Askofu Daniel Nlandu Mayi wa Jimbo Katoliki la Matadi DRC ameng'atuka kutoka madarakani kwa ridhaa ya Baba Mtakatifu Francisko. Askofu Daniel Nlandu Mayi wa Jimbo Katoliki la Matadi DRC ameng'atuka kutoka madarakani kwa ridhaa ya Baba Mtakatifu Francisko. 

Askofu Daniel N. Mayi Ang'atuka Kutoka Madarakani Matadi, DRC.

Askofu Mstaafu Daniel Nlandu Mayi alizaliwa tarehe 19 Oktoba 1953 huko Kinshasa. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 20 Aprili 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 29 Oktoba 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Matadi na kuwekwa wakfu tarehe 30 Januari 2000. Na tarehe 6 Machi 2021 akang'atuka madarakani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Daniel Nlandu Mayi wa Jimbo Katoliki la Matadi, nchini DRC la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mstaafu Daniel Nlandu Mayi alizaliwa tarehe 19 Oktoba 1953 huko Kinshasa. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 20 Aprili 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 29 Oktoba 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Matadi na kuwekwa wakfu tarehe 30 Januari 2000.

Tarehe 11 Novemba 2008 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mwandamizi mwenye dhamana ya kurithi Jimbo. Hatimaye, tarehe 21 Septemba 2010 akasimikwa rasmi kuwa ni Kiongozi mkuu wa Jimbo Katoliki la Matadi. Amewatumikia watu wa Mungu nchini DRC kama Padre kwa muda wa miaka 40. Amewaongoza, akawatakatifuza na kuwafundisha watu wa Mungu Jimbo Katoliki la Matadi, DRC kwa muda wa miaka 21. Sasa anapumzika na kujiandaa na awamu nyingine ya maisha!

Jimbo la Matadi
13 March 2021, 14:05