CHRISTMAS-SEASON/IRAQ Mwanamke nchini Iraq akisali CHRISTMAS-SEASON/IRAQ Mwanamke nchini Iraq akisali 

Kard.Parolin:Safari ya Papa nchini Iraq ni kuwatia moto wakristo!

Katika mahojiano ya na kituo cha matangazo ya Televsheni katoliki ya Ufaransa(Kto),Katibu wa Vatican amejitika kuelezea juu safari ya Papa Francisko nchini Iraq.Amegusia hata mada nyingine kama vile mageuzi ya Vatican,mkataba wa China na kuhusu mgogoro wa kiafya unaohusiana na janga la sasa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Juhudi za Kanisa ni zile za kuwa na uwezo leo hii wa kutangaza Injili kwa watu katika wakati wetu. Kanisa linalotoka nje ni Kanisa lenye uwezo wa kweli wa kupeleka maji safi ya Injili kwa watu leo hii ambao wana kiu ya maji haya, hata kama labda wanafikiri kuwa hawana haja nayo. Ndivyo alivyothibitisha Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, wakati wa mahojiano yaliyotangazwa mchana tarehe 29 Januari  2021 katika televisheni ya kifaransa (Kto). Akijibu swali kuhusu mageuzi ya Vatican, Kardinali amesisitiza kuwa zimepigwa hatua muhimu. Hata hivyo amesema mageuzi yalikuwa tayari yamefanya hasa kwa kile kinachotazama upande wa uchumi. Katibu wa Vatican amekumbuka kuwa vimeundwa vyombo vitatu: Baraza la Uchumi, Sekretarieti ya Uchumi, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.

Hadi sasa hatua kubwa imefanywa ya mageuzi

Kumekuwa pia na mageuzi makubwa ya sekta ya mawasiliano kwa kuanzishwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Halafu amekumbusha kuwa kumekuwa na kuunganisha baadhi ya mabaraza ya kipapa kwa mfano, Mabaraza manne ya Kipapa yameunganishwa pamoja na kuunda Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu. Kwa maana hiyo sehemu kubwa ya kazi imefanywa na sasa  kuna hatua nyingine za kuchukua. Lakini ni hatua ndogo ukilinganisha na ile ambayo tayari imekamilika, amesisitiza Kardinali Parolin.

Kanisa lazima lielekeze katika Injili

Akizungumzia tena juu ya mageuzi hayo, Kardinali amesema kuwa  hili ni suala  la kutoa sura ya umoja  kwa hatua zote zilizochukuliwa kupitia Katiba mpya ya Kitume ambayo imepewa jina la muda  “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” na ambayo inapaswa kuchapishwa mwaka huu. Kichwa cha muswada  wa muda, tayari kinaonesha mtazamo ambao walifanya kazi kwa ajili ya mageuzi ya Vatican iliyokabidhiwa kwa  Baraza la Makardinali, ambao ni washauri wa Papa. Hii inakwenda sambamba na kile ambacho Papa anasema katika Wosia wa Kitume wa “Evangelii Gaudium”, kwamba kila kitu katika Kanisa lazima kitazamwe kwa upya na kuelekezwa kutangaza Injili. Kwa maana hiyo Baraza zima la Roma  kama muundo unaomsaidia Papa katika kutekeleza utume wake kama Mrithi wa Petro, lazima uwe na mwelekeo huo. Kardinali Parolin pia amesisitiza kwamba, Baba Mtakatifu alipendelea kukabiliana moja kwa moja na matatizo ambayo yamejionesha hasa kwa  kuifanya Baraza zima la  Roma liweze kuwa wazi zaidi iwezekanavyo.

