Papa Francisko amekutana na Rais wa Shirikilisho la Uswisi
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.
Katika siku ya kuapishwa kwa Walinzi wa Uswisi, Alhamisi asubuhi tarehe 6 Mei 2021 jijini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Shirikisho la Uswisi, Bwana Guy Parmelin. Wakati wa mkutano wao, kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari wamekumbushana kuhusu huduma ya ukarimu ya Walinzi wa Kipapa wa Kiswisi. Kwa njia hiyo, pua uhusiano mzuri na ushirikiano uliopo na wenye matunda kati ya Vatican na Shirikisho la Uswisi hasa kwa kutazama masuala makuu ya kimataifa na maeneo yenye masilahi ya pamoja katika mwaka wa mia moja tangu kuanza tena kwa uhusiano wa kidiplomasia.
Mara baada ya mkutano huo pia Rais wa Shirikisho la Uswisi amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.