iliyopokelewa ina sehemu maalum inakoelekezwa, na mingine hutolewa kwa ajili ya Baba Mtakatifu kwa ujumla. Mnamo mwaka wa 2019, mkusanyiko wa sadaka ulikuwa euro milioni 53.86, iliyogawanywa kama ifuatavyo: milioni 43 katika utoaji wa jumla wa mfuko wa sadaka na milioni 10.8 kwa ajili ya maeneo maalum walio kayika hali za mahitaji katika Kanisa na ulimwenguni. Mnamo mwaka wa 2020, mkusanyo ulikuwa euro milioni 44.1, uliyogawanywa kama ifuatavyo: milioni 30.3 kwa ujumla wa mfuko wa sadaka na milioni 13.8 kwa ajili ya maeneo maalum.

Je! Unaweza kuelezea vema zaidi unamaanisha nini maeneo maalum?

Tunapozungumza juu ya maeneo maalum au yaliyokamilishwa, tunamaanisha misaada inayolengwa, kwa mfano, kwa ajili ya ujenzi wa makanisa katika nchi za ulimwengu wa tatu, huduma za kijamii kama vile hospitali za watoto au msaada kwa ajili ya shule katika maeneo ya kimaskini, msaada wa uwepo wa jumuiya za kitawa katika maeneo magumu kutokana na vurugu au umaskini, mafunzo ya wahudumu wa kichungaji, n.k. Mipango ya kijamii, katika maeneo haya, ni kama sehemu ya simba. Ikiwa tunapokea mchango na kusudi iliyofafanuliwa tayari na tunalikubali, tunaheshimu mapenzi ya wafadhili. Kwa upande mwingine, katika bajeti za baadhi ya mabaraza ya kipapa kwa mwaka huu wa mapato ya chini, gharama za kusaidia Makanisa katika shida zimeongezeka, kama ilivyo Baraza la Kipapa la maendeleo fungamani ya binadamu, ambalo limeongeza matumizi yake kusaidia hali nyingine ngumu kwa mwaka huu.

Padre Guerrero, kwa nini ni muhimu kushirikiana? Je ni kwanini kutoa sadaka kwa ajili ya mfuko?

Ni muhimu kushirikiana kwa sababu hatuwezi kufukiria kuwa utume wa Kanisa unaweza kujisaidia bila mchango wa waamini. Tangazo la Injili ulimwenguni kote pamoja na yote ambayo yanajumuisha, linahitaji muundo wa msaada. Kanisa limeishi daima namna hii. Kama alivyosema Papa Francisko katika ujumbe wake kwa Baraza la Kipapa la utume wa matendo ya kimisionari, Kanisa limekuwa daima linaendelea na kwenda mbele shukrani kwa mchango wa wajane, michango kutoka kwa watu wengine, na shukrani kwa zawadi ya imani na ambao wanatoa kile ambacho wanaweza. Tayari katika mwanzo wa Kanisa, Mtakatifu Paulo, alianzisha na kuhimiza ukusanyaji kwa ajili ya Kanisa la Yerusalemu, (taz 1 Cor 16,1).  Katika barua zake, mtume anatoa vigezo kadhaa vinavyozingatia kanuni ya ushirikiano wa jumuiya mbali mbali za Kanisa moja. Katika barua, mtume anawapatia baadhi ya mantiki yanayojikita juu ya msingi wa umoja hai.

Mfuko umetajwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari katika miaka miwili iliyopita kwa sababu ya uwekezaji katika mfuko wa wamiliki wa jengo la Sloane Avenue huko London: je pesa nyingi zilipotea na operesheni hii?

