Askofu Dieudonne Watio wa Jimbo Katoliki la Bafoussam tarehe 19 Machi 2021 ameng'atuka kutoa madarakani. Askofu Dieudonne Watio wa Jimbo Katoliki la Bafoussam tarehe 19 Machi 2021 ameng'atuka kutoa madarakani. 

Askofu Dieudonnè Watio Jimbo la Bafoussam Ang'atuka Madarakani

Askofu Dieudonné Watio wa Jimbo Katoliki la Bafoussam alizaliwa tarehe 18 Machi 1946 huko Mbouda nchini Cameroon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Julai 1975 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Aprili 1995 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nkongsamba na kuwekwa wakfu tarehe 10 Juni 1995.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake la kutaka kung’atuka kutoka madarakani na Askofu Dieudonné Watio wa Jimbo Katoliki la Bafoussam, nchini Cameroon. Itakumbukwa kwamba, Askofu Dieudonné Watio wa Jimbo Katoliki la Bafoussam alizaliwa tarehe 18 Machi 1946 huko Mbouda nchini Cameroon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Julai 1975 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 1 Aprili 1995 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nkongsamba na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Juni 1995. Ilipogota tarehe 5 Machi 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bafoussam, nchini Cameroon na hatimaye, akastaafu rasmi kama Askofu tarehe 19 Machi 2021. Amelitumikia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 45. Akawaongoza, akawafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu nchini Cameroon kama Askofu kwa muda wa miaka 25 na kwa sasa ameng’atuka, lakini anaendelea kuwahudumia watu wa Mungu nchini Cameroon katika huduma za kikuhani!

Cameroon
20 March 2021, 10:34