Wakristo wanaongezeka ulimwenguni Wakristo wanaongezeka ulimwenguni 

Wakatoliki wanaongezeka ulimwengu na pia mashemasi

Imetolewa takwimu ya Kanisa kuhusu idadadi ya wakatoliki ambapo wanasema kati ya mwaka 2018 na 2019 wabatizwa ni 17,7% ya watu wote ulimwenguni.Na wakati huo huo katika kipindi hicho kinaona ongezeko la makuhani lakini kwa kupungua waseminari,watawa kike na kiume.Idadi ya mashamasi wa kudumu pia inaongezeka kwa kiasi kipatao karibu 50,000.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tangu 2018 ulimwenguni unahesabiwa milioni 16 ya wakatoliki kuongezeka zaidi. Ni taarifa ya mwaka 2021 ya Kipapa na Takwimu za Mwaka za Kikanisa za 2019 zilizoandaliwa na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Kanisa na kuchapishwa katika chapisho la Vatican na  siku hizi kuwa katika maduka ya vitabu. Kuna Wakatoliki bilioni moja na 345 milioni waliosajiliwa mwishoni mwa 2019, sawa na 17.7% ya idadi ya watu ulimwenguni. Uchambuzi wa kijiografia wa mabadiliko katika kipindi cha miaka miwili 2018-2019 unaoneesha kuongezeka kwa 3.4% barani Afrika, 1.3% huko Asia, 1.1% huko Australia na 0.84% ​​huko Amerika, wakati Ulaya inashuhudia kupungua kidogo. Katika nakala 3,026 za Kikanisa, mwishoni mwa 2019 kulikuwa na maaskofu 5,364, huko Amerika na Ulaya zikiendelea kuwakilisha 68.8% ya jumla yote ulimwengu, ikifuatiwa na Asia (kwa 15.2%), Afrika (13.4%) na Australia (2.6%) . Wakati, mwishoni mwa 2020, katika shajara la Kipapa linaonesha kuchaguliwa viti 2 vya majimbo makuu   na viti 4 vya uaskofu (yaani majimbo 2 na parokia 2) kwamba maparokia hayo  yameinuliwa kuwa majimbo makuu 2 na nafasi mbili za kitaifa na 1 ya uwakilishiwa  kitume katika jimbo.

Ongezeko la makuhani lakini miito michache

Idadi ya makuhani iliongezeka katika kipindi cha miaka miwili 2018-2019; kwa jumla kuna 414,336, 271 zaidi. Dhidi ya ongezeko muhimu kwa Afrika na Asia, na ongezeko kidogo la 3.45% na 2.91%, huko Uropa na Amerika kuna kushuka kwa 1.5% na takriban nusu ya asilimia. Afrika na Asia kwa pamoja wanahesabu 28.9%, wakati Oceania inabaki imara karibu na sehemu ya zaidi ya 1.1%. Ulaya inapunguza asilimia yake kwa kiasi kikubwa: mnamo 2018 makuhani wa Ulaya 170,936 waliwakilisha karibu 41.3% ya jumla ya kikundi cha kikanisa, wakati mwaka mmoja baadaye walishuka hadi 40.6%. Miito ya ukuhani bado inapungua: wagombea wa ukuhani katika sayari hiyo kutoka 115,880 mnamo 2018 hadi 114,058 mnamo 2019, na kushuka kwa 1.6%. Huko Ulaya tofauti ni 3.8%, Amerika -2.4%, na Asia -2.6%. Lakini barani Afrika idadi ya seminari seminari Kuu, tena katika kipindi cha miaka miwili inayotangulia, iliongezeka kutoka 32,212 hadi vitengo 32,721, wakati huko Australia mnamo 2019, ilikuwa chini ya 5.2% kuliko mwaka uliopita. Bara lenye idadi kubwa ya waseminari ni Asia (33,821), ikifuatiwa na Afrika (32,721), Amerika (30,664), Ulaya (15,888) na Australia (964). Idadi ya mashemasi wa kudumu, kwa upande mwingine, inaendelea kuoneesha nguvu kubwa na inayotia moyo wa mabadiliko: waliongezeka kwa 1.5% mnamo 2019. Kati ya mashemasi 48,238 katika mabara 5, 1.2% zaidi wameorodhesha Amerika na Ulaya, wakati Australia kuna 481.

Kupungua kwa watawa

Idadi ya watawa waliofunga nadhiri ambao sio makuhani pia imepungua; mnamo 2018 walikuwa 50,941, mnamo 2019 wanakuwa 50,295. Ulaya na Amerika, kama ilivyokuwa 2019, ambayo daima ni maeneo yenye idadi kubwa zaidi ya watawa wasio kuwa makuhani, ambao ni 14,038 na 13,735. Watawa hata hivyo wa nadhiri wamepungua sana. Kwa upande wa ulimwengu, imepita kutoka 641, 661 mnamo 2018 hadi 630,099 mnamo 2019, na kupungua kwa 1.8%. Wakati Afrika ndilo bara lenye ongezeko kubwa zaidi, na + 1.1% - hasa kutoka 76,219 watawa, hadi mnamo 2018, na   77,054, hadi mnamo 2019, na Asia ya Kusini-Mashariki inasajili ongezeko la 0.4% (kutoka 170,092 hadi 170,754 watawa), maeneo matatu ya bara yaliyosalia yanashirikiana sana. Huko Amerika watawa waliongezeka kutoka 160,032 hadi 154,717, huko Ulaya kutoka 224,246 hadi 216,846 na Australia kutoka 6,999 hadi 6,718.

27 March 2021, 16:10