CHANJO DHIDI YA COVID-19 INAENDELEA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI CHANJO DHIDI YA COVID-19 INAENDELEA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI 

Jurkovič kwa Unctad:baada ya Covid kuna hitaji la kuzindua ujumuishwaji kimataifa!

Akihutubia katika mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa UN kuhusu Biashara na Maendeleo,uliopangwa kufanyika Aprili huko Barbados,Mwakilishi wa Vatican amerudia kusisitiza hitaji la kuzindua kwa upya ujumuishwaji kimataifa ili kuunda sura tofauti ya maendeleo baada ya Covid.

Na Sr. Angala Rwezaula – Vatican.

Kufufua ushirikiano wa kimataifa kati ya mataifa, unaozingatia na kuheshimu haki sawa na kujitawala kwa watu, katika roho ya Mkataba wa Umoja, ndiyo njia  ya kufanikiwa kukabiliana na changamoto mpya iliyo ngumu ambayo ulimwengu unakabiliwa nayo baada ya COVID-19. Haya yemesititizwa na Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswiss.  Kiongozi huyo amezungumza hayo siku ya Jamatatu tarehe 22 Februari 2021 katika  mkutano wa Kamati ya Maandalizi ya kikao cha 15 cha mawaziri cha “Mkutano wa UN wa Biashara na Maendeleo (Uctad XV)”. Kikao hicho, kilichokuwa kimepangwa kufanyika Oktoba 2020, kwa sasa kitafanyika tangu tarehe  25 hadi 30 Aprili 2021 huko Barbados kwa kuongozwa na kaulimbiu: “Kutoka katika ukosefu wa usawa na mazingira magumu hadi kufanikiwa kwa wote”.

Ni katika lengo la kufikia  Ajenda ya Maendeleo Endelevu la 2030 katika mwanga wa athari kubwa ya Covid-19, juu ya uchumi ulimwenguni kote. Kitovu cha majadiliano kitakuwa ni mikakati na sera za kisiasa zinazohitajika kuzisaidia nchi ili kuvumilia na kushinda vema katika wakati mgumu kama huu wa janga kwa matazamio ya siku zijazo na kupona haraka kutokana na mzozo wa kiuchumi, kifedha, hali ya hewa na kijamii.

Hayo ni malengo ambayo yanaungwa mkono na Vatican na ambayo wakati huo huo, anasisitiza umuhimu wa kungeza ushirikiano kati ya Mataifa, katika wakati ambao upendeleo wa kimataifa unajaribiwa kwa ugumu zaidi.  Mantiki tofauti ya shida hizi zisizotabirika, suluhisho zake na maendeleo yoyote mapya ambayo siku za usoni zinaweza kuleta, zinazidi kuunganishwa na kutegemeana, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Jurkovič katika hotuba yake. Hii ndiyo sababu Familia ya Mataifa inaitwa kutafakari kwa upya njia yake, ili kugundua aina mpya za kujitolea kwa uwajibikaji ameongeza. Kwa njia hiyo mgogoro unakuwa fursa ya kugundua jinsi ya kuunda maono mapya muhimu ya siku zijazo.

Kulingana na Vatican rasimu ya kwanza ya hati ya kazi ya Mkutano uliowasilishwa mwezi Desemba iliyopita inatoa msingi thabiti kwa maana hii. Miongoni mwa hoja zake muhimu, ni kutilia mkazo mipaka ya dhana ya maendeleo ya sasa, ambayo ilijitokeza katika ushuhuda wao wote hasa wakati wa mgogoro wa Covid-19, ambao  kwa mujibu wa mwakilishi wa Vatican  amesema umetumika  na kukubusha ukweli wa   hali  halisi ambayo inategemeana ulimwengu na kwa hiyo kuna hitaji la hatua ya pamoja ya kuwajibika na kuwa na maono ya mbali kwa pamoja.

Sio hayo tu, mgogoro huo pia umeangazia ni kwa kiasi gani mazingira, maendeleo na usalama vimeunganishwa. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Jurkovič, hati ya mwisho ambayo Unctad inajiandaa kujadili katika miezi ijayo inatoa fursa ya kipekee ya kuandaa majibu madhubuti katika matokeo ya kiuchumi ya Covid-19, ili mradi lengo sio tu juu ya hatua za uchumi, lakini pia ziwe kwenye mfululizo sera za kurekebisha michakato ya maendeleo ambayo ni sawa, fungamani  na inayoheshimu hali ya tabianchi.

22 February 2021, 16:45