Amanda Gorman wakati wa afla ya kiapo cha Rais Joe Biden wa Marekani  (AFP or licensors) Amanda Gorman wakati wa afla ya kiapo cha Rais Joe Biden wa Marekani (AFP or licensors) 

Amanda Gorman:Shairi ni lugha ya mapatano

Mwana mashairi kijana msichana wa Marekani ambaye alivutia Marekani kwa na shairi lake alilosoma wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Rais Joe Biden, anafakari na vyombo vya habari Vatican juu ya umuhimu wa elimu,nguvu ya mashairi na harakati zinazoanzishwa kutokana na kujitoa kwa vijana wanawake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Pamoja na mashairi yake, vyombo vya habari Marekani vilidai, kama kwamba aliweza kuiba nafasi ya onesho la Rais Joe Biden. Akiwa na umri wa miaka 22 tu, Amanda Gorman ni mwanamashairi mdogo zaidi aliyeweza kutumbuiza shairi lake wakati wa kuapishwa kwa Rais wa Marekani shairi likiongozwa na mada “The Hill We Climb”, yaani “Kilima tunachopanda”. Kijana huyo Mmarekani wa kiafrika na mkatoliki aliweza kusisimua Marekani na ulimwegu kwa kuonesha ndoto inayowezekana ya ubinadamu ulioponywa na ambaye anapata tumaini katika uchungu na kuthibitisha kwamba hawezi kukaa bila kuwa shuhuda wa migogoro na mafarakano. Katika mahojiano haya na vyombo vya habari Vatican, Amanda amethibitisha juu ya nguvu ya mashairi kama njia ya upatanisho katika wakati uliogandishwa na zaidi kusisistiza dharura wa kuwekeza katika elimu ili kubadilisha ulimwengu na kutoa maisha bora ya kizazi cha vijana kijacho.  Yafuatayo ni mahojiano yaliyofanywa na Na Alessandro Gisotti wa Vatican News na Amanda.

Papa Francisko katika matukio mengi amesisitiza kwa kiasi gani ni muhimu kujenga madaraja, mazungumzo na kufanya kazi kwa ujasiri kwa upatanisho. Je! Unafikiri mashairi yanaweza kusaidia kuponya vidonda ambavyo vinagawanya ulimwengu wetu?

“Ndio kabisa. Mashairi ni lugha ya upatanisho. Mara nyingi hutukumbusha namna yetu ya kuwa bora na maadili yetu ya kawaida. Huu ndio ulikuwa uzoefu ambao ulinitia msukumo wakati wa kuandika “The Hill We Climb”, “ Kilima tunacho panda”, kiukweli  nikijiuliza: Je! Shairi hili linaweza kufanya nini, sasa na baadaye, mahali ambapo nadharia haiwezi kufanya?  Kuna nguvu maalum katika mashairi ya kutakasa, kusafisha na kuweka sawa, hata katikati ya mafarakano”.

Mashairi wakati mwingine uhusishwa na wasomi au kitu kwa ajili ya watu wa umri fulani. Je! Unaweza kuwambia  nini  vijana ambao wamevutiwa na mashairi yako na wanasifu umri wako mdogo?

“Ni jambo la kusikitisha kuwa mashairi mara nyingi hufundishwa mashuleni kana kwamba ni haki ya wasomi wa zamani, wasio na kazi, marehemu, wazungu na wanaume tu, wakati ukweli mashairi ni lugha ya watu. Ninaweza kuwambia  vijana kuwa mashairi ni mahiri na yanabadilika kila wakati, na sanaa hiyo ni yetu sote, sio ya kikundi teule. Ninapenda kusema kuwa tunahitaji sauti zenu, tunahitaji historiazenu, kwa maana hiyo msiogope kuchukua kalamu mikononi!

Malala, Greta Thunberg, na sasa Amanda Gorman: katika miaka ya hivi karibuni tumeona wasichana wengi wakijitokeza kama viongozi wa harakati ambazo zinatoa changamoto kwa wenye nguvu duniani. Je! Unafikiri hii inaashiria mabadiliko ya kudumu?

“Nadhani tunaona wazi viongozi wanawake vijana wakipata ushindi kwa kiwango cha ulimwengu kwa sababu hii, inawakilisha jambo kubwa zaidi ulimwenguni: vijana, hasa wanawake vijana  ulimwenguni kote wako wanainuka na kuchukua nafasi zao katika historia. Kwa kila Amanda, kuna wengine wengi kama mimi. Ninaweza kuwa wa kipekee, lakini siko peke yangu kabisa. Ulimwengu utatikiswa na kubadilishwa na kizazi kijacho na ni wakati sasa wa kuwasikiliza.

Ukiwa mtoto mdogo ulikuwa na shida ya kuongea ambayo uliishinda, na leo ulimwengu unakupenda  kwa ufasaha wako. Je! Kwa maoni yako, ni kwa jinsi gani elimu ni muhimu sana kubadilisha ulimwengu wetu?

“Elimu ni kila kitu. Mimi ni mtoto wa mwalimu na hivyo daima nimekuwa nikijali masomo yangu kwa uzito. Nilielewa nikiwa bado na umri mdogo kuwa maarifa ni nguvu. Kwa watu waliotengwa, inaweza kuwa moja ya zana muhimu zaidi katika ‘sanduku la zana zetu’. Ili kubadilisha ulimwengu, lazima kuiweka katika majadiliano na lazima tujiulize; tupanapaswa kuzingatia historia nzima na tuone jinsi inavyohusiana na wakati wa sasa. Sina shaka kwamba harakati nyingine kubwa za kijamii zitaanzia katika chumba cha shule.

MAHOJIANO NA AMANDA GORMAN
13 February 2021, 16:30