Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Mosul,kuponesha majeraha&kuimarisha imani

Katika siku ya tatu ya Ziara ya Papa amekwenda Mosul mahali ambapo amesali kwa ajili ya waathiriwa wa vita na Qaraqosh,kukumbatia jumuiya ya Wakristo.Na hatimaye baada ya mchakato wake wa maeneo ya kishahidi amerudi Erbil kwa ajili ya Misa katika Uwanja wa michezo wa “Franso Hariri.Video fupi inaonesha kufika kwa Papa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Katika ziara hii ya 33 za Kitume ya Papa Francisko katika ardhi ya Ibarahimu, siku ya tatu, hatua ya kwanza ilikuwa ni Erbil, ambao ni mji mkubwa wa Mkoa unaojitigemea wa Kurdistan -Iraq, baadaye amekwenda Mosul mahali ambapo amesali kwa ajili ya waathiriwa wa vita na Qaraqosh, kukumbatia jumuiya ya Wakristo. Video fupi inaonesha kwa ufupi kufika kwake. Na hatimaye baada ya mchakato wake wa maeneo ya kishahidi amerudi Erbil kwaajili ya Misa katika Uwanja wa michezo.

UWANJA WA MCHEZO HUKO ERBIL
UWANJA WA MCHEZO HUKO ERBIL

Kati ya vifusi, ambapo kama ilivyojiita serikali ya Kiislamu  lilipanda giza la kifo na hofu, Papa hapo ameleta nuru ya imani na matumaini. Huko Mosul ni ktafuta ujenzi wa majengo na mioyo, Papa Fransisko ameomba msamaha wa Mungu na neema ya uongofu huku akioneesha kuwa njia ni kutekeleza mpango wa upendo na amani ambayo Bwana anayo kwa mwanadamu. Njia iliyooneshwa na matumaini kwamba uzoefu wa ushirikiano wa kindugu kati ya Wakristo na Waislamu unaleta ushuhuda, mambao ambayo yamesimuliwa mbele ya Papa.

SALAMU KWA PAPA
SALAMU KWA PAPA

 

 

07 March 2021, 14:41