Papa Paulo VI (Giovanni Battista Montini) Papa Paulo VI (Giovanni Battista Montini)  Tahariri

Watendaji wapya na jukumu la Papa la kuwa “mtetezi wa maskini”

Miaka hamsini iliyopita ya“Octogesima adveniens”,Paulo VI alizungumzia uhamiaji mkubwa kuelekea kwenye miji,hadhi ya wanawake na wingi wa chaguzi za kisiasa.Alikosoa maoni ya Marxi na huria.Kwa kuwasilisha Barua hiyo,alitetea “haki na wajibu” wa Kanisa kujieleza juu ya masuala ya kijamii.

ANDREA TORNIELLI

Maneno ya kinabii juu ya kile ambacho mrithi wake Papa Franciko leo anakiita “waliotupwa”. Uchambuzi wa kweli wa kukosekana kwa usawa mkubwa na matokeo ya mkusanyiko mkubwa wa miji. Ukosoaji wa itikadi ya Kimarx na kutokuamini kwake kwamba kuna Mungu, lakini pia kukosoa itikadi huria ambayo kabla ya miaka ishirini baadaye ingeweza kuenea, huku ikitengeneza njia za ubepari. Ilikuwa mwaka wa 1971, ambapo mnamo tarehe Mei 14, Papa Paulo VI alikuwa anadhimisha miaka 80 tangu kuchapishwa Waraka wa Rerum novarum wa Papa Leo XIII na barua ya kitume  inayohusu amasuala ya watendaji kazi au wafanya kazi iliyoelekezwa kwa Kardinali Maurice Roy, Askofu mkuu wa Quebec na Rais wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani wa wakati huo. Hati ya Montini, inayozungumzia umaskini na maendeleo na jitihada za kisiasa, inapaswa kusomwa katika mwelekeo wa Hati ya Populorum progressio (1967) yaani ya maendele ya watu, lakini pia katika mwanga wa mabadiliko ambayo yamefanyika katika miaka ya hivi karibuni.

Papa anazungumza juu ya “tofauti dhahiri” ambazo zipo katika maendeleo ya kiuchumi, kiutamaduni na siasa za mataifa”, akiwakumbusha watu wanaopambana dhidi ya njaa. Hati hiyo inasema mitindo ya mantedo ya jitihada na uingiliaji thabiti lazima uachwe katika uamuzi wa hali halisi ya eneo mahalia, kwa sababu “ni juu ya jumuiya za Kikristo zichambua kwa uangalifu hali ya nchi yao, katika mwanga wa maneno ya Injili, ili kutumia kanuni za tafakari, vigezo vya hukumu na maagizo ya utekelezaji katika mafundisho jamii ya Kanisa ”.

Kwa maana hiyo hati hiyo inazingatia umakini juu ya umuhimu wa matukio ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea, kwa maana ya miji, na uhamishaji kutoka maeneo ya vijijini kwenda miji mikuu. Katika kukua kwa fujo hizi kwa dhati, watendaji wapya wanazaliwa. (...) Badala ya kupendelea mikutano ya kidugu na kusaidiana, jiji linaendeleza ubaguzi na hata kutokujali; linachochea aina mpya za unyonyaji na utawala, ambapo wengine, wanafikiria juu ya mahitaji ya wengine, hupata faida isiyokubalika. Nyuma ya pazia kuna shida nyingi, ambazo hazijulikani hata kwa wale wa karibu zaidi”.

Papa Paulo VI, ambaye kama askofu mkuu alikuwa ameona shida za mitaa mipya ya pembezoni mwa Milano wakati wa miaka ya ukuaji wa uchumi, na ambaye hata kama Papa aliendelea kufuatilia maendeleo ya mitaaa ya Roma kwa umakini na msaada halisi. Kwa mfano katika kufadhili ujenzi wa Vyumba 99 katika kata ya Acilia kwa kuwasadia walioishi makazi duni katika jiji, aliandika: “Ni muhimu kujenga upya, kulingana na barabara, mitaa, au mkusanyiko mkubwa, muundo wa kijamii ambao mtu anaweza kukidhi mahitaji ya utu wake. Vituo vya kupendeza na utamaduni lazima viundwe au kuendelezwa katika ngazi ya jumuiya na maparokia”.

Kifungu cha Barua yake pia kinawekwa kwa ajili ya wanawake. Papa Paulo VI, ambaye mwaka uliokuwa umetangulia alikuwa amewatangaza wanawake wawili kuwa madaktari wa Kanisa yaani:  Teresa wa Avila na Catherine wa Siena  na hivyo alitoa wito wa kukomeshwa kwa ubaguzi na sheria ziendanane  “kwa maana ya kulinda wito sahihi wa  mwanamke mwenyewe na pamoja na kuwa na utambuzi wa uhuru wake kama mtu, usawa wa haki zake kwa kuzingatia ushiriki katika maisha ya kiutamaduni, kiuchumi, kijamii na kisiasa”.

