Papa Francisko amemteua Askofu Lazarus You Heung-sik kutoka Jimbo Katoliki la Daejeon kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri. Papa Francisko amemteua Askofu Lazarus You Heung-sik kutoka Jimbo Katoliki la Daejeon kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri. 

Askofu Mkuu L. You Heung-sik M/Kiti Baraza la Kipapa la Wakleri

Askofu mkuu Lazarus You Heung-sik alizaliwa tarehe 17 Novemba 1951 huko Nonsan-gun Chungnam. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 9 Desemba 1979 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mt. Yohane Paulo II tarehe 9 Julai 2003 akamteuwa kuwa ni Askofu mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Daejeon na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 1 Aprili 2003.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Lazarus You Heung-sik wa Jimbo Katoliki la Daejeon {Taejon}, Korea ya Kusini, kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wakleri na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Askofu mkuu Lazarus You Heung-sik alizaliwa tarehe 17 Novemba 1951 huko Nonsan-gun Chungnam. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 9 Desemba 1979 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 9 Julai 2003 akamteuwa kuwa ni Askofu mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Daejeon {Taejon}, na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 1 Aprili 2003. Na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 11 Juni 2021 akamteuwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wakleri na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu.

Askofu mkuu Lazarus You Heung-sik akiwa nchini Korea ya Kusini licha ya majukumu na wajibu wake wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifu watu wa Mungu, alibahatika kuteuliwa kuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Korea ya Kusini. Ni katika muktadha huu, amewahi kutembelea Korea ya Kaskazini ili kunogesha mchakato wa uponyaji na maridhiano kati ya Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Egidio Miragoli wa Jimbo Katoliki la Mondovì kutembelea na kukagua ofisi za Baraza la Kipapa la Wakleri. Amefanya hivi pia kwa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa. Bila shaka huu unaweza kuwa ni utaratibu mpya utakaotumika wakati wa kubadilishana uongozi kwenye Mabaraza ya Kipapa!

 

12 June 2021, 14:37