Sr. Smerilli ni Katibu Maidizi wa Maendeleo Fungamani ya Binada
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amemteua Katibu Msaidizi wa Kitengo cha Imani na Maendeleo cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu, Sr. Alessandra Smerilli, F.M.A., Mwanashirika wa Mabinti wa Mama Maria Mwombezi wa Don Bosco, ambaye ni Profesa wa kawaida wa Uchumi wa sera za kisasa katika Chuo Kikuu cha Elimu ya Sayansi cha Roma.
Sr. Alessandra Smerilli, F.M.A., alizaliwa mnamo tarehe 14 Novemba 1974 huko Vasto (CH), Italia. Alipata shahada ya udaktari wa Uchumi wa siasa katika Kitengo cha Uchumi cha Chuo Kikuu La Sapienza Roma. Baadaye aliendelea na masomo ya stashahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Anglia Mashariki ya Nowrich nchini Uingereza.
Pamoja na hayo, amekua akijitoa katika jitihada za Kanisa ambalo lilimpelekea kuwa sehemu ya Kamati ya Sayansi na mratibu wa Wiki za kijamii za Wakatoliki na tangu 2019 amekuwa mshauri wa Vatican vile vile tangu Machi 2020 mratibu wa Kikosi Kazi cha Uchumi cha Tume ya Vatican ya Covid-19, iliyoanzishwa na Papa Francisko. Miongoni mwa vitabu vyake alivyoandika ni: Mwanamke mchumi. Kutoka katika mgogoro msimu mpya wa matumaini”.
Akihojiwa na Vatican New, kuhusiana na uteuzi huo anasema alivyoshangaa kidogo na uteuzi kwa sababu amesema kwamba alikuwa amekuja kufanya kazi hapo katika ukumbi wa wakala kama mshirika wa Tume ya Covid-19. Alidhani ni kazi ya muda mfupi lakini kadiri ya siku ndivyo imeleta mshangao huo. Katika kufanya kazi hapo amegundua ni jinsi utume huo ulivyo mzuri wa Baraza hilo na jinsi gani linavyofikia ulimwengu wote. Yeye anahisi kutoa shukrani kwa Baba Mtakatifu na kwa Rais wa Baraza lake hilo, Kardinali Peter Turkson, aidha kwa wale wote wanaofanya kazi katika Baraza la Kipapa hilo ambao wameonesha kupendezwa na kumwamini. Anatumainia kuwa ataweza kufanyanao katika sehemu yake ipasavyo.