Hii ni hisotria chungu. Ni kweli kwamba kila wakati kuwa katika uwekezaji wakati mwingine unapata na wakati mwingine unapoteza. Lakini ikiwa kumekuwa na kasoro, lazima tuielewe na tuwaadhibu waliohusika. Uwekezaji wa sadaka kijadi ulikuwa kwenye kikapu pamoja na uwekezaji wa fedha nyingine zilizopewa Sekretarieti ya Vatican. Haikuwa rahisi kusema kwamba sehemu hii, hizi hisa au jengo hilo ni la mfuko na hii ni ya mifuko mingine. Kama nilivyosema, Vatican imeanza njia ya mchakato wa uwazi na njia hii pia inajumuisha ufafanuzi wa vipindi visivyo vya wazi. Kinachowezekana kusema, wakati huo huo ni kwamba kushuka kwa thamani na upotezaji wa jengo la London - nadhani ilifanywa kwa kuheshimu michango ya waamini - haikuangukia mfuko wa fedha, bali kwa pesa nyingine zilizoshikiliwa na Sekretarieti ya Serikali. Hii iliamuliwa wakati wa kufanya mgawanyo wa kila mchango wa mfuko wa hasara.

Wameandika kiasi kikubwa, wanazungumzia euro milioni 800? Je! Unaweza kutuambia ni pesa ngapi za mfuko huo?

Kuzungumza euro milioni 800... inaonekana kuwa ya ajabu kwangu! Katika akaunti ambazo nimeona, jumla ya pesa zote za Sekretarieti ya Serikali katika miaka kumi iliyopita zimekuwa chini ya kiwango hiki. Mfuko wa mchango wa mnamo 2015 ulikuwa euro milioni 319. Katika miaka ya hivi karibuni wametumia wastani wa euro milioni 19 zaidi ya zile walizokusanya. Mfuko wa wa mkusanyo, kuanzia 31 Desemba 2020 ulikuwa, takriban euro milioni 205, sehemu ya hizi katika uwekezaji mdogo wa cash pamoja na jengo maarufu huko London. Mfuko wa mchango umepunguzwa kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na gharama za mabaraza ya kipapa, ambayo yanahitaji zaidi ya ile iliyokusanywa. Ni dhahiri kwamba hii haiwezi kuwa hivyo tena.

Je ni nani anasimamia mifuko ya fedha hiyo?

Michango ya Mfuko wa fedha hadi mwaka jana ilikuwa imekusanywa na kusimamiwa na Sekretarieti ya Nchi. Mnamo Desemba 2020, ilichapishwa barua ya Motu proprio ambayo pesa zilihamishiwa APSA. Kwa upande wa ukusanyaji, sehemu kubwa inatoka katika makanisa wakati wa mkusanyiko wa sikukuu ya Mtakatifu Petro ya tarehe 29 Juni. Mwaka jana katika nchi nyingi, kwa sababu ya kufungwa kwa makanisa kwa sababu ya janga, mkusanyo ulihamishiwa mnamo tarehe 4 Oktoba katika sikukuu ya Mtakatifu Francis. Mwaka huu itakuwa Siku ya Mtakatifu Petro tena. Makanisa binafsi hutuma mkusanyo katika majimbo, na majimbo hupeleka ubalozi wa kitume, ambao nao hutuma Roma.

Waamini wengi hutoa moja kwa moja kupitia ukurasa wa wavuti au kwa kuhamisha moja kwa moja kwenye akaunti za IOR. Kufuatia na kile ambacho kiliandikwa kwenye Motu proprio ya Desemba iliyopita, inalingana na hitaji la kuhakikisha uwazi zaidi, katika utofautishaji wa kazi katika umoja wa utume. Vatican ni moja. Sisi sote tuko katika utume wa utume wa Papa, Mfuasi wa Petro. Uendeshaji na usimamizi wa mfuko na mapato sasa ni jukumu la APSA, ingawa, kiukweli, Sekretarieti ya Nchi, ambayo kupitia balozi za kitume inajua vizuri mahitaji ya Makanisa na nchi, ndiyo inayoteua mipango ya kusaidia. Udhibiti wa mapato na matumizi ni jukumu la Sekretarieti ya Uchumi, ambapo Ofisi ya Mfuko iko sasa. Tunatumaini haraka iwezekanavyo kuweza kutoa hesabu sahihi kwa waamini kwa kila kitu kinachohusu Mfuko wa Mtakatifu Petro, kuanzia mapato na matumizi.

25 June 2021, 15:17