2020.09.16 mons. Janusz S. Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika OSCE 2020.09.16 mons. Janusz S. Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika OSCE  

Mons.Urbańczyk kwa Osce:kuhamasisha nafasi ya wanawake na haki za kimataifa

Mazungumzo na heshima ya haki za kimataifa ndizo zana kwa ajili ya suluhisho la migogoro,ambayo amekumbusha Monsinyo Janusz Urbańczyk wakati wa hotuba yake kwenye mkutano wa Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo Barani Ulaya,OSCE.

Na Sr. Angela Rwezaula,- Vatican.

Kujaribu kutiana moyo Mataifa yote wanachama katika kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya amani na haki, na wakati huo huo kukazia jitihada ambazo wamejiwekea, ndiyo msisitizo wake wakati wa hotuba yake Monsinyo Janus Urbańczyk Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika  Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo Barani Ulaya,(OSCE). Katika mchakato wa mkutano wao wa 1298 wa Baraza hilo, kwa namna ya pekee mwakilishi wa Vatican amekumbusha kuwa amani ya kweli na ya kudumu itawezekana tu kwa msingi wa maadili ya ulimwengu, ya ushirikiano katika huduma ya siku zijazo zinazojulikana na kutegemeana na uwajibikaji wa pamoja katika familia nzima ya wanadamu. Akirejea katika maadhimisho ya miaka 20, iliyofikia kilele chake tarehe 3 Oktoba 2020 ya kupitishwa kwa Azimio 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya wanawake, amani na usalama, Mwakilishi wa Vatican amesisitiza hitaji la kukumbuka wazi kile kisichoweza kubadilishwa cha mchango ambao wanawake wanautoa wakati wa upatanisho na ujenzi wa amani. Vatican  ameongeza kusema, bado inaendelea kuamini  juu ya hitaji la kuhamasisha jukumu la wanawake katika ngazi zote za kuzuia migogoro, usimamizi wa shida na utatuzi wa migogoro na michakato ya ujenzi wa maisha  baada ya vita

Haki zote za binadamu zilindwe kwa kipimo kilicho sawa

Jambo msingi pia alilosisitiza lilikuwa ni kutoa kipaumbele hasa kwa haki za binadamu, demokrasia na usawa wa kijinsia, kupitisha njia inayoheshimu kwa kipimo sawa cha haki zote za kibinadamu zinazotambuliwa ulimwenguni, ili kuepusha kuanzisha madaraka kati yao. Hii ni kwa sababu, alibainisha Mwakilishi wa Kudumu kuwa haki za binadamu hazipaswi kutumiwa kamwe kama njia ya kuendeleza ajenda ya kisiasa, kiuchumi, kijeshi, kitamaduni au kiitikadi, au kama maneno wazi ambayo wahusika tofauti wanaweza kubadilika kulingana na malengo yao. Kwa njia hiyo ni , matumaini ya Vatican kwamba nchi wanachama wa Ukanda wa OSCE zinaweza kuheshimu vigezo vya kutopendelea na weledi wa miundo yao ya utendaji, ili kutekeleza kazi na mipango  kufuatana na  ahadi zilizoaidhiwa, hasa katika muktadha wa usawa kati ya wanawake na wanaume.

Uvumilivu na kutobagua ni vipaumbele vya OSCE

Mwakilishi wa kudumu wa Vatican pia amekumbuka kanuni ya imani njema, ili kuhakikisha kwamba ahadi zilizopo hazibadilishwi kimsingi , kubadilishwa au kufutwa kwa njia ya tafsiri isiyofaa, kutokana na hatari ya sheria ya idhini ambayo inategemeana na Osce. Kwa kuongezea, kwa niaba ya Vatican, Mwakilishi wa Kudumu amehimiza urais ambao mwaka huu 2021 wanaoandaa  na kuongoza ni Sweden kuweka mada ya uvumilivu na ubaguzi juu ya ajenda yake, wakizingatia  kuwa ukosefu wa uvumilivu unazidi kukua na ubaguzi dhidi ya Wakristo, Wayahudi, Waislamu na washiriki wa dini nyingine. Kwa kifupi ni pendekezo ambalo limepitishwa katika njia ambayo inatambua upendeleo wa aina hizi za kutovumiliana na ubaguzi na kujibu mahitaji maalum ya jamuiya zinazohusika, bila kuonesha hukumu au upendeleo kati yao. Kwa njia hiyo, Monsinyo Urbańczyk amesema anaamini kuwa OSCE itaweza kujibu vyema changamoto juu ya usalama na usalama unaokabiliwa na jamuiya zote za kidini katika kanda yake.

Matendo ya pamoja dhidi ya janga yanahitajika

Hatimaye Mwakilishi wa kudumu ameshauri Mataifa Wanawachama kujikita katika matendo ya pamoja ya dhati mbele ya hatari za ulimwengu, pamoja na janga la Covid-19”, kwa namna ya kufanya OSCE yenye nguvu  zaidi, ikijiruhusu kuongozwa na uongozi wa utu wa kibinadamu na dira ya kanuni msingi za kijamii.

15 January 2021, 16:12