UCHUMI WA HONG KONG UCHUMI WA HONG KONG 

Vatican yazindua mikutano 3 kabla ya Mkutano Mkuu wa UN kuhusu Mifumo ya chakula

Umezinduliwa mfululizo wa mkutano kwa njia ya mtandao kuhusu "Chakula kwa ajili ya maisha,haki ya Vyakula na Chakula kwa Wote" katika matazamio ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo ya vyakula 2021 ili kufikia Maendeleo endelevu (SDGs) ya kukomesha njaa kufikia 2030.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika mwanga wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo ya Vyakula kwa 2021, Katibu wa Vatican, Utume wa Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Fao, Ifad na Pam, Baraza la Kipapa la Maendeleo ya Fungamani ya Binadamu na Tume ya Vatican dhidi ya COVID-19 pamoja na washirika ambao wanafanya kazi katika uwanja wa usalama wa vyakula, wamezindua mfululizo wa mikutano kwa njia ya mtandao inayoongozwa na mada: “Chakula kwa ajili ya Maisha, Haki ya Vyakula, Chakula kwa Wote”.

Kwa kuongozwa na Waraka wa Laudato si wa Papa Francisko, mikutano hii inataka kuonesha jinsi ambavyo Ekolojia Fungamani, inafanana na kile ambacho kinafikiriwa kuunganisha kwa pamoja kati ya mambo mengi ya watu, kati ya mifumo ya kijamii na kiuchumi kijamii  na inaweza kweli kuungizwa na kuzaliwa mifumo mipya ya vyakula katika wakati ujao baada ya COVID.  Mikutano inataka kubainisha jinsi ambavyo Kanisa na washirika wengine wanaweza kweli kuchangia katika mabadiliko ya mifumo ya chakula kuelekea utunzaji bora wa nyumba yetu ya pamoja na kuondoa kabisa njaa, kulinda na hadhi ya kibinadamu na huduma ya wema wa pamoja kwa namna ya kwamba hakuna yoyote anabaki nyuma

Mfululizo wa mikutano hii ina sehemu tatu ambao zinatarajiwa kufanyika katika 'Wiki ya Laudato Si' ambayo imeanza tarehe (16-24 Mei 2021), ili kusaidia kutoa sauti za wanawake, jumuiya za watu asilia, watu ambao wanaishi katika hali ya mgogoro, wakulima wadogo na wengine, kwa lengo la kujifunza kutokana na uzoefu wao na hakima yao ya kiutamaduni na kuunda mijadala ulimwenguni na mipango ya matendo madhubuti.  Mkutano wa kwanza kwa njia ya mtandao ni Jumatatu tarehe 17 Mei 2021 ambao ni kama Jukwa la Roma, likiongozwa na mada ya Chakula kwa ajili ya Maisha: Nafasi ya wanawake katika kuhamasisha maendeleo ya kibinadamu fungamani,  wenye tabia ya mazunguzmo juu ya nafasi moja ya wanawake katika maendeleo kwa namna  ya pekee umakini ulimwengu mzima.

Mkutano wa pili kwa njia ya mtandao utaongozwa na mada ya Vyakula: kazi, ubunifu na fedha katika huduma ya haki ya vyakula” ambao utafanyika tarehe 26 Mei 2021 saa nane mchana hadi saa 11 jioni, ukisisitiza umuhimu wa kazi yenye hadhi, katika kujenga upya mifumo ya vyakula endelevu, kwa namna ya pekee kwa wakati ujao baada ya –COVID. Mkutano wa mwisho utakaoandaliwa na   Taasisi ya kipapa la Elimu ya Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Sayansi kijamii kwa kuongozwa na kauli mbiu: “chakula kwa wote: migogoro ya vyakula na mifumo ya vyakula ijayo”, utafanyika tarehe 31 Mei saa 8.00 mchana hadi saa 10 jioni, ambao utaweza kuvumbua majibu juu ya migogoro ya chakula na jinsi gani Kanisa linaweza kufanya vizuri kuchangia na kushirikiana kwa ajili ya kikabiliana na njaa, na ukosefu wa usawa wa vyakula duniani.

Kwa kuongozwa na mada  ya Mafundisho jamii ya Kanisa, kutoka katika uzoefu wa kila siku wa wahudumu wa Kanisa mahalia, shauku kimaadili ya kuondoa baa la najaa, mfululizo wa mikutano hii, unatazamia kwanza kusikiliza na kupyaisha mazungumzo ndani na nje ya Kanisa. Pili, kuwasiliana na mazoezi bora katika ulimwengu ambayo yanahamasisha mifumo ya vyakula endelevu, na tatu kuinua sauti za kitumaduni ambazo zimebaguliwa ili kusikiliza wito wa haki wa vyakula.

Mfululizo wa mikutano hii utahitimisha kabla ya Mkutano wa kwanza wa Mifumo ya Vyakula wa Umoja wa Mataifa (UN), ambao unatarajiwa kufanyika jijini Roma kuanzia Julai 2021 katika muktadha wa matazamio ya kufikia hatua ya maendeleo endelevu (SDGs) ya kukomesha baa la njaa kufikia 2030. Hata hivyo matokeo yake yatashirikishwa kama sehemu ya mchakato wa Wakuu ili kuchangia kuongoza matendo binafsi na pamoja kuelekea katika wakati ujao wa vyakula ambavyo viwe endelevu, sawa na salama.

16 May 2021, 17:16