Safari ya Papa nchini Iraq

Kardinali Parolin katika mahojiano hayo pia amejikita kutazama hali halisi ya wakristo wa Nchi za Mashariki na zaidi juu ya Ziara ijayo ya Papa Francisko, inayotarajiwa kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 nchini Iraq. “Licha ya matatizo ambayo katika ziara hiyo yanawezekana kutokea, Papa Francisko anapendelea kwenda katika Ghuba hiyo, hasa kwa ajili ya kuwatia moyo wakristo”. Katika Nchi nyingi kikanda zimerekodiwa idadi kubwa ya wakristo wahamiaji kwa sababu ya migogoro na vurugu. Katika ardhi zile,Jumuiya ya wakristo imepungua sana. Kwa maana hiyo Papa anahisi kwa dhati hitaji la kwenda na kuwapa moyo wakristo hao, kuwaalika waendelee kutoa ushuhuda wao licha ya matatizo, amethibitisha Kardinali Parolini. Mada nyingine katika ziara hiyo ni mazungumzo ya kidini. Kwa maana hiyo Kardinali amesisitiza kuwa ziara ya Papa nchini Iraq pia ni fursa ya kuwatia moyo ili wafanya mageuzi ya kisiasa na kuimarisha Nchi.

Udugu kibinadamu

Mada nyingine katikati ya mahojiano hayo ilihusu Hati juu ya Udugu wa kibinadamu, iliyosainiwa na Papa Francisko na  Imam Mkuu wa Al-Azhar mnamo tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi. Kwa njia hiyo Kardinali amesema kwamba haya ni maendeleo makubwa katika uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu. Katika hati zinashirikishwa kanuni nyingine msingi kwa sababu kwamba  sisi sote ni viumbe wa Mungu na  lazima itufanye tuhisi kuwa ndugu zaidi. Lakini pia inatambuliwa ukweli kwamba hakuna vurugu inayoweza kuhesabiwa haki kwa jina la Mungu. Kardinali pia amekumbusha mchango ambao dini zinaweza kuleta katika ujenzi wa ulimwengu ulio na haki zaidi na umoja. “Katika Hati juu ya Udugu wa kibinadamu imeandikwa kwa rangi nyeusi na nyeupe kuwa kuna mapenzi hayo”. Mipango mingi imeanzisha  na inaendelea kuanzishwa kutokana na maandishi hayo hasa  kwa ngazi ya elimu.

Kuangazia dhamiri

Kanisa halina jukumu la kisiasa. Kwenye masuala makuu ambayo yanashirikisha jumuiya ya kimataifa, kama vile suala la uhamiaji na mabadiliko ya tabianchi, jukumu lake ni kuangaza dhamiri. Utume wa Kanisa wakati mwingine unaweza kugongana hata na fikira kuu. Vatican katika muktadha wa kimataifa, inajaribu kuwafanya watu watafakari juu ya matokeo ya chaguzi fulani. Lengo ni kumfanya kuelewa mhusika kwamba kusudi la Kanisa ni kuokoa hadhi ya mtu, amebainisha Kardinali Parolin.

Mkataba wa Vatican na China

Akijibu swali kuhusu Mkataba wa muda wa Vatican na Jamhuri ya Watu wa China, Kardinali Parolin amesema kwamba imechaguliwa njia yenye hatua ndogo. Makubaliano haya yasingeweza kutatua shida zote zinazolikabili Kanisa nchini China, lakini ni hatua ndogo tu ambayo ni kuanzia na kujaribu kuboresha hali hiyo. Mkataba huo kwa namna hiyo hauna madai ya kuwa neno la mwisho. Ni mbegu ndogo ambayo imewekwa duniani. Matumaini ni kwamba inaweza kukua na kuzaa matunda lakini inahitaji uvumilivu mwingi, amethibitisha Kardinali Parolin.

Utamaduni wa kutunzana

Mwaliko ambao unatolewa katika  Kanisa ili kukamilisha  na kutatua hali ya janga la sasa  la corona ni kuzingatia utamaduni wa utunzaji wa pamoja. Kardinali Parolin amesema, “hatupaswi kupoteza tumaini, vinginevyo upeo wote umefungwa. Sisi sote tuko kwenye mtumbwi mmoja na tuna hatima ya pamoja. Mbali na tumaini, ni muhimu kuchukua njia ya mshikamano. Sio kujifunga binafsi bali kutunza kila mmoja”. Na hatimaye Kardinali Parolin amekumbusha kuwa “Tunahitaji kuwa na imani kwamba chanjo itatusaidia kutoka kwenye mgogoro huu”.

30 January 2021, 17:23