Akizungumzia ukuaji wa idadi ya watu katika nchi maskini, Papa Montini alifafanua ile aina ya kusumbua ambayo hatma, yake ni kutawala na ambayo hata inachukua wale waliohusika na wakati mwingine husababisha suluhisho lisilo zuri, ambalo linaonesha juu na propaganda inayofanya kazi kwa niaba ya uzazi wa mpango na utoaji mimba”. Papa pia alizungumzia juu ya mazingira na alionya kwamba “kupitia unyonyaji wa hovyo wa maumbile, mwanadamu ana hatari ya kuharibu na pia kuwa mwathirika wa uharibifu kama huo”.

Akinukuu juu ya jitihada za kijamii na kisiasa, Papa Paulo VI anamwalika mkristo awe makini kutokubali mifumo ya kiitikadi ambayo inapingana sana au kwa ishara kubwa za imani yake na dhana yake juu ya mwanadamu;  wala kwa itikadi ya Kimarxi, kwa kupenda kwake kutokuamini kwamba kuna Mungu, na kwa unyanyasaji wake wa vurugu na njia ambayo inajiingiza tena katika uhuru wa mtu binafsi katika jamii, ikikanusha pamoja mwanadamu na historia yake binafsi na ya pamoja kutoka kwa Mungu; wala itikadi ya huria inayoamini kuinua uhuru wa mtu binafsi kwa kuondoa mipaka yote, ikiichochea kutafuta tu maslahi na nguvu”.

Hatimaye katika kifungu kinachokumbukwa zaidi cha waraka huo, Papa alijieleza kwa kupendelea chaguzi nyingi za kisiasa kwa Mkristo, bila kuacha kufuata kanuni za kiinjili: “Katika hali halisi na kwa kuzingatia mshikamano ambao umefanywa na kila mtu lazima zitambuliwe chaguzi halali zinazowezekana. Imani hiyo hiyo ya Kikristo inaweza kupelekea jitahada tofauti”.

Siku mbili baada ya kuchapishwa kwa Waraka wa Octogesima, Jumapili tarehe 16 Mei, Papa Paulo VI aliongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu  Petro kusherehekea kumbukumbu ya Waraka wa Papa Leo XIII, akifafanua maneno ya mtangulizi wake kama “ya kukomboa na ya kinabii”. Mahubiri yaliwakilisha fursa ya kulezea sababu za mafundisho jamii ya Kanisa, Papa alisema: “Kwa nini Papa alisema? Je! Alikuwa na haki? Je! Alikuwa na umahiri? ndio, tunajibu, kwa sababu alikuwa na jukumu. Hapa ingekuwa suala la kuhalalisha uingiliaji huu wa Kanisa na Papa katika masuala ya kijamii, ambayo ni ya asili yao ya masuala ya kidunia, masuala ya ardhi hii, ambayo utafikiri yanaonesha wazo uwezo wa wale ambao wanapata sababu kutoka kwa Kristo, ambaye alitangaza kuwa ufalme wake siyo  wa ulimwengu huu”.

Lakini, kwa kutazama kwa karibu  Papa Paulo VI anasema,  halikuwa suala kwa Papa wa ufalme wa ulimwengu huu, tuseme kwa urahisi wa  siasa au wa uchumi; ilikuwa ni juu ya wanaume wanaounda ufalme huu, ilikuwa juu ya vigezo vya hekima na haki ambayo lazima pia imuhamasishe; na katika mantiki hii sauti ya Papa, ambaye alikuwa mtetezi wa maskini, alilazimika kubaki maskini katika mchakato wa kuzalisha utajiri mpya, mtetezi wa wanyenyekevu na wanyonywaji, haikuwa jambo jingine isipokuwa mwangwi wa sauti ya Kristo, ambaye alifanya kitovu cha wale wote wanaofadhaika na kuonewa kuwafariji na kuwakomboa; na ambaye alitaka kutangaza  kuwa heri maskini na wenye njaa ya haki, pia alitaka kujionesha katika kila mwanadamu, mdogo, dhaifu, anayeteseka, mwenye bahati mbaya, akichukua  juu yake deni la tuzo isiyo na kipimo kwa mtu yeyote ambaye alikuwa na moyo na dawa kwa kila ya aina ya shida ya kibinadamu”.

Kutokana na hiyo, aliongeza kusema Askofu wa Roma, kwamba ni jukumu la haki la Papa, anayemwakilisha Kristo, na la Kanisa lote, ambalo pia ni Mwili wa fumbo la Kristo, na kiukweli la kila Mkristo halisi, aliyetangazwa kuwa ndugu wa kila mtu, kujali, kufanya kila awezalo kwa ajili ya wema wa  jirani; mwenye nguvu na dharura na kama ilivyo mbaya na ya kusikitisha zaidi ni hali ya jirani anayehitaji”.

Kwa kuhitimisha Papa Paulo VI alisema: “Na pia inamaanisha kwamba Kanisa, katika wahudumu wake  na washiriki wake, ni mshirika asili wa wito wa kuzaliwa kwa ubinadamu maskini na mvumilivu; kwa sababu wokovu wa wote ni utume wake, na kwa sababu kila mtu anahitaji kuokolewa; lakini upendeleo wake ni kwa wale ambao wanahitaji, hata katika uwanja wa muda, kusaidiwa na kutetewa. Mahitaji ya mwanadamu ni jina kuu la upendo wake”.

Sehemu ya Mahubiri ya Papa Paulo VI 16 Mei 1971
08 May 2021, 15:49