Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi, Kenya, tarehe 4 Januari 2021 ameng'atuka kutoka madarakani, baada ya Papa Francisko kuridhia ombi lake. Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi, Kenya, tarehe 4 Januari 2021 ameng'atuka kutoka madarakani, baada ya Papa Francisko kuridhia ombi lake. 

Kardinali John Njue, Jimbo Kuu la Nairobi, Ang'atuka Madarakani!

Kardinali Njue alizaliwa mwaka 1944. Tarehe 6 Januari 1973 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 9 Juni 1986 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Embu na kuwekwa wakfu tarehe 20 Septemba 1986. Tarehe 9 Machi 2002, akateuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Nyeri. Tarehe 6 Oktoba 2007 akateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya. Itakumbukwa kwamba, Kardinali Njue, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Nairobi, alizaliwa kunako mwaka 1944 huko Embu, Kenya. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 6 Januari 1973 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na Mtakatifu Paulo VI. Tarehe 9 Juni 1986 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Embu, Kenya na kuwekwa wakfu tarehe 20 Septemba 1986.

Ilipogota tarehe 9 Machi 2002, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Nyeri, Kenya. Tarehe 6 Oktoba 2007, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya na kusimwa rasmi kama Askofu Jimbo tarehe 1 Novemba 2007. Tarehe 24 Novemba 2007, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Kardinali na kusimikwa rasmi tarehe 17 Februari 2008. Kwa ufupi kabisa, Kardinali John Njue, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya, amewaongoza, kuwafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu kama Padre kwa muda wa miaka 47.99, na kama Askofu muda wa miaka 34.28 na kama Kardinali miaka 13.11.

Kardinali Njue

 

04 January 2021, 11:57